True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

...13
Basi tuliingia ndani ya slopu ile, nikaingia chumbani huku babu akiningoja pale sebleni, nilichukua elfu 60 ndani ya begi na kurudi nayo sebleni ambapo nilimkuta babu amengoja kwa hamu, nilimkabidhi akafurahi sana,
Kubyala kwa wiza (kuzaa kuzuri sana) alisema babu huku azificha fedha zili ndani ya puzo (bukta kubwa) alokuwa amevaa kwa ndani,
Usimwambie bibi yako kama umenipa mzigo, sawa mzee mwenzangu?
Alitahadhalisha babu, nikamwambia wala asijali, kwani bibi yeye nmempa masukari na maunga ya ngano kutoka kwa mama mkwe wake (mama yangu) hivyo simwambii chochote bibi,
Sawa pumzika kijana wangu, kesho ntakusimulia ntakayoyasikia huko kwenye tukio, alisema babu, kisha akaondoka,
Nilitoka nje kumuaga bibi kwamba nataka nipumzike, kwani nilitaka pia kuhakikisha kama babu ameondoka ili bibi naye nimpe mzgo wake,
Kweli babu alikua ameelekea senta kwenye tukio la fisi kuiba mtoto mapema tu,
Nilirudi ndani ya slop na kuchukua 50 elfu nikamkabidhi bibi na kumwambia, 30 imetoka kwa baba na 20 kwa mama.
 
...14
Basi bibi alifurah mno na kunitakia usiku mwema, akoondoka nami nikafunga mlango na kujipumzisha,
Sasa nikawa nawaza mambo niloyasikia kwa muda kidogo niliopata kuwa pale kijijini!
Eti kwa babu yangu panaogopeka kwa uchawi?
Nikae mbali na wasichana wa pale kijijini vingnevyo nitakoma?
Fisi kukamata mtoto mapema tu!
Hili la mademu halikuniumiza kichwa sana, ila hili la uchawi niliogopa mno! Nilitoa kiredio changu ndani ya begi na kuweka stasheni ya redio maria usiku ule walikua wanapiga nyimbo za noel mfululizo!
Nilipitiwa usingizi mpaka nilipokuja kustuka baadae mvua kubwa ikinyesha! Nilipo sikiliza vizuri, nikahis dirisha linagongwa kwa nguvu! Niliogopa, nikasogea dirishani taratibu na kuuliza nan wewe! Fungua mwenzio nalowa, sauti ya kike ikasikika! Nilijikaza na kufungua mlango, hah? Yunge?
 
...15
Sikuamini macho yangu kumwona yule msichana nilomsindikiza mapema kwenda nyumban kwao amerudi usiku huu na mvua yote!
Mwenzangu saa 6 hii pekeyako na mvua hii yote shida nini? Nilimwuliza yunge!
We acha tu, yaani nimelowa mpaka nahisi kuganda, alijibu yunge na kuongeza, nyumba ninayolala inavuja sana, hivyo nimeona bora nije nilale hapa!
Na je wazazi wako wakigundua haumo ndani si watapatwa taharuki?
Hapana, nimeshazoea kuja kulala humu mvua ikinyesha usiku, hivyo wala usiwaze! Akajibu,
Bas alichukua kapet chini ya uvungu na kuelekea nalo sebleni kwa ajili ya kutandika alale. Yaani leo nalala chumba ki1 na dem? Hii bhagoshaaa!
 
