True story
Yule mtoto wa kichaga baada ya kunikataa niliendelea kupambania Kama siku mbili hivi, lkn yy anadai anajitahidi Sana kunipenda Ila anafeli na hajui kwanii anashindwa kunielewa, baada ya kuongea nae Sana akanieleza yeye Kuna mtu ashakuwa nae kwenye mahusiano, Ila kwa Sasa wameachana na jamaa ndo hamtaki lakini yeye anamsubiria pengine jamaa atarudi waendelee na mahusiano yao.
Nimejitahidi kumuelewesha kuwa huyo mtu anampotezea muda, hapo alipo ana miaka 27 kwa maana ya kwamba kachelewa Sana kwa mtoto wa kike asichaguwe Sana muda unamtupa mkono, lkn bado binti amekuwa mgumu kunielewa na kudai anampenda Sana jamaa...
Inauma Sana kweli, nikaamua kukaa kimya Leo ni siku ya tatu tangu nipige kimya, namuona online Wala hanitafuti hata haniwazi naandika sms kumsabahi lkn roho inaniambia kaza atakuona munyonge, basi naamuwa kukaza na kudelete nlichokuwa naandika.
Wanaa JF Kama Kuna namna naeza fanya niambieni Ushauri wenu.