True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

Nipo makini nafatilia mkuu, ila siku ukifunga ukurasa nitakufata PM nina memaa kwajili yko ndugu. Kwa hii kazi uliojitolea kwa jili ya wengi sio kazi ndogo kabsa kwanza nikupongeze unajitahidi sana👏👏.
Kukaa chini na kuanza kuyakumbuka matukio yaliyopita kisha kuyapanga kwenye mtiririko wa kuvutia kwakweli sio jambo dogo. Wengi wetu humu ndani tunashindwa ila sio kwamba vyakusimulia hatuna lahasha, ila tatzo ni misingi tulio jijengea tangu tukiwa masomoni.
Ni rahisi sana kusikia watu wakijitetea kwa kauli tu; Walio soma art wapo vizuri..HKL ni wepesi.. nk. Ila watu wapo walio pitia mambo mazito sana mkuu believe me!! ni vile tu hawana mwandiko. (wanaogopa kejeli za humu, tukijirekebisha kwahilo tutafaidi na kujifunza mengi muno).
..📢OVaa..
 
150
Niliogopwa na watu wote, si wakubwa tu, bali watoto pia, si wanawake tu, bali wanaume pia, nikaona sasa hii hali sio na bora nibadili zindiko ama adhabu kwa watu wavivu kufanya kazi ila wanataka wavune kuliko hata wanaofanya kazi, nikaweka zindiko ambalo mtu akija kufanya michezo yake shambani mwangu badala ya kuniibia basi yeye ndo huniletea mazao yake, alinieleza kwa urefu babu.

Pia licha ya yote yale ya watu kudhurika kila wafanyapo michezo michafu shambani, huwezi amini watu hawakukoma kuja tena wakiwa wamejipanga kwa mbinu mpya, na walipoona sasa hawadhuriki wakajua tayari wameshaniwezea, hawakujua kama nimebadiri zindiko na matokeo watayaona wakati wa mavuno, alimaliza kunieleza babu.

Inawezekanaje babu mtu amekuja mikono mitupu na akuongezee mazao kivipi? Nilimwuliza babu.
Mtu anaanza kukuharibia ubora wa mazao yakingali bado machanga kabisa, yaani utaona mimea yako haistawi vizuri ilihali huduma zote muhimu unaihudumia, sasa kama hukujipanga vizuri utalia wakati wa mavuno, yani unagawana nao.
 
Kanda ya ziwa kwa uchawi nawapa 5stars rating
 
151
Ila kama umejizatiti badala ya kukuchukulia watakua wanakuletea mazao bila wao kujua, alijibu babu na kuongeza, kwahio mwanangu kilimo cha sasa bila kukikinga ni kazi bure tu, utakuwa unafaidisha watu tu.

Tulipiga stori nyingi huku babu akinambia alikuwa anataka kuukomesha ulozi wa bibi hapo baadae kwani aliamini lazima tu ipo siku bibi atataka kumtoa babu awe kitoweo kwa walozi wenzie.

Tuliondoka na kurudi nyumbani mida ya saa 7 kisha muda mchache mbele walikuja wale jamaa vibarua kwaajili ya msosi, tulikula msosi ule huku mimi nikitengwa nile pekeyangu.

Niliingia chumbani mwangu nakujilaza baada yakula na usingizi mwepesi ulinichukua mpaka mida ya saa 11 jioni nilipoamka na kwenda nje kuandaa kuni kwaajili ya moto.

Leo mapema tu? Alikuwa bibi akiniuliza mbona nawasha moto mapema tu.
Naona leo kuna baridi sana hivyo ngoja niandae mapema, nilimjibu bibi ambae muda mwingi alikuwa bize na shughuli za pale nyumbani.

Muda kidogo aliwasili yunge mdogo na kunisalimia kwa upole.
Nimeambiwa unaumwa mchumba.
 
152
Nikweli jana homa ilinibana na kichwa kikawa kinaniuma sana ndipo babu akanitengenezea dawa, ila kwa sasa najiona afadhali kidogo, nilimdanganya yunge mdogo.

Samahani nzehe, naweza kuja usiku wa leo tukaongea jambo muhimu sana? Aliniuliza kwa upole yunge mdogo ambapo nilimkatalia kistaarabu bila kumchukiza kwa kisingizio naumwa hivyo nahitaji kupumzika.

Aliondoka huku nikiwa nimemwahidi siku nikijisikia vizuri nitamwambia aje tuongee ishu yake hiyo ya muhimu huku nikiwaza atakua anataka sex tu.

Siku ilofuata mida ya saa 6 bibi aliniomba nimsaidie kufata maji japo dumu 1 kwani alikuwa kaishiwa maji ya kunywa na vibarua karibu wanakuja kupata msosi.

Nilifika kisimani na kuwakuta wasichana kadhaa na tatu akiwemo.

Kwahio ukanifanya mtoto mdogo kuniweka nakungoja hutokei mpaka nikachoka? Alinidaka tatu juujuu, alafu sijui unaringa nini tu, kwahiyo unajiona mzuri sana ama hizo chale alizokuchanja babu yako ndo zinakupa kiburi? Naunavyonuka jasho sijui umeambiwa usioge wiki nzima ili dawa ikukae sawasawa?
 
Tatu midomo yake haina breki kabisa unaweza mpiga makofi.

Mnalalaje huku jambo linaendelea

Gily Antonnia Dejane Kelsea Numbisa
 
153
Aliendelea kuniporomoshea maneno ya shombo tatu nikiwa nangoja zamu yangu ya kuchota maji na kweli aibu flani ilinikumba kwani chale zilionekana waziwazi mwilini mwangu.

Sasa kama umepewa sharti la kutokuoga mimi nakuosha ili tuone sasa maana huwezi niweka nakusubiri kumbe wewe unawanga na babu yako huko, aliongea tatu kama masihara kweli nilishtuka nimemwagiwa maji kifuani, mwaaa!

Nilishangaa na hasira zikanipanda mno, nilimfata pale juu ya bomba na alikua akiningoja nimfanye nachotaka ili anioneshe umwambawake kwani alisimama na kuniangalia kwa dharau na kujiamini mno.

Paah! Nilimweka kofi 1 la ujazo ambalo lilimpeleka chini huku akiugulia maumivu.

Mh! Mh! Mh! Mh! Aliguna huku akiwa pale chini, alinikazia macho yake kwa hasira nami nikayakaza yakwangu, taratibu joto la mwili likawa linanipanda na ghafla zile chale zote zikawa zinawasha huku zinacheza mno, tuliendelea kukaziana macho na ghafla tatu alipiga yowe la maumivu huku akishika kichwa.

Joto lilinishuka ghafala na tahamaki chale zinatoa damu!
 
Tatu hajaaribu dawa kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…