True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

...30
Nimekuja nzehe, umenieurahisha sana leo, alijibu yunge!
Mimi: nimekufurahisha vipi mchumba?
Yunge: ulivyomkaushia yule binti mchawi mpaka ameamua kuondoka!
Mimi: msichana mchawi nani?
Yunge: nani alikuwa hapa dakika kama 10 zilizopita? Kiufupi nimeona yote tangu anabisha hodi mpaka alivyoondoka, nilidhani utajipendekeza kwake kumbe nilijidanganya,
Nilijiona nimepiga bao la kisigino kama lile chama dhidi ya nkana,
Mimi: jana ulinitahadharisha juu ya huyu dogo, hivyo nilikuelewa kabisa,
Yunge: haya nisalimie mimi dada yako!
Mimi: dada yangu? Umeanza tena kunikwepa?
Yunge: kukukwepa nini, unataka nikuite nani ikiwa tumelala kitanda kimoja na hakuna kilichotendeka?
Mimi: sawa, shikamoo bibi,
Yunge: nani bibi yako hapa?
Mimi: wewe hapo, si unautaka ukubwa?
Yunge: sasa kwani uwongo mimi si mkubwa kwako?
Mimi: ndo nakuamkia shikamo bibi,
Yunge: ninazawadi nzuri kwako, twende nyumbani nikupatie,
Mimi: poa twende.
Tuliinuka na kutoka nje, nilifunga milango yote tukaondoka,
Kabla ha2javuka mwisho wa kiwanja...!
UANDISHI WAKO WA KITOTO UNAWEKA MANENO MENGI YA UONGO AMBAYO KWA WATU WA KIJIJINI HAWAWEZI YATAMKA. UNATAKA KUONESHA UMECHANGAMKA SANA MPAKA UNAHARIBU. BADO JIFUNZE KUSIMULIA IONEKANE KAMA YA UKWELI. WEWE UNASIMULIA INAONEKANA NI UONGO KABISA.
 
Hii ni chai,saa moja jioni kuku hajarufi bandani,saa moja jioni anaenda mashineni kusaga,mwezi december saa moja ni giza sana huko
umeona eeehhh..... jamaa anadhani anasimulia watoto wenzie. mara babu yake alimtuma kisimani mara anaenda bombani anajichanganya tu. na uandishi wake dogo anaweka maneno ya kitoto tu hajui hata kusimulia.
 
WAJUAJI WAKIJA WATAKUULUZA

Mpaka sasa huyu bwana hajafikisha masaa 24 hapo ugenini kwa Babu yake kifupi alifika saa 12 na mpaka Sasa n saa nane mchana lakini sasa

👉Ameshajua kuku huwa wanakaa WAP mchana?
👉Kaonana na msichana jion nayeye akiwa mgen lakin usiku alimfungulia geto?
👉Saa 11 asubuh unasindika mtu ambae hujui kwao n wap na vp heshima yako kwenye mji husika ipoje?
👉Inakuaje we n mgen tena mjukuu ulipewa jina lababu alafu wote wanakuacha walijua we n mgen bila hata chakula Cha mchana?
👉Hukuwah kulala na msichana Ila mpaka sasa umeshalala nae na bado una shauku ya kupata mwingine.(mkojo wa kwanza kutoka kwa Mara ya kwanza huwa unakuchukua akili kwa aliyekukojolesha)
👉Unapata ujasiri gani kutoa nguo zako na shuka la Bibi yako liende kwenye mji usioufahamu ili Hali ulishataadhirishwa na Mambo ya ushirikina?
👉Muda n mchache Mambo n mengi.



Jamani achen mihemko hapa tupite Kama kuburudika na kuongeza kitu kichwan tusiwe serious Sana.
dogo muongo sana. halafu hatumii akili kudanganya maana hana.. anafikiri sisi wote madogo wenzie
 
Ukitaka kujua humu kuna watu hawana akili hata ya kuvukia barabara siku moja njoo na story yako unayotamani kushare na jamii

Utasikia Muongo, umecopy sio wewe, chai hii dah

Mtu anakwambia nimelala na njaa wewe unamwambia "Muongo" ulikuwepo?

Kuna siku nilitamani kushare na jamii na kuwaelezea simulizi flani jinsi nilivyofanikiwa kumkamata mwizi wa mitandaoni na zile njia nilizotumia na wao wezi njia wanazotumia

Yanii mimi mwenyewe ndio nimemkamata huyo Mwizi ,
Na Rb ninayo mfukoni anatokea mtu humu hata hana anachokijua anakwambia tu chai hio Muongo, umecopy wewe

Mara nyingi tunakosa kupata taarifa mbali mabli kwa sababu ya watu wachache wenye Tabia za utoto utoto na za kijinga zinawakatisha tamaa wasimuliaji


Binafsi nikifunga hadith au simulizi humu nikiona alijanipendeza naondoka bila ya kuaga sio kucomment vimaneno vya kuwakera wengine wanaofatilia
 
Back
Top Bottom