True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

168
Niliona mafisi makubwa mawili yenye macho yang'aayo yakiwa yanamvuta babu kuelekea vichakani huku kila moja limeshika kwa meno mkono mmoja wa babu ambae macho yake bado yalikuwa yanang'aa kama zamani.

Nilichanganyikiwa kumwona babu yangu kipenzi akiwa anavutwa chini tena na mafisi, hapa niliijiwa na picha mbaya sana kichwani, yaani babu yangu kipenzi aliwe na fisi? Nililia kwa sauti lakini hakuna aliyetokea.

Nilitimua mbio na mpaka nikamfikia babu na kumshiki miguu kwa ujasiri, nilianza kushindana nayale mafisi kumvuta babu ambae alilia kwa maumivu ya kuvutwa huku na huku, nilimwachia babu kwa ghafla na yale mafisi yalipigiza matako chini kwani hayakutegemea kama ningefanya kitendo kile ghafla vile.

Ondoka hapa hatuna shida na wewe, ilisikika sauti ya mwanamke kutoka kinyani mwa mmoja wa yale mafisi, nilishangaa sana fisi kuongea.
Naomba mniachie babu yangu msimle nyama, nilibembeleza.
Mpumbavu sana wewe, ondoka haraka kabla hatujakutafuna, aliongea kwa sauti yule fisi mwingne.

Siondoki, nililia mno.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Punguza Kamba basi Mwamba
 
170
Ndio babu nilifumbua macho uliponipiga na kitu mkononi, kwani nilimsikia yunge analia kwa maumivu akisema eti bhuhabhi mmeamua kumwua mtoto wenu? Ndo nikafumbua nimwone huyo mtoto, nilijitetea.

Kweli ulisikia sauti ya yunge? Aliuliza babu ambae nilimhakikishia ilikuwa sauti ya yunge mkubwa.

Basi tupumzike ila leo nauna mwisho wangu, aliongea babu kwa masikitiko na kukata tamaa.
Hapana babu, hakuna wa kukugusa upo na mimi, nilimtia moyo babu huku nikiwa sijui nini kilinipa jeuri ya kusema vile.

Nini kinakufanya ujiamini hivyo mjukuu wangu? Aliniuliza babu huku akijitaidi kutabasamu ilihali akiwa na maumivu.

Swali lile lilinifikrisha kidogo, nikawa najiuliza mimi mwenyewe, eti kweli, ni nini kinachonipa jeuri ya kutunisha kifua na kumwaminisha babu kwamba alikuwa katika mikono salama kwa uwepo wangu mimi ikizingatiwa nilikuwa nalia kama mtoto mdogo muda mfupi uliopita.

Huku babu akinitazama na kungoja nitampa jibu gani,
Ghafla nilikumbuka kitu, niliangaza chumbani nisione nichokitafta, vimeenda wapi?
 
Doh, Bibi yako keshafanya yake
 
Back
Top Bottom