Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
TRUE STORY: KUTOKA KWENYE KUONGEA KITHEMBE NA KUGUGUMA GUGUMA MPAKA KUWA MWALIMU MAHIRI WA KWAYA.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Kama kuna jambo unadhani huliwezi, nakuhakikishia unaliweza. Kama unadhani kuna jambo unalihitaji na umekata tamaa kulipata. Nakuhakikishia huja haja ya kukata tamaa. Unaweza kulipata. Sitaongea kama motivesheni spika kuwapa matumaini ya uongo kwa sababu sisi watibeli sio waongo. Nitakupa uzoefu wangu kupitia mimi mwenyewe.
Jina langu ni Robert hilo ndilo jina ofisho ambalo wengi hunitambua nalo ingawaje pia ninamajina mengine niliyopewa na wazazi na walezi wangu kuachana na yale majina niliyojipa mwenyewe au kupewa na watu wengine.
Kiasili Mimi sio mwongeaji kwani nilikuwa na kithembe na kuguguma guguma. Kama alivyokuwa Nabii Musa. Ingawaje kwa sasa ni muongeaji na wengi huniona mcheshi, mwenye maneno mengi na mizaha. Lakini kwa wanaonijua Fika watakuambia huyo sio Robert tunayemfahamu.
Nilikuwa na kithembe kikali sana. Na kama hujui kithembe ni nini, basi nikujuze tuu; Kithembe ni hali ya mtu kuongea sauti zisizo ulimi na meno anaziweka kwenye ulimi na meno. Mfano sauti za ulimi na meno ni "th na Dh" sasa mtu hutamka baadhi ya sauti za kaakaa gumu yaani sauti "S" na "Z" na kuzipeleka kwenye sauti za ulimi na meno kwa kutoa ulimi nje katikati ya meno
Yaani Sauti "S" anaitamka "Th"
Na sauti "Z" anaitamka. "dh"
Mfano akiongea atasema,
Thatha Thi uthogee mbele. Badala ya
Sasa si usogee mbele.
Hiyo ndio inaitwa kithembe.
Tatizo jingine lilikuwa kuguguma guguma. Hii wengi mnaijua. Yaani mtu anaongea kwa kustaki lakini hii haikuwa kwa kiwango kikubwa. Hasa nikiongea polepole bila haraka.
Hii ni kumaanisha nikiongea kwa wengine ilikuwa burudani kubwa sana. Wapo waliokuwa wakinicheka. Lakini ajabu ni kuwa sikuwahi kuona kama ni tatizo. Kuchekwa vile ninavyoongea na baadhi ya watu iliniongezea udadisi na kuwaelewa watu zaidi na ulimwengu ningali nikiwa mdogo.
Baadhi ya waalimu shule ya msingi nao mara chache walikuwa wakinitania na kunikejeli labda nikifanya kosa fulani. Hiyo pia haikuwahi kuwa tatizo kwangu. Unajua kwa nini?
Haikuwa tatizo kwa sababu sikuona ni kizuizi cha mimi kufika malengo yangu ya kusoma na kupata Elimu. Labda kama ingekuwa kizuizi huenda ingenipa shida na kuniathiri.
Pili, Nilikuwa moja ya vijana waliokuwa Smart darasani, kwenye mpira, na shughuli zote za vijana kwa wakati huo. Na niliwazidi wengi wakiwepo wale waliokuwa wananicheka au kunikejeli. So tuseme niliwadharau. Kumbuka pia sikuwa mwongeaji.
Tatu, Dini ilinipa ujasiri na uhodari. Na upeo wa ziada kwani nilikuwa nasoma vitabu mara kwa mara hasa nikiwa pekeangu nyumbani. Kumbuka nilikuwa introvert.
Nne, Mwonekano; Nilikuwa na mwonekano ambao ulikuwa haunipi mashaka. Sijisifii ila nilijiona na kuambiwa kubwa nina mwonekano wenye kuvutia kama kijana.
Nimetaja haya kwa makusudi ili kukupa ujasiri na kujiamini kuwa kwenye maisha yako yote, kamwe usisikilize yale unayokejeliwa nayo ambayo ni mapungufu yako kama wanavyoyaona na kuyatafsiri. Siku zote angalia yale ambayo Mungu amekubariki. Yale mambo ambayo umebarikiwa nayo ndio yakae kifuani mwako, yabebe, yalinde, yaonyesha, yatumie kama silaha kuendesha maisha yako.
Kila mtu anakitu alichobarikiwa. Yaani hata wewe hapo ulipo hata uweje jua kuna jambo umenizidi. Hata kama ni moja litumie hivyo hivyo. Hiyo ni mbinu mojawapo ya kupiga hatua.
Usijilaumu, usijilalamikie. Usijione haufai kwa kuangalia madhaifu yako.
Watibeli hatuna madhaifu kwa sababu hatuangalii madhaifu yetu. Always tunaangalia our strengths na kuzitumia.
Sio unafika sehemu hauna pesa au jambo fulani ambalo ni common, unajidogodesha na kujiona Duni. Nope! Tumia vile ulivyonavyo.
Basi bhana, usijesema TaikonMaster unamaneno mengi na nimetoka kwenye pointi.
Nikafika Kidato cha Tano.
Nikasema nataka uzoefu mpya. Tayari nina miaka 17 naelekea 18.
