True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

...48
Nijibu basi, yule msichana alikuwa hapa muda si mrefu, sivyo? Alinikazia yunge,
Ebu leta hayo maziwa kwanza, mie ninanjaa,
Nilimpotezea,
Shauri yako, nilikuonya jana ila leo tu umeshaharibu, hao paka na bundi ni maarufu sana hapa kijijini, wale ni walinzi wa yule msichana, na wanafahamu kila kitu juu yetu mimi na wewe, sasa wameshajua kwamba unataka kumchezea mtoto wao na ndio sababu walikuwa wanakuangalia kwa hasira, bahati yako babu naona amekuwekea kinga, vinginevyo...!
Nyiee mbona mmejifungia ndani jua kali hivi? Kuna nini humo? Ilikuwa ni sauti ya bibi akiuliza.
Sihuyu mme wako nimemkuta amejilaza ndani muda huu, hata mimi namshangaa!
Alisema yunge,
Tulitoka ndani na kumsalimia bibi, kisha yunge alipeleka sufuria la viazi na birika la maziwa pale kivulini, tulikaa pale mimi na yunge huku bibi akiingia ndani.
Usiwaambie babu na bibi, hilo jambo dogo ntalimaliza mwenyewe, ila sasa umeanza kuamini niliyokuambia juu ya yunge,
Naomba uachane nae kabisa utapotea sawa mchumba..!
Nyie ndo mnakula sasa?
 
...49
Bibi nilichelewa kidogo, kulikuwa na nguo chafu nilienda kuzifua, alijibu yunge,
Tulishambulia viazi na maziwa yale mpaka tulipo maliza,
Naona mmependeza sana! Mnanikumbusha enzi zetu na babu yenu, alisema bibi akiwa anavunja kuni,
Ndio nakumbuka ulivyokuwa unanitunzia wali mwingi na maziwa ya kushiba, ulikuwa binti mjinga, yaani ulikuwa tayari baba mkwe alale njaa, ila sio mimi mpenzi wako, alidakia babu ambae alitokezea kwenye ile njia ya kuelekea kisimani,
Kwahio nawe umesahau siku ulipoacha mifugo ikaingia shambani na kuharibu mazao ya balozi kwa sababu yangu? Na mbaya zaidi mlilipishwa sh10 ambayo kwa hela ya leo unaweza kutoa mahari kwa wanawali wawili na chenchi inabaki? Alihoji bibi.
Sawa bwana, tulipendana kweli na ndo sababu tupo pamoja mpaka uzee huu!
Alimaliza babu huku akitupia chini gogo alikokuwa amebeba kwaajili ya moto jioni!
Yunge aliaga na kuondoka,
Bibi akaingia jikoni na babu alikuja pale kivulini na kimkeka kilichochakaa!
Tulipiga stori pale mpaka bibi alivyoivisha msosi..!
 
..50
Baada ya kula nilimweleza babu juu ya yule kijana aliekuja kuchangisha fedha kwa ajili chakula cha timu ya kijiji, hivyo nilimtaka aniruhusu niende kiwanjani nikafanye zoezi kwani mpira ndo ulevi wangu! Hakuna tatzo mdogo wangu, we nenda kacheze, mie naenda kutafta watu wa kulima majaruba yangu, nataka wiki ijayo nipande mpunga, alijibu babu.
Lakini kabla sijainuka nilimwona yunge mdogo kwenye shamba la mahindi akinipa ishara twende kisimani kuchota maji!
Nilisahau kwenda kiwanjani! Niliingia jikoni na kubeba dumu moja, kisha nikaelekea kisimani! Nilizichapa hatua haraka ili nimpate yunge mdogo ambae alikua ametangulia! Mbona simuoni kajificha wapi? Yunge! Niliita kwa sauti ya chini, lakini ikawa kimya, nilitembea mpaka kisimani lakini nisimwone, nilikaa kama dakika 5 kungojea labda atatokea, lakini wapi! Sikumuona.
Nilichukia sana, nikachota maji na kuondoka huku nikiwa nimechukia sana.
Nitakukomesha, niliwaza.
Nilibeba maji na kutembea haraka ili niwahi kiwanjani.
Nisubiri bwana, mbona unaniacha...!
 
Kijijini Kuna kanisa?
Jifunze RIGHTING SKILLS ili uwe unaandika aya ndefu ndefu.
Katika hii simulizi jina Yesu lazima liwepo.sio unataja wachawi tu
Kwanza uelewe mimi si mwandishi, wala sina mpango huo, ninachofanya ni ujumbe wakueleweka ufike BHAAASH! Sihitaji righting skills wala writing skills.
 
Back
Top Bottom