Pettymagambo
JF-Expert Member
- Aug 21, 2017
- 1,490
- 8,227
- Thread starter
-
- #1,361
165
Babu aliongea maneno mengi kwa kikabila ambapo baadhi niliyaelewa na mengine yalinipita bila kuambulia maana yake.
Nilimsikia akisema ndugu zangu, nimeishika leo hii silaha yenu ya maangamizi si kwa lengo la kulipa kisasi ama kumwadhibu mbaya wangu, bali naomba msaada kijana wangu ameonewa na msichana ambae ni mkuu wa miliki ya giza kwa upande wa kati, tena pasipo kujua aliingia nae maagano ya damu kwa kumvua usicha wake, sasa anataka kumsumbua na mimi sitaki kumwumiza binti yule, kama nilivyokwisha kuwaambia ndugu zangu sitaki tena kumwaga damu ya mtu, nataka niishi maisha yangu ya uzeeni kwa amani kabisa, aliongea maneno yale babu akiwaomba watu wasioonekana.
Nikiwa nimefumba macho huku nayatafakari maneno yale ya babu, ilionekana zamani alikuwa mwanga huyu naye, kwani amejuaje kwamba yunge alikuwa ni mkuu wa kanda ya kati? Pia nilimsikia akisema hataki tena kumwaga damu ya mtu, huyu mzee ni mlozi naye tu, niliwaza.
Shusha mkono chini na uunyoshe kwa mbele, alinambia babu nami nikafanya vile.
Paaah!