Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Upendo ni factor lakini tabia ya binadamu ni dynamic kuna serial killers waliopata kila kitu utotoni na bado waliturn out kua janga la jamii. Mfano wa haraka ni Ted Bundy, John Wayne Gacy na somebody Love.Hongera kwa mabandiko na ahsante kwa kutenga muda wako kushea nasi simulizi hizi.
Nilichojifunza ni kua japo serial/Psycho killer wengi hua na motive mbalimbali kwa mawazo yao zinazowafanya watende matendo hayo ila kubwa zaidi ni kua wengi wamepitia maisha ya kutopewa UPENDO. Upendo ni kitu muhimu kwa mwanadamu wengi hua hatujali jambo hili tunawaTreat watoto/watu vile tunavyoona sisi inafaa mwisho wa siku tunazalisha watu kama hawa mtoa mada anao waelezea.
Upendo unaweza kumfanya mtu mbaya kupita kiasi kua mwema na upendo unaweza kumfanya mtu mwema awe mbaya zaidi na zaidi. Tujitahidi kuwapa upendo wale walio karibu yetu
Maana kila mwanadamu anahitaji kuoendwa, since we're all need to belong to someone-thing.
Kumekua na debates mbalimbali juu ya adhabu ya kifo, deep kidogo kumekua na debate za njia za kutumia kutekeleza adhabu ya kifo.
Zamani kulikua na njia nyingi za kutekeleza adhabu ya kifo kutegemea na eneo Ufaransa walikua wanatumia 'guillotine' ambapo mtu anawekwa kichwa chake usawa wa makali yanaponing'inia kisha hayo makali yanaachiwa yakiwa speed na kufikia kutenganisha kichwa na kiwiliwili. It was a famous practice and it was done in public view.
View attachment 2013836
Guillotine
Overtime hii practice ikawa banned isifanyike hadharani. Mtu wa mwisho kuadhibiwa na guillotine hadharani aliitwa Eugen Weidmann.
Eugen Weidmann alizaliwa mwaka 1908 nchini Ujerumani kipindi cha WW1 Eugen alipelekwa kuishi na babu na bibi yake katika kipindi hichi akaanza udokozi. Tabia ikakomaa na akiwa na miaka 20 Eugen akafungwa miaka 5 kwa kosa la wizi wa kutumia nguvu.
View attachment 2013840
Eugen Wedmann
Akiwa huko gerezani akapata marafiki watatu, Roger Million, Blanc na Fritz Frommer, urafiki wao ukabadilika na kua ushirika wa uhalifu. Walipotoka gerezani wakaamua wawe wanawateka na kuwaibia watalii wanaotembelea Ufaransa. Ili kutimiza adhma yao wakakodi na nyumba Saint Clous eneo ambalo ni karibu na Paris.
Jaribio la kwanza likafeli. Mhanga wao alikua mtata, hatulii wakalazimika kumuachia. Dancer maarufu kutoka New York Jean De Koven akawa jaribio la pili na jaribio hili likafanikiwa. Eugen mwenyewe ndiye akamuua na kumfukia Koven kwenye bustani ya nyumba waliyopanga.
Hiyo ilikua July mwaka 1937. Eugen ana miaka 29.
Kisha hiki kikundi kikampa hundi za Koven mchepuko wa Roger Million ili akazicash hizo hundi. Kupata pesa kwa urahisi hivyo kukachochea ari yao ya kuendelea kupata faida.
Mwaka huo huo mwezi wa 9 tarehe 1 Eugen akamkodi dereva bwana Joseph Couffy ili ampeleke pwani maarufu ya French Riviera, walipofika Eugen akamshoot Joseph kisogoni na kuiba gari. Mwezi wa 10 tarehe 17 mwaka 1937 Roger na Eugen wakapanga miadi na producer aliyeitwa Roger Le Blond wakimuahidi kuwekeza pesa katika moja ya filamu zake badala yake Eugen akamshoot kisogoni (Kama kawaida yake) na kuondoka na wallet yake.
Kisha Eugen akamshoot Raymond Lesobre, real estate agent aliyekua anamuonyesha Eugen mazingira ya nyumba. M.O ile ile alimshoot kisogoni na akaiba gari na wallet ya Raymond.
Kisha mwaka huo huo yeye na Roger Million wakamhadaa Janine Keller, nesi, kwamba wanataka kumpa kazi. Badala yake wakampeleka pangoni na kumuua kisha kuchukua mali zake na kutokomea nazo.
