True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

...95
Nilirudi ndani baada ya kukumbuka sikuwa najua ni nyumba ipi analala kati ya tatu zilizokuwepo kwao yunge mdogo, niliingia ndani na kulala, usingizi haukupita kwa sababu ya ndoto ile ya kutisha.
Sikujua usingizi ulinichukua muda gani kwani nilishtuka kutoka usingizini jua likiwa limechomoza, kulikuwa kumepambazuka sasa, niliamka na kuelekea nje ambapo nilimkuta bibi anaosha vyombo, nilimsalimia kisha nikaingia jikoni kuchukua madumu ili nifate maji.
Kitendo kile kilimfurahisha mno bibi kwani alikuwa ananisifia sana na kufurahishwa na ujio wangu pale.
Kwa hali hiyo yunge atakuwa amepata mme kwelikweli, yaani mpaka namwone wivu mke mwenyangu huyu, alitania bibi bila kujua mjukuu wake mawazo yamehamia kwa yunge mdogo.
Sasa bibi kuchota maji mbona kawaida yangu, na hata nyumbani namsaidiaga mama hata kuosha vyombo, nilimjibu bibi huku nikianza kuuchapa mwendo kuelekea bombani.
Niliwakuta wasichana wengi pale wakiwa wamepanga foleni kungoja zamu ya kuchota maji na miongoni mwao alikwemo yunge mdogo.
 
...96
Habari za asbuhi kina mama, nilisalimia kwa aibu kwani kulikuwa na kina dada zaidi ya 15 pale na mzee mmoja ambae alisimama pembeni akingoja vibebeo vyake vya maji vijazwe, wadada wale walimpa heshima ya kumchotea kwanza ingawa hakuwa amefikiwa zamu yake.
Woliitikia wote kisha nikamsabahi mzee yule ambae baada ya dakika 5 aliondoka.
Mbona yunge hujaitikia jirani yangu? Nilimchokoza yunge mdogo ili anitazame kwani kiukweli pale sikuona msichana mzuri kama yeye.
Mbona hata tatu hajaitikia, wewe umeona yunge pekeake ndo hajaitikia? Alijibu na kijembe juu mdada alieonekana anamdomo kuliko wote pale.
Tatu ni yupi kati yenu ambae anaroho mbaya mpaka asiitike salam yangu? Niliuliza.
Ni mimi hapa, alijibu yuleyule mwongeaji mkuu.
Sasa unaonesha tabia mbaya mbele ya mchumba atakuoa nani? Nilimtania.
Kuolewa kwenyewe ndo kwahao wazee? Heri kukosa mme, alijibu jibu ambalo sikulipenda kabisa.
Niliona pia baadhi wanzie pale hawakupendezwa na majibu ya tatu.
Nawe tatu uchungage mdomo wako sio kulopoka tu kama chizi.
 
...97
Alichamba yunge mdogo na kuongeza, uwe na breki mdomoni basi, mtu anakuongelesha kirafiki wewe unajibu hovyo tu, sio vizuri hivyo tatu, alimaliza yunge ambae aliungwa mkono na wadada karibia wote walionekana kutofurahishwa na majibu ya tatu.
Alikaa kimya tatu huku aibu ikiwa waziwazi usoni mwake.
Basi walikuwa wakichota maji na kuondoka kimafungu mafungu kutokana na urafiki baina yao, hatimae ilifika zamu ya yunge mdogo ambae alikuwa akinitazama kwa aibu nadhani ni kutoka na kosakosa za jana.
Beba twende, alinambia yunge mdogo akinitaka nibebe madumu yangu ambayo yalikuwa na maji tayari.
Ameyajaza muda gani wakati kulikuwa na ndoo kama 5 kabla ya zamu yangu? Niliwaza, inamaana huyu anafanya uchawi mchana kweupe tena mbele ya watu?
Alikuwa ameshabeba ndoo ya maji na kuanza kuzipiga hatua kuondoka.
Nilibeba dumu zangu na kumfata yunge mdogo ambae alikuwa anatembea taratibu ili nimfikie.
Umenichotea maji muda gani? Nilimwuliza.
Achana na hayo bwana, alinikatisha.
Sawa lakini jana ulinikakomesha kwakweli.
 
...98
Achana na hayo, mie bado mdogo niliogopa utaniumiza, alijibu kwa kudeka yunge mdogo.
Nikuumize nini, kwani nilikuwa na mapanga ama mavisu?
Hapana, ila iposiku utafurahi japo unaonekana wewe ni kichomi (mhuni) sana, alijibu yunge na kunizodoa.
Mimi Kichomi nimefanya nini? Niliuliza kwa pupa.
Yaani wewe kila mwanamke ukiongea nae ni mchumba wako? Sijapenda tabia hiyo, kama umempenda huyo unambie mapema nijue, alilalamika yunge mdogo ambae alionekana kutokua na utani.
Jamani yaani huyo msichana mwenye sura na mdomo mrefu anakupa wasiwasi? Nlimtuliza.
Nyie wanaume hamtabiliki, mchumba mchumba mpaka unamwingiza chumbani mimi sitaki, alisema.
Mimi nakupenda peke yako tu, bila shaka unajua kwamba hapa kijijini hakuna msichana mrembo kama wewe, sasa mimi nimtake huyo msichana mwenye maneno machafu wa nini sasa, nilijitetea.
Wewe sema hivyo, haya maneno unanitamkia mimi, pia ulikuwa unamtamkia yunge mkubwa, si ulimsikia jana alivyokuwa anakusuta? Lakini ulinifurahisha ulivyonishika na ukaanza kupaa, yaani Raha.
 
Leo breki hapa
 
Mje huku Gily Antonnia Angel Nylon Amehlo Depal Kalpana Kelsea Lenie Darlin
 
Back
Top Bottom