Itaendelea kweli
 
...16
Basi nilimsikia yunge anatandika pale sebleni, nikwa najiuliza sijui nimwambie aje tulale wote pale kitandani, atakubali kweli? Niliogopa!
Ghafla alikuja chumbani na kusema mhh! Nmesahow nguo ya kutandika maskini, hivi hakuna nguo ya akiba humu? Aliuliza!
Hapo hapo nkapata ujasiri! Nakumwambia, kwanini usije tulale wote mchumba?
Wewe nani mchumba wako hapa? Umri huu naweza kuwa mchumba wako? Ebu acha utoto bwana! Aliongea yunge kwa kujiamini!
Kwahiyo unadhani tukilala wote ntakufanyaje? Shakwambia huku sikufata mademu wala nini, nipo hapa kuwasalimia wazee wangu,
Nilimchimba mkwara yunge ambae alionekana kupatwa na aibu kdgo! Nikweli kwa kumwangalia ilionekana ananizidi kama miaka miwili ama mitatu hivi!
Basi kama unaogapa kulala namie mchumba, njoo ulale hapa kitandani na mie ntalala hapo sebleni! Nilimwambia ila alikataa katakata mimi kumwachia yeye kitanda ilihali mie mgeni!
Sawa we lala hapo sebleni na hilo baridi tuslaumiane,
Nilijilaza huku nikimchombeza hata iweje wewe ndo mchumba wangu! Ebo?
 
Weka full ndefu au weka yote hizi short sana wanaona kama haupo serious ni tag
 
...17
Tutaona, alisema yungu huku akitokomea sebleni!
Niliwaza sana! Je huyu binti amekuja kwaajili ya kujikinga na mvua kweli ama danganya toto?
Iweje mapema nilipomchombeza kwamba yeye mzuri akanambia sijamwona tu yunge mdogo, nakwamba siku nikimwona ntayafuta maneno yangu mara moja! Na vipi anitahadharishe kuhusu waschana wa pale kijijini kwa msisitizo sana?
Basi nilifungua kiredio changu nikajilaza, wakati nakaribia kupitiwa usingizi nilistuka yunge anabisha hodi!
Karibu, nikamwitiakia! Aliingia chumbani akasema nimevutiwa sana na nyimbo unazopiga kwenye redio yako! Napenda mno nyimbo hizi roma (katoliki) naomba tulale wote ila tusigusane, pale sebleni baridi kali linapita chini ya mlango! Nikamwambia poa! Kukuondolea wasiwasi mie nageuka mzungu wa pili!
Hapana tulale tu, unaonekana ni kijana uliyepevuka, hivyo nakuamini! Alisema yunge! Binti anaakili sana huyu, niliwaza,
Tulilala kila mtu shuka lake! Nlijitahdi kubana pumzi nisipumue kwa nguvu!
Nmeipenda radio yako! Niazme kesho nkasikilize kwaya,
No!
 
....18
Kwanini?
Siazimishagi redio yangu kwani huyu ndo mke wangu!
Yunge: kwahio umechukia?
Mimi: nichukie nini tena?
Yunge: vp umesikia yalotekea senta leo?
Mimi: dah! Ya mtoto kubebwa na fisi?
Yunge: ee! Hayohayo
Mimi: nimeskia, alitusimulia babu.
Yunge: kumbe babu karudi?
Mimi: alirudi punde ulipoondoka tu! Na kwamambo yanayotokea hapa mie kesho narudi nyumbani!
Yunge: nyumbani? Hutaki kulima tena?
Mimi: silimi kesho narudi nyumbani nisije bebwa na fisi nikakuacha mchumba wangu nnaekupenda ukabaki ukiteseka duninani! Nilimchombeza yunge ambae aliguna, kisha akasema, sasa hutuq tena kulima wakti nshamwomba mama yale majarubb ma3 na amekubali?
Mie silimi naenda nyumbani, nilichimba mkwara kwani nilishaamini huyu ashanasa kwangu huyu!
Basi usiogope ntakulinda mme wangu! Alisema.
Sikuamini ile kauli kama imetoka kwa yunge! Nilimwambia unanizuga tu mwisho wa siku mwenzio nafanywe kitoweo!
Tena nasema hakuna atake kugugusa! Yeyote atakaekusogelea ntamwonesha nguvu yangu, alisema yunge!
yunge mdogo ndo nan?
 
