True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

...102
Almanusura niangue kicheko baada ya kusikia mkwara ule alioutunga mzee maduhu na kuwaaminisha watu kapata ajali ya moto.
Aisee pole yake sana, nitarudi jioni kumwona, nilimwambia juma.
Basi poa dogo usiache kuja senta jioni ili tukutembeze uyajue vizuri mazingira ya hapa kijijini, alimaliza juma.
Sawa ntafika wala usijali, nilimjibu juma huku nikiona ananichelewesha kumuwahi yunge mdogo ambae kwa akili zangu za kipuuzi wakati ule nilijua bado atakuwa ananingojea, nilikimbia huku sasa nikimtafakari yule mze wa kiwanjani na uwongo wake wa kuungua na moto ilihali aligonga mwamba kunitia mikononi mwake na kumsababishia hayo maumivu.
Nilifika pale nyumbani nikamkabizi bibi chumvi yake, nilichukua haraka madumu yangu na kuanza kukimbia taratibu, nilipotoka tu upeo wa pale nyumbani mbio ziliongezeka mpaka pale makutano ya njia iendayo kwao yunge mdogo n. ile yakwetu, sikumwona pale hivyo nikajua moja kwa moja atakua bombani anachota maji, niliongeza speed, mbele kidogo nikaona wasichana wasiopungua wanne.
 
...103
Niliacha kukimbia, nilipowakaribia niligundua mmoja kati yao alikuwa yunge mdogo.
Nilipishana nao huku nikimtaka samahani yunge mdogo kwani nilikuwa na maongezi nae.
Bwana eeh! Mimi unanichelewesha, kwanza nimebeba ndoo ya maji ni nzito ujue, alinichimba mkwara yunge mdogo.
Basi sawa nisikuchoshe nenda mama, nilisusa huku nikianza kuondoka, wakati huo wale wasichana wengine wakiwa wamesimama kama hatua 10 mbele wakisikiliza huku wakimngoja mwenzao.
Kwahio umesusa, Loh! Mwanaume unasusa kweli? Alichamba binti mmoja kati ya wale watatu.
Sasa wewe nimekusubiri pale zaidi ya dakika 10 hutokei, mpaka wakanikuta hawa marafiki zangu ikabidi niongozane nao tu, alijitetea yunge mdogo.
Sawa baadae, nilimwambia kishingo upande.
Usijali nitakuja hapo nyumbani nikimaliza kupika nije tupige stori sawa mme? Alichombeza yunge mdogo huku akiniangalia kwa jicho flani hivi takatifu sana.
Nilitikisa bichwa kwa madeko kuonesha kwamba nilikuwa nimekubaliana na alichonambia hivyo niliondoka na kwenda kuchota maji.
 
...104
Nilifika nyumbani pale na kumkuta bibi keshaivisha, muda kidogo babu alifika pale, tulisalimiana kisha babu akenda kwoga kisha alirejea pale tunapo pendelea kukaa chini ya kivuli, utani wa hapa na pale uliendelea mpaka wakati bibi alipotenga chakula asubuhi ile, tulikula wali wenye radha nzuri sana kwani ulipikwa kwa mafuta ya ng'ombe {samli} pia maharage mazito yaliyotiliwa karanga, pia kulikuwa na chai iliyokuwa imezidi sukari na kuwa tamu ka asali.
Nmekuja kuoga na kubadili nguo, narudi kule msibani kwani mazishi bado hayajafanyika kutokana na mwili wa marehemu kuwa bado unatokwa damu mdomoni, puani na masikioni hivyo, hivyo baba mzazi wa marehemu ameomba nafasi afatilie kwanza kwa wataalam swala hili kwani linampa mashaka sana, kingine mama wa marehemu nae yu mgonjwa taabani kitandani hawezi hata kuinuka, inasemekana kuna jambo zito wanalificha, alieleza babu.
Hapa nilimkumbuka marehemu anaezungumziwa ni yule jamaa aliedondoka juzi mtini.
Niliwaza mengi mno niki nimejiinamia, nilipoinua macho...!
 
Back
Top Bottom