True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

Oya we mbwa bado dakika 10 saa 1 ifike uko wapi mda huu? Tunataka muendelezo wa hii story

Aliuliza hilo swali huku amekaza sura mithiri ya nyoka koboko alieona panya mwenye mimba huku akiwa amekaa senta kusubiri mejibu ya msimuliaji yatakuaje, laahaula...
 
kumbe nawewe ni mdada?
 
...44
Zilpita kama dakika 10 ndipo yunge mdogo alipokuja na sinia likiwa na mchanganyiko wa mahindi yaliyochomwa nayale yaliyochemshwa,
Hakika sitorudi nyumbani kwetu kwa ukarimu huu mlionao watu wa huku,
Nilimdaka kwa maneno kabla hajatua sinia la mahindi.
Hivi kwenu wapi? Aliuliza.
Nilimjibu huku tayari akiwa ameshatua sinia la mahindi, alikaa pale chini tukaanya kuyashambulia huku tukiendelea kujuana kila moja wetu,
Ila wewe ni msichana mzuri sana, sijaona wakukukaribia hata kidogo hapa kijijini.
Nilimwambia huku nimemkazia macho,
Kiukweli sipendi dhihaka kaka yangu, kula mahindi ushibe ufanye mambo mengine, alijibu huku akionekana kutofurahishwa na chombezo lile,
Hodii! Ilisikika sauti ya kiume,
Karibu, nilimkaribisha mgeni yule alieonekana kuwa na umri wa miaka kati ya 22 na 24 hivi.
Asanteni.
Alitusabahi na kuniuliza, wenyeji wa hapa wapo?
Nilimweleza walipoenda kisha nikamwuliza kama naweza msaidia kwani alikuwa na daftari mkononi,
Nimepita kuchangisha fedha kwa ajili ya chakula cha wachezaji!
 
...45
Tunamechi weekend hii hapa hapa nyumbani, hivyo nimepita kuchangisha mchele, maharagwe ama fedha kwa ajili ya wachezaji wetu, alijibu yule jamaa ambae baadae nilimtambua kama captain wa timu ya kijiji!
Fedha kiasi gani? Nilimwuliza.
Kiasi chochote utachojisikia kutoa, alijibu.
Nilinyanyuka na kuingia getoni kwangu, nilichukua shilingi elfu kumi na kurudi pale mwembeni ambapo niliwakuta wanaendelea kuyashambulia yale mahindi, nilimkabidhi na kumtaka akate elfu 5, jamaa alifurahi mno, yaani wengi walikua wanatoa 500 na wengine 1000, hivyo jamaa alishukuru sana.
Vipi kaka naweza pia nikajiunga na timu yenu? Niliuliza.
karibu sana, unacheza namba ngapi?
Nakanyaga wings zote kaka, nilijinadi.
Basi karibu kwenye mazoezi leo jioni, tuanaanza saa 10 kamili.
Nilimjibu nitahudhuria bila kuchelewa.
Aliaga na kuondoka nikabaki na yunge ambae alianza kusunda sania lale ili aondoke.
Kwahio hela yote hiyo unatoa mchango wa mpira? Alinitupia kijembe,
Mimi: napenda sana mpira, yaani tena nimefurahi kupata nafasi hii!
 
...46
Nyie chezeni washabiki tupo tutashangilia, ila sioni kama utapata nafasi ya kucheza maana huyu alietoka hapa ndo mchezaji mdogo kuliko wote, na anaujua kuucheza mpaka wakampa cheo cha kuwa kiongozi wao (captain) sasa wewe kwa umri wako huo utakua mshangiliaji kama sisi tu,
Alinichimba mikwara yunge mdogo.
Sio mbaya kama nitakua shabiki pia, kwani lengo langu mimi ni kufanya mazoezi, lakini pia ikitokea hao wakubwa mmoja wao kapata tatizo naweza nikaziba pengo lake, nilimjibu huku nikiwaza kumshangaza siku ya mechi kwa mautundu ntayoyafanya uwanjani,
Yunge: mie naenda sasa
Mimi: tupige stori basi, unajua nakuwa mpweke kukaa pekeyangu hapa na kulivyozungukwa mahindi naogopa sana.
Yunge: twende tukakae kwetu sasa.
Mimi: hapana, nimeachiwa kulinda hapa.
Yunge: kwahio kwetu umeona kuna mlinzi? Imebaki zamu yako kuja kunitembelea, nahilo ni deni.
Aliongea huku akiondoka pale nilipokua nmekaa.
Kwa mara nyingine nikapata nafasi ya kulisha jicho, alitokomea. nikatupa macho kwenye ile njia ya kwenda kisimani!
Mh!
 
Hii simulizi yako, ndio simulizi iliyoandikwa kivivu zaidi hapa JF. Yani episode inakua na mistari kumi, alafu tunasubiri episode nyingine.

Unazingua "bloangu". Andika paragraph za kutosha.
 
Back
Top Bottom