...19
Mhh? Umemjuaje yunge mdogo mara hii? Aliuliza yunge!
Umesahau ulinambia nikikutana nae ntakusahau mke wangu? Nilimjibu na swali juu,
Yunge: Nilisahau bwana, yunge ni msichana aliepo hapo jirani tu! Yaani ukipita nyuma ya hio nyumba ya nyasi (jiko la bibi) ukivuka mahindi unatokezea kwao na yunge mdogo! Ni msichana mzuri ila mchawi balaa! Ukimwona utanisahau mimi nakwambia!
Mimi: mhh? (niliguna huku picha ya binti alienikamatia jogoo ndani mwao ikipita haraka!
Yunge: mbona unaguna, umemwona?
Mimi: hapana sijabahatika kumwona,
Yunge: basi kaanae mbali, na si huyo tu, kuna mhoja huko senta, nyanzara na shija pia, sitotaka wakusogele,

Hapo niliona wazi wivu umeanya kummeza mtoto wa watu, nikaona hapa nicheze kama mwamba wa lusaka (chama) kudeshi kama napiga kumbe nafanya, bila kujua kwamba ntayaharibu mambo yaloanza kujipa,
Samahani natamani natamani kumwona huyo yunge mdogo anafananaje, nilisema,

Nini?
 
....20
Nsehe unasemaje? Aliuliza yunge,
Mimi: nataka kumwona yunge mdogo alivyo mzuri!
Dah! Binti wa watu akakaa kmya,
Niligundua kachukia kusikia hvyo, mara ghafla akainuka na kusema, naona mvua imekata naomba nirudi kwetu!
Mimi: usiku wote huu ukatize mashamba hayo huogopi mafisi? Ebu lala mchumba utaenda mapema asbuhi!
Yunge: nani mchumba wako
Mimi: wewe hapo yunge ndo mchumba wangu! Bibi amekuchagua na mie nikaridhika kiroho safi kabisa! Nakupenda mno mchumba wangu!
Kiukweli nilijishangaa nmeyatowa wapi maneno matamu kama yale, sikuwahi kumwambia msichana maneno matamu kama haya tangu nmeanza kubalehe! Hatari sana
Basi yunge alijinunisha pale, lakini nilifanikiwa kumcontroo na tukarudi kitandani kulala huku nikijihesabia ushindi njenje!
Tulilala sasa nikapata kaujasiri kakupititisha mkono kumkumbatia kwa nyuma kwani sasa tulijifunika shuka moja japo alinitegea mgogo! Alistuka kidogo na kusema...!
 
.....21
Jamani mimi ni mkubwa kwako bwana, alisema yunge!
Mimi: labda kama unatafta njia ya kunikataa tu, maana naona hunipendi na hujaridhika mimi kuwa mchumba wako, najua siwezi kulazimisha mambo! Tulale tu wala sikufanyi chochote, miaka hii 19 sijawahi kufanya leo hii nikubake mtoto wa watu? Siwezi bwana, nilipama kina cha maji!
Yunge: umechukia?
Mimi: kwani nmefoka?
Yunge: haya tulale usiku mkubwa huu
Mimi: poa,
Nikazima radio nakujigubika ghubighubi! Tulipitiwa usingizi mpaka yunge aliponistua kwamba kumekucha na anataka ondoke! Basi saa 11 na dakika 37 ile nikamsindikiza mpaka karibia na nyumbani kwao, kabla sijaanza kurudi akasema, mhh! Nmeamini wewe ni mchumba wangu kweli! Naomba usirudi nyumbani kwenu leo, baki nitakurinda na mafisi na hao wachawi wachawi! Alisema,
Pia ukibaki ntaamini unanipenda kweli, usiku ntakuletea zawadi ambayo hutoisahau! Sawa nzehe? Aliuliza! Sawa ntaona!
So kuona baki bwana!
 
Leta mwendelezo
 
Back
Top Bottom