Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kimya mzeee...62
Sasa unahisi nani anaefanya mambo haya na kwafaida gani? Nilimwuliza yunge,
Mh! Watu wakijiji hiki wakiamua kukuchezea hawana cha sababu wala nini, alijibu.
Sasa inakuwaje wanakuja kufanya michezo yao hapa wakati inasemekana babu ni kiboko yawote na anaogopeka kwa ulozi?
Kwanza nikwambie tu, babu yako sio mchawi kama wanavyovumisha watu, kinachotokea ni kwamba, yeye babu katika kilimo chake anawekaga zindiko ambalo hakuna kati ya wanakijiji wote anaeweza kulitegua ili aweke chuma ulete, badala yake ukimwekea chuma ulete utakua unamwongezea mazao yako shambani mwake bila wewe kujua,
Hivyo kitendo hiki hupelekea babu yako kuvuna mazao ya uhakika kila mwaka na kupelekea chuki kwa wananzengo dhidi yako nahapo huanza kuvumisha ni mchawi! Alieleza yunge na kuendelea,
Kuhusu hii michezo ya mapaka na mabundi ni mtu wa karibu na familia hii ambae na ukitaka nitakuonesha ila uwe na kifua usije ukayamwaga kwenye kuku wengi, alifafanua kwa kirefu na kunitazama kungoja ruhusa yangu ili kama nnakifua anioneshe...!
Atatuuua huyu jamaa...Kimya mzeee
JigoBhebe Pita zhogo Ahaaa...
Pita mwana fuba ali ku mbiti......65
Nilifumba na kuruka juu kwa nguvu, ajabu tayari nilikuwa juu ya ule mti nikiwa nimeshikilia tawi la ule mti ambao sikupata kuujua jina mpaka leo.
Nakuacha hapa, naomba ukaze moyo kwa utakachokiona, vinginevyo wakikuona utakuwa kitoweo, alitahadharisha.
Sasa nilianza kuogopa hata kabla sijaona nini nimekuja kuoneshwa, yaani mimi niwe kitoweo? Ngoja tuone, niwaza.
Chukua upembe huu, usogeze karibu na sikio lako, nitakuwa nakupa maelekezo ya nini ufanye kupitia upembe huu, alimaliza yunge kisha akanivika miwani iliyotengenezwa kwa manyoya, miwani hii haikuwa na galasi kwenye mboni ilikuwa ya fremu pekee.
Kwaheri, alisema na kupotea pale kitendo kilichonifanya niogope na kuanza kuangaza juu yamti.
Nilitupa macho mbele ya ule mti kama mita 80 hivi ambapo niliona moto mkubwa unawaka.
Nilishangaa kumwona pale yunge huku akiwa kajifunga nguo nyeusi kusitiri matiti na nyeti zake tu.
Ghafla niliona vumbi kwa zito linatimka kwa mbali ambapo nikaza macho nione nini kile.
Nilimwona bibi juu ya fisi mkubwa mno.
Mh?
Kuna baadhi ya mavichwa ngumu yanabishaTuko ndaani ndani kabisa usukumani........
Sure. This is a true story. Kuna baadhi ya vitu najua vipo hapo Shy.
Wanaobisha hajawah fika usukumani....Kuna baadhi ya mavichwa ngumu yanabisha
Ohoooooo kumekuchaaa...66
Basi nilistaajabu sana, sasa nikawa natumbua macho kwa makini kuona kila fisi atakefika kama babu nayeye atakuwepo, waliendelea kuwasili pale watu wale kila mtu kwa mtindo wake, kuna waliotokeza ghafla wakiwa wamepiga goti moja na mkono mmoja kushika chini! Wengine walikuja wanapaa kama ndege, kiujumla uwasiliji wawatu wale ulikuwa burudani iliyoogopesha.
Ghafla nilisikia sauti pale chini ikiamrisha fumba macho na uruke juu,
Nilitaka kutazama chini nione kuna nini, lakini kabla sijafanya hivyo nilisikia sauti ya yunge kupitia upembe ule akinitaka nisijishughulishe na wale kwani kuwatazama tu, watasisimkwa miili hivyo kuhisi uwepo wa mtu pale.
Mara kidogo nikasikia sauti ileile ikitowa maelekezo kwa mtu yuleyule kwamba ajikaze ili aone kitu ambacho huwa anaambiwa na yeye kutoamini, wakati huu sauti ilisikika usawa wangu juu ya mti upande wangu wa kulia, nikajua pale tupo wawili sasa ambao tumeletwa kila mmoja kwa mpango wake.
Kule kilingeni kwa wachawi kulianza kuchangamka na watu walikuwa wengi sasa.!
watu gani tena?