Huyo ndiye akawa mhanga wa mwisho wa Eugen Wedmann.
Maaskari walikuta business card ya Eugen ofisini kwa bwana Lesobre na walipoifuatilia na kufika kwenye nyumba waliyopanga majibizano ya risasi yakaanza. Baada ya kuzidiwa Eugen na wenzake wakakamatwa.
Eugen akakiri makosa yote. Mwezi wa 3 mwaka 1939 hukumu ikatoka. Eugen na Roger Million wakahukumiwa kifo. Blanc akafungwa miezi 20 jela na kimada wa Roger Million akaachiwa huru. Baadaye adhabu ya kifo ya Roger Million ikabadilishwa na kua kifungo cha maisha.
17th June 1939 Eugen akakatwa kichwa kwa kutumia Guillotine. Mtandaoni kuna video yake ikionyesha jinsi tukio lilivyotokea. Zamani watu walishangilia kushuhudia mhalifu kuuawa lakini watu wa 1939 walikua tofauti walilaani na 'hysteria' iliyowapata ikazuka na skendo zingine ikabidi Rais apige marufuku kukata wahalifu vichwa hadharani.
View attachment 2013844
Eugen Wedmann Siku ya Hukumu
Adhabu kwa kutumia guillotine ikaanza kufanywa behind closed doors. Adhabu hii iliendelea mpaka 1977 na mtu wa mwisho kuadhibiwa kwa Guillotine baada ya kuhamishwa na kufanywa kwa kificho aliitwa Hamida Djandoubi.
Watu wachache wanaweza kufanya makosa halafu wasiadhibiwe kwa makosa yao. No I lied. Actually ni wengi, just mwezi uliopita watu walianzisha petition ya kutaka kijana mmoja aachiwe huru.
Kosa lake? Anatuhumiwa kuua.
Sababu ya kuachiwa? Ana sura nzuri.
Just that.
Now going through history tunakutana na watu ambao wamewahi kuachiwa huku wamefanya makosa. Mmoja wa hao watu ni Issei Sagawa, mJapan aliyemuua, kumbaka na kumla mwanafunzi mwenzake mHolanzi Renee Hartevelt
View attachment 2030871
Issei Sagawa
Sagawa ni maarufu anajulikana kama celebrity cannibal au Pang na umaarufu wake umeletwa na uhalifu wake alioufanya tarehe 11 June 1981. Crime doesn't pay, huh?
Sagawa anasema alianza kutamani kula binadamu tangu akiwa mtoto na alitamani kula mwanamke wa kizungu, alitamani kumla Grace Kelly, akiwa na miaka 23 huko kwao Japan akavamia nyumba ambayo kuna mwanamke wa Kijerumani aliishi.
Akafanikiwa kuingia ndani na kujaribu kumbana lakini Sagawa ana mwili mdogo, urefu wa futi 5'0, mwembamba mno utajiri wa baba yake haukusaidia kumpa mwili mkubwa.
Bahati nzuri mwanamke alishtuka kabla Sagawa hajafanikiwa azma yake na mwanamke mwenyewe alikua na nguvu kumzidi hivyo polisi walipofika walikuta Sagawa kabananinshwa hawezi kufurukuta.
Alipofikishwa kituoni akaandikiwa mashtaka ya sexual assault baba yake akatoa kitita kwa yule mwanamke ili aachane na ile kesi. As we know money talks so kesi ikafa.
Ambacho hawakujua ni kwamba Sagawa hakuvamia ile nyumba kwa ajili ya kubaka aliingia mule ili aende kumla yule mwanamke so ikabidi aendelee kushikilia fantasy zake zikisubiri muda mwingine.
Sagawa akaenda Ufaransa kusoma katika chuo cha Osborne alienda kusomea maswala ya lugha na fasihi, miongoni mwa classmates wake alikuepo Renee Hartevelt. Sagawa anasema alikua akileta madada poa kwenye apartment yake karibia kila siku kwa nia ya kumtafuna mmoja wapo lakini hakuweza kutekeleza dhamira yake.
Kisha siku ikafika Sagawa akamualika Renee nyumbani haikua mara ya kwanza kwenda kwa Sagawa kwahiyo haikua tatizo. Alipofika akawa anasoma shairi Sagawa akatokea nyuma ya Renee akiwa na bunduki na kumshoot shingoni.
