True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

UANDISHI WAKO WA KITOTO UNAWEKA MANENO MENGI YA UONGO AMBAYO KWA WATU WA KIJIJINI HAWAWEZI YATAMKA. UNATAKA KUONESHA UMECHANGAMKA SANA MPAKA UNAHARIBU. BADO JIFUNZE KUSIMULIA IONEKANE KAMA YA UKWELI. WEWE UNASIMULIA INAONEKANA NI UONGO KABISA.
 
Hii ni chai,saa moja jioni kuku hajarufi bandani,saa moja jioni anaenda mashineni kusaga,mwezi december saa moja ni giza sana huko
umeona eeehhh..... jamaa anadhani anasimulia watoto wenzie. mara babu yake alimtuma kisimani mara anaenda bombani anajichanganya tu. na uandishi wake dogo anaweka maneno ya kitoto tu hajui hata kusimulia.
 
dogo muongo sana. halafu hatumii akili kudanganya maana hana.. anafikiri sisi wote madogo wenzie
 
Uzi umekuwa wa ki…….

Nothing to hear
 
Ukitaka kujua humu kuna watu hawana akili hata ya kuvukia barabara siku moja njoo na story yako unayotamani kushare na jamii

Utasikia Muongo, umecopy sio wewe, chai hii dah

Mtu anakwambia nimelala na njaa wewe unamwambia "Muongo" ulikuwepo?

Kuna siku nilitamani kushare na jamii na kuwaelezea simulizi flani jinsi nilivyofanikiwa kumkamata mwizi wa mitandaoni na zile njia nilizotumia na wao wezi njia wanazotumia

Yanii mimi mwenyewe ndio nimemkamata huyo Mwizi ,
Na Rb ninayo mfukoni anatokea mtu humu hata hana anachokijua anakwambia tu chai hio Muongo, umecopy wewe

Mara nyingi tunakosa kupata taarifa mbali mabli kwa sababu ya watu wachache wenye Tabia za utoto utoto na za kijinga zinawakatisha tamaa wasimuliaji


Binafsi nikifunga hadith au simulizi humu nikiona alijanipendeza naondoka bila ya kuaga sio kucomment vimaneno vya kuwakera wengine wanaofatilia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…