120
Alikuwa anaimba nyimbo za malenga wa kisukuma waliokuwa wanashindana zamani enzi za mababu.
Tulifika pale bombani na babu aliwasalimia wote waliokuwa pale, nilitupa jicho kuona kama nitamwona yunge mkubwa, lakini sikufanikiwa kumwona na badala yake nilimwona yunge mdogo ambae tulipokutanisha macho tu, aliangalia pembeni kama mtu ambae hajafurahishwa na uwepo wangu.
Tuliendelea na safari kwa muda wa dakika 10 tukayafikia majaruba mengi yaliyonyooka huku nyasi laini zikiwa zinakaribia kumezwa na maji, kwa mbele kidogo kulikua na majembe matatu ya kukokotwa na ng'ombe (plau) yakiigeza ardhi na kufanya zile nyasi laini zimezwe na ardhi ile.
Haya yote ni majaruba yangu, na hawa wanatulimia sisi, alisema babu na kuongeza, hapa kila mwaka napata junia 30 mpaka 40, na shamba silimagi lote, ila kwa mwaka huu kwakuwa umekuja mdogo wangu nitaongeza majaruba manne kwaajili yako, hapa utakuwa na uhakika wa kupata junia 15 mpaka 17.
Kiukweli nilifurahi mno, kwani nilianza kupiga hesabu ya gunia 15 x 50000 =750k.