View attachment 2030874
Renee Hartevelt
Anadai kwamba alitamani kuita ambulance lakini akaona kwamba kama siyo leo lini tena?
So akaanza kwa kuibaka maiti ya Renee. Anasema ni siku ambayo alisikia raha kuliko siku zote alizowahi kulala na mwanamke. Alipomaliza sasa ndipo upishi na ulaji ukaanza.
Akaukata mkundu, akaukaanga ila harufu ilikua kali akashindwa kuutafuna akaachana nao. Akahamia kwenye maziwa, kisha lips. Halafu akaanza kula vigimbi vya miguu.
View attachment 2030877
Mwili wa Renee
Alitumia siku mbili kuanzia kumuua Renee mpaka kumla na kuona ameikinai nyama. Akatoka kwenda kununua mabegi mawili makubwa na kuhifadhi mabaki ya mwili wa Renee. Akaita taxi na kumuambia dereva taxi ampeleke Bois de Boulougne, public park, alidhamiria kwenda kutupa mwili hapo.
Dereva taxi akiwa anamsaidia kubeba mabegi akamtania Sagawa 'Mabegi mazito sana kuna maiti nini humu?' Sagawa akacheka bila kujibu na safari ikaanza.
Kutegemea na wapi unaenda kuconsult sources zako juu ya hii kesi kuna sources zinasema alikamatwa hapo hapo na askari walioitwa baada ya kuona mabegi yanavuja damu na zingine zinasema hakukamatiwa hapo badala yake ni watu wakiwa wanajog wakaona mabegi yameachwa hapo huku yakivujia damu.
View attachment 2030876
Mojawapo ya begi
Kwa msaada wa dereva taxi wakapapata anapoishi Sagawa na kufanya ukaguzi wa kushtukiza.
Ambacho sources zinakubaliana ni vyombo vilivyokutwa na nyama, kitambulisho cha Renee na mvinyo. Sagawa akakamatwa na kupelekwa katika taasisi ya magonjwa ya akili ili ifanye tathmini kama ni legally sane kusimama kizimbani.
Hapa ndipo ucelebrity ulipoanzia.
View attachment 2030878
Alikaa hapo kwa miaka 2 katika hiyo miaka 2 akaandika kitabu alichokiita 'In the Fog' na kikawa bestseller because people love to read about murder.
Anyway, baba yake kwa pesa alizonazo akakodi wakili mwenye influence nene tu hivyo majibu yakaja kusema Sagawa ni chizi hivyo hawezi kushtakiwa.
Akakaa miaka 2 mingine katika taasisi ya magonjwa ya akili.
Kisha yule wakili akaishawishi mahakama kwamba ni vyema zaidi kama Sagawa ataenda kupata matibabu yake kwao Japan.
Mahakama ikakubali.
Sagawa akarudishwa Japan.
Japan akafikia taasisi nyingine ya magonjwa ya akili ambayo baada ya evaluation majibu yakasema kwamba Sagawa ana bipolar disorder ila siyo chizi hivyo anaweza kupelekwa mahakamani.
Ufaransa ikasema haina nia ya kuendelea na kesi.
Sagawa akaandika vitabu zaidi ya 20 akawa ana column yake kwenye gazeti, akaonekana katika interviews mbalimbali, akaonekana katika filamu, akatoa reviews za migahawa na akaonekana katika filamu ya porn ambayo alionekana akimng'ata tako porn actress.
Sagawa became famous at the expense of Renee's life.
Sasa hivi ana miaka 72 ila anasema anataka kabla hajafa amle nyama mtu mwingine.
Lakini hii nadharia ikawa inaelekea kufeli kwakua kila tarehe iliyotabiriwa kua ni mwisho wa dunia, dunia haikuisha. Ikapelekea kuzalishwa kwa minong'ono ya chini kwa chini juu ya uongo na utapeli wa Mwerinde na wenzake.Credonia Mwerinde - Kanungu District Massacre
Katika historia kuanzia ya kale mpaka sasa mwanamke ameonyeshwa kama kiumbe dhaifu ambaye anamtegemea mwanaume kwa kila kitu. Ukikaza macho kidogo katika historia utakutana na wanawake ambao walitenda uhalifu, mauaji na uhuni sawasawa na wanaume na wengine wamewazidi wanaume.
King Tamara (Wafuasi hawakumuita Queen) amewazidi wanaume wengi ila Credonia (Walitamka Keredonia) Mwerinde yupo level moja na Jim Jones.
