...24
Niliondoka kuelekea kisimani kuchota maji kukiwa kumeanza kupambazuka sasa na ukungu unaelekea kuisha! Nmetembea kama dakika 4 hivi, nikaona waschana wawili kwambele wanatoka kisimani wamebeba ndoo vichwani! Wanaelekea niliko mimi yaani uso kwa uso nakutana nao!
Ng'wangaluka yunge (habari ya asbuhi yunge) nilimsalimia yunge mdogo ambae alisimama ghafla na kunikata jicho, umelijuaje jina langu? Usinizoee sawa? Alinikoromea yunge mdogo huku akizichapa hatua na kuondoka, nilimtizama kwa nyuma, dah! Kweli nilikiri yale aloniambia yunge mkubwa, niyule binti alie nikamatia jogoo ndani mwao, ambae nilimkuta amepauka anaanua maharagwe, leo namwona asbuhi hii akiwa safi kabisa! Kweli alikua msichana mzuri sana ika aliniudhi kwa dharau alonionesha, nikawaza ntakuonesha pimbi wewe! Nilienda kuchota maji pale kisimani ambapo kulikuwa na kina mama na wasichana kadhaa waliokuwa wamepanga foreni kungoja zamu ya kukinga maji kwenye bomba lile, nikawasalimia kwa heshma na wakaniitikia freshi tu, mama mmoja aliniuliza!