163
Bibi alirudi nduki kutoka ndani na alikuja tulipokuwa tumesimama na babu, aliushika mkono wangu na kunivuta tukausogelea moto, bibi alikisogeza kiganja cha mkono wake karibu kabisa na moto kwa muda kama wa sekunde 10 kitendo kilichonishangaza na kujiuliza inamaana haungui?
Alinishika mkono wangu kwa mkono wake wa kulia huku nikiwa nimeanza kulia kutokana na maumivu ya ile mikia, haraka bibi aliutoa mkono kwenye moto kwa haraka na kunichapa kofi pale ilipokua inazama ile mikia, nilipiga kelele za maumivu lakini babu alikuwa amenikamata vizuri na tayari bibi alisharudisha mkono wake karibu na moto kama mwanzo, nilianza kuhisi ile mikia imezama yote mwilini mwangu na ilianza kujiviringisha kitendo kilichonipa maumivu makali mno, nilipigwa tena kofi kali na la moto kwelikweli na bibi kama mwanzo, maumivu makali niliyasikia na nilitoa sauti ya maumivu, sauti ile nadhani ilifika kwa majirani.
Mh! Tumechelewa, aliongea bibi kwa kukata tamaa huku akianza kumtupia lawama yunge mkubwa kwa kitendo alichonifanyia.