True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

126
Nimekuwa na hisia siku nyingi kwamba huenda mke wangu nae anajishughulisha na kikundi hicho cha walozi, lakini kama hujui ni kwamba mtu ukijiingiza anga hizo lazima kuna kiingilio utakitoa (kafara ya mtu wa karibu yako zaidi) lakini licha ya kutega mitego yangu yote sijawahi kumnasa bibi yako na kujihakikishia kwamba ni mshirikina, japo niponae miaka mingi sijawahi kuona dalili zozote za kumhusisha na ulozi japo ndoto zangu huwa zinaniambia ni mtu hatari sana.

Jambo lingine ambalo hunifanya nipuuze mawazo yangu ni kwamba tangu nimemuoa hatujawahi kufiwa na mtoto, hata mjukuu mmoja, na hata mimi mpaka leo nipo hai, je kama anajihusisha na ulozi basi yeye anatoaga sadaka gani? Alizidi kuongea babu.

Ebu sasa nambie ulimwona ama hukumwona? Alinitega babu.

Niliinamisha kichwa pembeni nikiwaza kwamba nikimwambia babu akajua kwamba bibi ni mlozi itakuwaje pale nyumbani, siuvunjifu wa amani utatokea? Naikiwa hivyo pale hapatakalika kamwe, niliwaza sana.

Basi usjali mwanangu, uso wako tu unaeleza wazi, inuka.!
Hatari na nusu
 
Back
Top Bottom