Pettymagambo
JF-Expert Member
- Aug 21, 2017
- 1,490
- 8,227
- Thread starter
- #181
...51
Nilisikia sauti ya yule msichana, niligeuka nimwone,
Ajabu na kweli, alikuwa yeye amebeba ndoo ya maji kichwani!
Huyu kapitia wapi! Niliwaza, lakini pia maji kachota muda gani? Hapa simngojei,
Niliongeza kasi ya kuzichapa hatua kwa uharaka, lakini bado aliendelea kunisihi nimngojee,
Sikutaka kumwelewa,
Ebu ona hiki, nimekuletea wewe, alichimba mkwara, lakini sikutaka kumwelewa.
Nilikaza mwendo sikutaka kumsikiliza,
Sasa unaenda wapi huko? Nilistuka! Mhh! Nipo wapi hapa? Nilishangaa, nilikua nimekivuka kisima na kuendelea mbele, nilishangaa, wakati nasikia sauti yake akiniomba nimsubiri, nilikuwa nimeshakaribia nyumbani na nilianza kuuona ule mwembe wa nyumbani kwa babu, sasa imekuaje nimefika huku? Nilimkata jicho la mwana ukome yule msichana na kumwambia,
Sipendi upumbavu mnaonifanyia, mbona wasichana wadogo mnakuwa wanga tena waziwazi bila kujificha?
Nani kakuroga? Aliniuliza.
Sasa nimefikaje hapa wakati nilikuwa nakaribia nyumbani? Nilimwuliza wakati akiwa kanifikia.
Ebu geuka,
Niligeuka haraka..!