True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

Kwa waleta story humu umejitahidi sana
kuna mmoja alileta episode 1 na kupotea wadau wamemtukana na kumbembeleza lakini wapi, na yupo anacomment mada nyingine ila hadithi yake katelekeza
Nitaweka stori hii mpaka iishe wala sihitaji kubembelezwa, sema majukumu yanabana muda ila natamani kutupia kila muda.
 
Nitaweka stori hii mpaka iishe wala sihitaji kubembelezwa, sema majukumu yanabana muda ila natamani kutupia kila muda.
Aandika iishe ndo ulete mambo ya kusema sijui umebanana hatutaki kama uliona kubanana kutakuwepo kwann umeileta ungeacha siku upo free uilete
 
...54
Nilifika nyumbani giza likiwa limetanda sasa,
Babu akiwa anafaidi joto la moto, nilimpa salamu pia bibi ambaye alikua jikoni kuandaa msosi!
Oga haraka uje hapa tupange mipango maana hapa sasa tupo vijeba wawili.
Alitania babu,
Sasa mbona nakuona umekaa pekeyako au umeanza tena mikwara kama ya asubuhi? Nilijibu huku nikichukua karai lilokuwa limeegeshwa ukutani.
Sasa kumbe wewe unajiona bado mtoto wa shule wakati tayari ushaharibu mambo kwa mtoto wa watu? Yaani wewe muda si mrefu unakwenda kunyea ndoo! Alisema babu bila masihara,
Niliogopa sana, nani nimemfanya nini? Nilibaki nimeduwaa tu huku maswali mengi bila majibu yakinizonga kichwani!
Hahaaa Kaoge mdogo wangu nakutania tu, macho yamekutoka kama umekabwa koo, mwanaume hutakiwi kuwa muoga bwana, alisema tena!
Nilishusha pumzi kwa nguvu kisha nikamimina maji yaliyokua kwenye dumu la pembe nne na kuelekea bafuni.
Hata wakikukamata nitahakikisha unatoka wala haipiti miaka mitano,
Alizidi kunitisha mzee huyu wakati huu nilikuwa nakarbia mlango wa bafu!
 
...55
Acha mkwara we mzee nakama wakinikamata nitasema wewe ndo ulinituma.
Nilijikakamua na kumwambia ingawa moyoni nilikuwa na kimuhemuhe.
Hahahaaaa! Pumbavu, tena umejichanganya, hukupaswa kuoga bali ungeanza kutimua mbio kabla hawajafika. Aliendelea kutania babu wakati huu nilitambua kumbe ni utani tu.
Nichelewe wapi wakati kuna baiskeli yangu humo ndani haina kazi? Nilitania na kuongeza, ebu ikague kama pumzi inatosha ili nikiipanda iwe kamserereko tu.
Hiii! Sasa hapo kwenye usafiri wangu nitakufunga kabla hata wafungaji hawajakufata alikoroma babu na kweli utani ulikorea nasasa nilianza kumzoea babu yangu na kuvutiwa na ucheshi wake,
Wakati huu natoka bafuni alitania kwa kunong'ona, leo tunabadilishana mawindo dogo! Wewe utakula ng'homele
(nyama iliyobanikwa) akimaanisha bibi, namimi nitakula freshi akimaanisha yunge.
Hapo nipo tayari kabisa unajua bibi yangu bado kisu kabisa? Yaani humwangaliagi tu huko nyuma, nilitania huku nikizichapa hatua kuingia ndani.
Pumbavu nitakung'oa p..bu,
Alifoka babu!
 
...56
Nitoka ndani baada ya kubadili nguo kisha nikaungana babu pale kweny shikome, wakati huu bibi alikuwa anatenga chakula, tulikula ugali mzuri wa mahindi uliochanganywa na udaga uliotwangwa huku mboga ikiwa maharage yaliyosagwa na kuchanganywa na karanga, kiukweli mbaga hii niliipenda sana na mpaka leo hii mama watoto wangu huwaga ananiandalia kila mara! Pia kulikuwa na mboga inaitwa chubhu (ujimzoto uliochanganywa na samli na maziwa fresh) jamani kwa hizi mboga nilianza kusadiki maneno ya bibi jana kwamba nitaondoka huku nikiwa chibonge, kulikuwa na maziwa mgando pia.
Baada ya kula bibi aliingia ndani kulala nikabaki na babu ambae alinitaka nimsimulie yaliyotukia tangu asubuhi walipokwenda msibani mpaka waliporejea.
Nilieleza kila kitu bila kuacha hata moja kwani sasa nilimchukulia babu kama mchizi wangu,
Sasa sijui kwanini huyu binti anifanyie uchawi vile? Nilimaliza kusimulia na swali juu.
Kwanza nikupe pole kwa yote yalotukia, nishakwambia hakuna mtu atakugusa na hicho alokufanyia si uchawi bali ni..!
 
...57
Alichokufanyia ni kiini macho tu wala hakuna cha bundi, paka wala kupotea! Siku nyingine ikitokea hivyo we sonya msonyo mrefu na puuza ulichokiona, lakini kabla ya hayo ebu ngoja nije.
Alisema babu na kuingia ndani kisha akarejea na wembe mkuukuu na ungaunga ulokuwa umefungwa fundo kwenye kikaratasi! Alinitaka twende nyuma ya nyumba ambako alinichanja juu ya jicho na kunipaka dawa ile.
Sasa inatakiwa ungie ndani mwako ukiwa umefumba, hutaqiwi kuona mwanga wa moto, alitoa maelekezo babu.
Nilianza kutembea kuzunguka nyumba ile nikiwa napapasa, uzuri nilikuwa nyuma ya slopu nilokuwa nalala hivyo sikusumbuka kuupata mlango.
Niliengua mlango na kuingia ndani, nilifunga mlango nikapapasa kuelekea chumbani ambako kulikuwa na kitaa cha sola (solata) kilchokuwa kinawaka.
Nilikizima na kujitupa kitandani, kulikuwa na joto wala sikujifunika shuka, sikufungulia redio kwani pia ilikuwa na vitaa kidogo vya kuelekezea band kama ni fm ama mw.
Kutokana na uchovu uliotokana na kufanya mazoezi nipitiwa usingizi mapematu.
 
Kanyaga twende
 
Back
Top Bottom