172
Kitendo cha wewe kukumbuka kuwa unasiraha ambazo zinaweza kukusaidia ni ushindi tosha na hizi zana ndo msaada pekee kwetu kuliko hata hata bibi yako na majirani uliokuwa unawaita na kuomba msaada kwao, alisema babu.
Inamaana kumbe alikuwa ananisikia wakati naenda kuomba msaada nyumbani kwa kina yunge mdogo? Niliwaza.
Sasa nenda nyuma ya nyumba ukaniletee ile zana niliyokuwa nimeibeba wakati ule nakufanyia tiba kisha uje hapa, hakikisha ukiibeba zana hiyo hutoiweka chini mpaka uje unipe mikononi mwangu, alitoa angalizo babu akiwa gizani na hatuonani kabisa.
Nilifika nyuma ya nyumba na bila kuhangaika kutafuta nilikifikia tu kile kitu kilichoonekana kama chungu kidogo sana huku kimezungushiwa matambala madogo meusi na mekundu makuukuu, nilishangaa licha ya giza zito lakini kilionekana vyema tu.
Nilikisogelea haraka huku nikiangaza macho huku na kule kuhakiki usalama wangu, nilikifikia na kuinama haraka, nilikitwaa na ghafla nilihisi mkono wangu wa kushoto kukakamaa na misuli kubana.
Nilitoka nduki...!