True Crime Thread: Updated Regularly

Mmmhhh. Hii ni zaidi ya hatari.

Ki Hitler Hitler zaidi
 
Tunaendelea

Makuzi yake kielimu hayakua mazuri, Gacy shule ilimshinda akaenda Las Vegas huko akaona hapamfai kwakua hakupata pesa ya kumtosheleza akaamua kurudi Chicago. Alivyorudi Chicago mwenyewe akaamua kujiunga na Chuo cha Biashara,Gacy ni mzuri katika kuongea angeweza kujitoa matatizoni kwa mdomo tu.


John Wayne Gacy

Hivyo hiki kipaji na elimu aliyoipata vikamnufaisha ipasavyo alivyomaliza chuo akaajiriwa katika kampuni ya Nunn-Bush Shoe Company kama Management Trainee. Kipaji na juhudi vikasababisha ahamishwe kwenda kusimamia Wing ya nguo huko Springfield, Illinois.

Gacy akaanza kugain uzito kwa fujo, akapatwa na matatizo ya moyo na mgongo na akaishi nayo milele. Alivyofika Springfield alijiunga na taasisi mbalimbali zilizojihusisha na jamii. Akawa mwenyekiti wa Chi Rho Club, akawa mjumbe wa bodi ya Catholic Inter-Club Council, akawa Kapteni wa Kamandi ya Chicago Civil Defense, akawa Afisa wa Holy Name Society na akawa makamu Rais wa Jaycees na huku ndipo alitumia muda wake mwingi.

Mwaka 1964 akakutana na Maryln Myers mtoto wa kishua, wazazi wake walimiliki migahawa mbalimbali franchise ya KFC. Baada ya ndoa baba mkwe akamwambia Gacy aje wafanye kazi pamoja. Kwa wastani Gacy alitakiwa kufanya kazi kwa saa 12 lakini haikua ajabu kufanya kazi saa 14 na zaidi alijitoa kwelikweli kwenye kampuni ya mkwe akiamini watakuja kuzirithi.

Wakapata mtoto wa kiume, kisha akafuatia wa kike. Myers akabaki kulea Gacy akaendelea kujitoa kihali na mali KFC na kwenye kila taasisi aliyohusika nayo na bado alipata muda wa kukaa na mkewe.

Katika kitabu cha Clifford Linedecker, The Man Who killed Boys, amenukuliwa volunteer wa Jaycees, Charlie Hill akisema "Mara zote alionekana kuna project anaishughulikia, alijitoa mno Jaycees. Hii taasisi ilikua ndiyo maisha yake" Mwaka 1968 akaanza kampeni za kuutaka urais wa Jaycee.

Kisha minong'ono ikazuka kwamba anapoonekana Gacy basi lazima kuwe na vijana wa kiume "Gacy is gay" kabla minong'ono haijasambaa sana May 1968 Gacy akashtakiwa na Mark Miller kwa kosa la kumlaghai, kumfunga kamba na kumbaka kikatili.

Gacy akajitetea kwamba alikubaliana na Miller juu ya kilichotokea na walikubaliana kua atamlipa na akapoint kua huu ni mchezo unafanywa na washindani wake wa nafasi ya urais. Kwa status yake ni rahisi kuaminika lakini kesi ikiwa inaendelea miezi minne mbele Gacy akashtakiwa kwa kosa la kukodi kijana wa miaka 18 ili ampige Miller.

Kijana alipokamatwa akasema alitumwa na Gacy. Gacy akarudi mahakamani akiwa na kesi mbili na akapigwa nyundo 10 jela katika gereza la Iowa State Reformatory. Baada ya hiyo hukumu mkewe akadai talaka wakaachana. Gacy alijua kua akionyesha tabia nzuri paroli yake italeta matunda, miezi 18 baadaye Gacy akaachiwa kwa paroli.

Akarejea Chicago.

. . .
 
Imekua muda mkubwa aisee
 
Tunasubiri muendelezo
 
kimya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…