Ulaghai, utapeli na mauaji vyote unakutana navyo ukiangalia historia ya Mwerinde. Ingawa historia nyingine inamtaja kama kahaba aliyejiuza katika kilabu chake cha pombe za kienyeji lakini aliyekua mume wake anasema ni kweli Mwerinde alikua malaya ila alikua hajiuzi. Hakuwa akilipwa kwa ajili ya ngono.
Mume wa Credonia Mwerinde Bwana Eric Mazima anasema kwamba biashara yao ilipata changamoto ikafa kisha 24th August 1988 Credonia akamuambia kwamba amepata maono kutoka kwa bikira Maria na sasa anataka kugeukia dini.
Wiki moja mbele Credonia akaondoka nyumbani.
View attachment 2042297
Credonia Mwerinde
Akiwa na wenzake watatu safari yake ikamchukua mpaka Nyamitanga, akawa ana shughuli ya kutoa ushuhuda juu ya maono anayopata kutoka kwa Bikira Maria. Akiwa hapa akakutana na Joseph Kibwetere, Kibwetere alikuja Nyamitanga na mkewe ili kuja kusikiliza hizi shuhuda. Hata yeye Kibwetere alidai anapokea maono kutoka kwa Bikira Maria, alitaka kukutana na mwenzake siku hiyo.
Juvenal Mugambwa, mtoto wa Kibwetere, anasema Credonia akamuambia baba yake kua "Nimepewa maono nimtafute mtu anayeitwa Kibwetere na tushirikiane kueneza injili" Juvenal anasema hiyo jioni baba yake alirudi nyumbani na Credonia, dada yake Credonia, marafiki zake wawili na mama yake wakati aliondoka nyumbani na mama pekee.
Credonia na Kibwetere wakaanzisha kanisa waliloliita Restoration of the Ten Commandments of God, kanisa lilikusanya watawa na mapadri ambao walitengwa na kanisa katoliki. Hili kanisa jipya likawa kimbilio la mabaki ya kanisa katoliki.
View attachment 2042300
Joseph Kibwetere
Kisha pale nyumbani zikaanzishwa sheria mbalimbali, ikawa hamna kuongea badala yake mawasiliano yakawa kwa ishara, hamna kula pipi ni ushetani, hakuna kutumia sabuni na mpangaji wa maisha ya pale alikua ni Mwerinde mwenyewe, na yeye alitoa maelekezo kutoka kwa Bikira Maria na Bikira Maria alimfikishia ujumbe Credonia kwa kupitia simu.
Simu ilikua ni kifaa chochote ambacho Credonia ataamua kiwe simu. Kwahiyo angeweza kutumia kikombe, kijiko au sahani kama simu ya siku hiyo ya kupokelea maagizo kutoka kwa Bikira Maria. Kanisa likazidi kukua na pale nyumbani pakawa hapatoshi wakatafuta sehemu mpya huko Kanungu, Kibwetere akamuacha mkewe na kumuambia ameamua kwenda na Credonia ili kusambaza injili vizuri.
Juvenal Mugambwa anasema inawezekana baba yake na Credonia walikua na uhusiano uliosababisha wagandane ila anaamini sababu zingine ni Credonia alihitaji mwanaume atakayekua sura ya kanisa, pia baba yake alikua ni tajiri kwa viwango vya Uganda ya 1970s hivyo hakuna namna Credonia angemuachilia Kibwetere.
Kanisa likazidi kukua. Sheria kali zilikua pale pale makosa yaliambatana na adhabu kali, kuongea uongo ilikupasa kusali rozali mara elfu moja. Kosa kubwa zaidi ilikupasa kumuomba msamaha Bikira Maria moja kwa moja, wakati mwingine inabidi uende kwenye jiwe lililosemwa ni kiwakilishi cha Bikira Maria na uende kuomba msamaha hapo.
View attachment 2042302Jiwe lililofanana na Bikira Maria
Kanisa liliamini dunia itaisha. Na kutii amri kumi za Mungu ndiyo njia pekee ya kuokoka, kanisa lilivuna waumini kupitia hii nadharia, lilivuna na mali za waumini pia kupitia hii nadharia.
. . . Baadaye kidogo . . .
