True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

...72
Huyooo! huyoon! Mtangizieni, mleteee mletee! Walipiga kelele wale watu wa ajabu nakunifanya niongeze mbio huku hofu kuu ikinijaa kwani sasa nilimwona yule mzee wa kiwanjani na lile jimama lenye fisi mkubwa kuliko wote wakiwa wamebakiza hatua kama 20 tu wanidake.
Zungusha upembe kwa nyuma, uwe kama unamkata mtu panga, usigeuke wala kusimama, sauti kutoka kwenye ule upembe ilitoka!
Nilieanya kadri ya maagizo, yaani chwaaa!
Nilisikia vilio kwa nyuma,
Uwiii! Twafaa! Mayheee!
Zilikuwa ni kelele za maumivu za watu wale wakigugumia.
Niliendelea kutoka nduki hatari huku jasho sasa likiwa limekubali kama mvua za elmino, muda kidogo sauti ya upembeni ikasikika tena, wanakukaribia tena, ebu geuka uone, niligeuka haraka na kumwona mzee wa kiwanjani na lile jimama ndo bado wameniungia huku wakiwa na hasira,
Tutakukomesha leo mshenzi wewe! Alisema mzee yule kwa hasira,
Fanya kama mwanzo watakukamata sasa.
Nilizungusha upembe kwa nyuma.
We mpumbavu unafikiri sisi ni watoto wenzio? Simama hapo kabla sijfyeka shingo..
Woooooh
Lyambalii yambalii ya mfipaaaa
Santamaligaaaaa
 
...73
Nasema simama utuambie nani kakuleta anga zetu kabla sijakugeza nyama, alizidi kunitisha mzee yule ambae sasa niliisikia sauti yake ikiwa karibu kabisa na mimi.
Kwahofu ya kukamatwa na wachawi hawa niliongeza mbio huku nikisahau kabisa kuusikiliza upembe ule.
Hahahaaa! Yaani we mbwa umekubali kuyatoa sadaka maisha yako kirahisi hivi? Sasa nafyeka shingo kabla sijainywa damu yako tamu na nzito, alizidi kunitsha mzee yule huku vishindo vya nyayo za mafisi nikivisikia.
Nikiwa nimesahau kuutegea sikio ule upembe nilishtuka unatikisika mkononi mwangu, ndipo nilipousogeza karibu na sikio ambapo nilimsikia yunge akiniamuru niutupe ule upembe kwa mbele yangu kisha niutambuke nikiwa nimefumba macho haraka sana kwani yule mzee alikuwa anajiandaa kurusha panga anifanye manyamanyama kama ya kule kilingeni.
Haraka kama radi niliutupa upembe ule kwa mbele kama hatua mbili kisha nikafumba macho na kuuruka kwa speed ya hatari.
Mayeee twachaa! (tumekwisha jamani) nisauti ya maumivu ya yule mzee aliekaribia kunikata..!
 
...74
Nilishangaa ghafla nikiwa pale sebleni kwangu tena mlangoni ambapo tuliondokea.
Unabahati sana, usahaulifu wako wa kusikiliza maagizo ungeniletea shida, yaani nilikua nakupa maelekezo muda mrefu nashangaa hunisikii mpaka nimeamua kutumia ngoma kubwa ili ikushtue maana sauti yangu ilishindwa kukushtua kabisa, alisema yunge akimaanisha ulemtikisiko wa upembe ulitokana na yeye kupiga lingoma kwani sauti yake haikutosha kunistua kabisa.
Nilibaki kumtumbulia macho tu huku picha yote ya matukio niliyo yaona muda mfupi uliopita yakijirudia kichwani mwangu, yaani yunge huyu anaeonekana mpole na mstaarabu ndo anatoa ruhusa ya kuchinja na kunywa damu na kula nyama za watu kwa wale wachawi? Dah hatari.
Nilimlaumu pia yule jamaa aliepiga kelele kwamba mama yake anamchinja mwanae, nilitamani kuona kama yunge na bibi wangekula nyama ya binadamu.
Umejitahidi mpenzi kwa mara ya kwanza siyo mbaya, umemwona mwenzio aliepiga kelele kwa kushindwa kujikaza? Yule wameshamgawana nyama na kesho kutakuwa na msiba kijijini...!
 
...75
Msiba tena? Nani atakufa?
Niliuliza maswali dabo.
Ngoja kukuche utaona, alijibu.
Vipi yule mzee anaependa mpira na yule mwanamke mnene nini kilitokea baada ya mimi kuuruka upembe maana nilisikia wakilalama kwa maumivu makali, nilihoji.
Wale sasa walijikuta wamelivaa zindiko la babu yako, waliungua moto ila sema mafisi yao yalinusa hatari hiyo na kugeuka haraka, alijibu yunge.
Sasa mbona umewageuka na kuwaumiza wenzio? Nilimwuliza tena,
Niliahidi kukulinda muda wote inapowezekana na kwahilo sina chaguo lingine, alijibu.
Vipi kuhusu bibi hatojua kama nimemwona?
Hajui chochote japo alikuwa na wasiwasi mwingi kule kilingeni lakini jambo muhimu kwako ni kutoonesha tofauti yoyote kila unapoongea ama kutazamana naye, alijibu yunge.
Je wewe ni mkuu wa wale wote mpaka wakusikilize vile? Nilimwuliza.
Nikweli mimi ni kiongozi wao na ndo maana nimeweza kukukinga wasikukamate, kama ningekua na nguvu sawa na wengine basi leo ungekamatwa na kuliwa nyama kama yule aliyepiga kelele! Alijibu.
Nawewe unakula nyama ya mtu?
 
Naomba mungu nisije pangiwa kazi mikoa yenye uchawi kiasi hicho mbona ni maajabu haya , ila endelea basi na story za kunyanduana mbona umeacha😎😎
 
Back
Top Bottom