True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

.....!
Niliwasha moto pale nje(shikome) kisha nikachukua kiti na kukaa karibia na moto, muda kidogo alikuja yule binti akiwa kabeba rufuria na kisu, ndani ya sufuria kulikua na yule kuku alienyonyolewa manyoya, basi binti kwa ustaarabu akaniomba nimshikie ili amkate vipande vipande yule kuku kwani anakazi nyingine ya kufanya nyumbani kwao,
Nilimshikia akaianza kazi ile mara moja.
Unaitwa nani? Aliniuliza yule binti huku anaendelea na kazi yake,
Naitwa Buhabhi jina la babu, ila nitapenda ukinita nzehe, nilijibu,
kwanini unapenda jina la nzehe (mzee) aliuliza tena,
Napenda jina hilo kwa sababu ndo jina ambalo mama hupenda kuniita kwa kuhofia kulitaja jina la baba mkwe wake (babu kizaa baba) nilimjibu.
Nikweli sio vizuri kutaja jina la mkwe, alisema yule binti na kuongeza,
Sasa mbona hujaweka kuni kubwakubwa (shitinde) kwenye moto wako? Aliuliza huku akinitazama usoni,
Mie sijui bwana, nilimjibu,
Kuni kubwa ndo uhai wa moto ule, yani bila hizo moto hautodumu, basi nilisogeza magogo mawili makubwa nikachochea
Endelea mkuu
 
...41
Nilihitimisha zoezi la kumkandakanda, aliinuka kivivu kama mwanamke mwenye ujauzito wa miezi 18, yaani ameshaanza kudeka tayari, niliona ameifurahia huduma ile, aliaga na kuondoka nayale mashuka pamoja na nguo zangu nilizovaa siku iliyokuwa imepita, nilitazama juu ya godoro, kulikua na damu, nilchukua tambala nakufuta ile damu kisha nikageuza godoro, nilitoka ndani nikaenda kukaa nje kwenye kivuli cha mwembe kwani jua lilianya kuwa kali sasa,
Niliyafikiria yote yaliyotokea tangu asbuhi, nilijikuta nasimuliwa na mchezo walionifanyia bibi na babu, yaani mtu anahama siti bila mimi kujua wakati nipo karibu yao!! Nilibaki kusikitika tu,
Nilimkumbuka yunge mdogo, hivi huyu mtoto nae atakua nalake jambo, inakuaje arudi ndani ya dakika 30 kuulizia jambo lilelile ilihali anajua mtu akienda msibani kurudi ni mpaka jioni? Analake jambo huyu, ila ni mtoto mzuri sana, amenivutia sema anadharau, niliwaza muda huo nimeshahau tunu alionitunukia yunge mkubwa, wanaume ndo maana dada zetu wanatuitaga hizi mbwa!
 
...42
Wazo ilikuwa kumwona yunge mdogo sasa, tena niliona anachelewa utafikiri aliniahidi angekuja punde,
Lakini nilikumbuka hali alotukutanayo mimi na yunge mkubwa, nikaona hapa hawezi kuja,
Sasa nifanye nini? Niliwaza, ebu ngoja,
Nilizunguka nyuma ya nyumba ya nyasi (jikoni) nilikumbuka huko ndipo kuku wanapenda kutulia wakati wa jua kali kwani kunakivuli cha mahindi, nilinyata na kuwastua wale kuku, halooo walipiga kelele la hatari! Walitimua mbio kuelekea nyumbani kwao yunge mdogo, sasa nilingoja kuona mtego wangu utafanikiwa?
Kama nilivyotarajia, yunge mdogo alitokea huku akiwa makini kuangaza aone kunanini chenyekuwatoa mbio vile wale kuku,
Tulikutana huku mimi pia nikivunga kuangaza nione nini kimewapigisha kelele wale kuku,
Kumbe wewe, mie nikajua labda fisi amekuja kukamata kuku mchana kweupe, nilimtupia mpira kana kwamba yeye ndo kawastua wale kuku,
Mimi pia nmesikia kelele za kuku, tena wamekuja mbio nikajua kimbulu (pakashume) anaetusumbuaga amekuja tena, alijibu yunge mdogo.
Atakua yeye eti?
 
...43
Nilijishangaa hayo maujanja nmeyatoa wapi? Yaani nilijiona mwamba kweli kweli! Nilikua nimepiga bao mbili kwa shuti moja kama mayele kupitisha mpira katikati ya miguu ya beki mmoja wa simba na mpira kutinga nyavuni!
Mimi: wala sio kimburu, ni mimi nilitaka nikuone tu.
Yeye: kwahio umemalizana na mkeo ndo ukanikumbuka na mimi? Acha mikwara basi,
Mimi: achana na huyo, wewe hukuniona nilivyokua nafurukuta aniachie lakini alining'ng'ania?
Yeye: si ungekuja nyumbani kwani hupajui?
Mimi: napajua, lakini kwahapa kwetu ndo nahisi ntakua huru zaidi.
Yeye: enhe unasemaje maana ushaniona sasa, naweza nikarudi?
Mimi: naomba unisaidie kama kuna mahindi yalokomaa nichome maana nnahamu nayo sana!
Yeye: mhh! Yapo nimechemsha ila kama unataka ya kuchoma ntakuchomea,
Nitashukuru maana njaa nayo ishaanza nitafuna, nimwambia.
Basi ngoja nikiayandae sawa? Alisema,
Poa nangojea kwa hamu, nilimwambia akaondoka nakuniacha najipongeza kimyakimya kwa kumweka karibu nami! Nilishasahau kumkomesha kabisa, Nilirudi kivulin kungoja.
 
Back
Top Bottom