Asante sana mwambaLakini hii nadharia ikawa inaelekea kufeli kwakua kila tarehe iliyotabiriwa kua ni mwisho wa dunia, dunia haikuisha. Ikapelekea kuzalishwa kwa minong'ono ya chini kwa chini juu ya uongo na utapeli wa Mwerinde na wenzake.
Hii ilimaanisha wanahitaji kuja na suluhisho haraka ama dunia iishe au warudishe mali walizotoa kwa waumini. Kiendacho kwa mganga hakirudi na pili ile nadharia ya dunia kuisha? Mwerinde & co walijua kabisa hakuna kitu kama hicho so kabla mamlaka kidogo waliyobaki nayo wakayatumia kuita kusanyiko.
Kusanyiko lilikua ni kwaajili ya kua pamoja siku dunia inaisha. Na ikaamuliwa kusanyiko liwe tarehe 17 March 2000.
Ukiangalia pattern za matukio ya wauaji kuna points mbili au tatu utapata zinazoweza saidia kutabiri baadhi ya matukio mfano, Mwerinde kabla hajahamia kwa Kibwetere aliwahi kuchoma moto nyumba ya mwanakijiji mwenzake na akapotea hilo eneo akarudi wiki mbele. Akadai amechanganyikiwa, kipindi hicho alikua na miaka 20.
Kisha kuna madai ya kumtongoza dereva pikipiki, usiku walivyolala akamuua na kumuibia pesa. Kuna ripoti pia ya kaka zake 3 kufa mmoja mmoja kabla hajabaki peke yake na kurithi nyumba ya baba yao. Haya matukio yameelezwa katika barua iliyoandikwa na rafiki wa karibu wa familia ya Mwerinde.
Kisha tukio la mwisho kabla hajahama nyumbani kwa Kibwetere lilikua la kumchomea moto mke wa Kibwetere kabati lake la nguo. Hii kazi alimpa mdogo wake Ursula Mwerinde, yeye akachukua kazi ya kumshushia kipigo Bi Teresa Kibwetere. Bi Teresa alikimbia kukwepa kipigo.
Kama unashangaa mume alikua wapi mume alikuepo na alikua anasupport.
Kwa haya matukio na pattern iliyopo vyovyote iwavyo 17th March ilitakiwa iwe siku ngumu. Ripoti za mwanzo zilisema baada ya kukutana wakajifungia kwenye jengo lao la makao makuu wakajimwagia petroli na kujiwasha moto.
Lakini kama watu walienda kudai mali na pesa zao au dunia iishe hivi utawamwagia petroli wakuangalie? Haiingii akilini na ndivyo uchunguzi ulivyothibitisha.
Baada ya wote kuingia ukumbini milango ikafungwa kwa nje, sehemu ambazo zingeweza kutoa upenyo wa kutoka zikagongelewa misumari na petroli ikamwagwa kuzunguka jengo zima.
And then the building was set on fire.
Maeneo ya kanungu ni ya milimani na mabondeni wenyeji wanasema mlipuko wa moto wa ghafla na vilio ulitawala eneo la Kanungu. Kisha ikafuatiwa na harufu kali ya nyama inayochomwa kiasi kwamba ilibidi wachukue majani yenye harufu kuziba pua kukata harufu ya nyama.
Ripoti zinasema hata baada ya moto kuzimika harufu ya nyama ilitawala eneo lote kiasi kwamba wenyeji walishindwa kula nyama mwezi baada ya tukio kuisha.
Askari walipofika eneo la tukio walikuta miili inayokadiriwa kufikia 600 ikiwa imekua mikaa, wakaripoti tukio zima kama mass suicide na kutulia, walipoanza kuchunguza viwanja vilivyokua chini ya umiliki wa Movement wakagundua kuna makaburi ya pamoja mengi yaliyokutwa na maiti zaidi ya 300. Kaburi moja urefu wake ulifikia hecta 40.
Miili iliyokutwa humo ilikua na majeraha ya visu, kupigwa na kitu kizito kichwani na kulishwa sumu askari wakabadili walichoripoti. Wakasema hii ni mass murder na wakatoa hati ya kimataifa ya Mwerinde na Kibwetere kukamatwa popote walipo.
Miaka hiyo, njia za mawasiliano zilikua hafifu zilitosha kufanya hawa wawili wasikamatwe. Kibwetere ilisemekana amejificha Malawi lakini Uganda walipofuatilia walishindwa kumpata.
Jeshi la Polisi la Uganda linaamini Mwerinde na Kibwetere wapo hai na kuna mahali wamejificha.