Sitakaa mara kwa mara pekeangu kama nilivyozoea. Nitajichanganya na watu. Nitakaa pekeangu muda wa kutafakari (kwani napenda sana kutafakari) au muda wa maombi(huo mara nyingi ni usiku). Wakati huo nipo Advance.
Ulimi wangu ni mzito. Nikasema, ili niulainishe itanipasa kubwa na ratiba ya kuimba. Nakumbuka zamani nikiwa mdogo Babu yangu wakati ananifundisha kingereza nyumbani alikuwa akiniambia ili nijue kingereza na ulimi uwe laini katika lugha ya kingereza, itanipasa niwe naomba mara kwa mara nyimbo za kingereza na kama ni kuongeza msamiati basi nisome vitabu vya kingereza na kusikiliza taarifa habari ya kingereza.
Sasa mbinu hiyo nikasema acha niitumie kusafisha na kulainisha ulimi ili niweze kuongea kwa kasi.
Nilitaka kujua watu wanapoongea kwa kasi inakuwaje, wanajisikiaje na kuwazaje.
Nilitaka nianze kujifunza ubishi kama vijana wengine.
Kwani mimi sikuwa na huo muda wa kubishana kumbuka mara nyingi ninafurahia kukaa mwenyewe na kuongea ongea au kusikia mtu anaongea ongea kwangu ilikuwa ni kero kubwa. Hasa akiwa anaongea vitu visivyokuwa na Maana.
Sasa nami nilitaka kujifunza kuongea vitu hovyohovyo. Blahblahblah! Lakini for Funny 🤣.
Basi nyakati za jioni ule muda wa maombi saa moja jioni baada ya Kula chakula cha jioni kule shule. Nikawa nawahi haraka darasa la ibada. Nachagua nyimbo nikiwa mwenyewe naimba wee kwa nguvu kweli. Ungedhani nipo kwenye ibada au ninamuimbia Mungu kumbe wala, mimi nilikuwa na agenda nyingine.
Wanafunzi wa kidato cha sita mwanzoni walipokuwa wakipita darasa nililokuwepo walishangazwa na tabia yangu hiyo ambayo eneo lile ilikuwa mgeni. Mimi sikujali. Hata hivyo nilijua hiyo itanipa feedback kama nitaihitaji.
Imba wee! Imba weee! Mpaka wanafunzi wengine watakapotoka Kula watanikuta, na tuendelee na ratiba za ibada.
Baada ya muda, nikashangaa wanafunzi wengine wasio wa dhehebu langu lakini wanapenda kuimba basi wakani-join tunaimba weee! Ikifika muda wa kusali wanaenda kwenye madhehebu yao.
Hivyohivyo.
Kumbuka mimi ni mwandishi by nature, so kila ambacho kilikuwa kinatokea nikikaa mwenyewe nakiandika huku nikikifanyia tathmini.
Nilijifunza, Kila jambo utakalolifanya ukiwa na uthabiti na consistency kuna watu watakuunga Mkono. Lazima upate wafuasi.
Pili, Jambo lolote jipya watu wengi hulipinga. Kwa sababu wanadamu wengi huathiriwa na mazoea.
Tatu, jambo lolote ukilifanya mara kwa mara unaanza kulimudu na kuliweza.
Basi bhana, nikaanza kuona mabadiliko katika kuimba kwangu. Kumbe kuna watu wananitazama bila ya mimi kujua. Na hilo limenifundisha mpaka leo. Kitu chochote unachokifanya usidhani watu hawakuoni. Wanakuona.
Kidato cha sita wanaondoka, nakabidhiwa chama cha ASSA na Mwenyekiti Joseph Msukuma. Kwenye Uenyekiti napigiwa kura nashinda. Wanachama wananichagua licha ya kuwa mimi nilikuwa ni mgeni nimehamia hapo mhula wa pili.
Nikiri, sikuwa nimejiandaa, pili sikuwahi kufikiri nitakuwa Mwenyekiti wa ASSA.
Tatu, Nilikuwa na Deni mmoja hivi Mkali huko O' Level. So niliona kwa kuwa mwenyekiti wa dini itanipa msalaba wa kutofanya mambo yangu ya gizani.
Ukizingatia Demu mwenyewe nimemchukua kwa kijana mwingine na ambaye alikuwa akipiganiwa na shule nzima mpaka walimu na huko mtaani. Lakini mnyama nikaibuka kidedea tena wakati huohuo ndio napewa Uenyekiti.
Sasa nikaona hapa hili nijaribu. Nikubali kubwa mwenyekiti ila niachane na huyu demu na mambo ya kiasherati. Au niukane uenyekiti ili niendelee kuwa huru na mitikasi yangu. Ili nisichafue nafasi ya uenyekiti na dhehebu letu.
Unajua kale kasichana kalikuwa kazuri Sana. Keupe peee, kanavaa hijabu kumaanisha kenyewe ni kaislam. Kanasoma kidato cha tatu nami ndio nipo kidato cha tano. Alafu kanagombewa, mimi nimekapata kutokana na ujanja ujanja wangu wa kimedani, hata bado sijakafyeka wananipa Uenyekiti. Aiseeh! Aiseeh! Nilikuwa kwenye mgogoro mkali sana.
Lakini sikusahau majukumu yangu. Ilinibidi nichague heshima ya uenyekiti kuliko Tamaa ya kukachapa kale katoto ambako tayari nilishakadiria utamu wake. Nilikaacha nikiwa na uchungu mkubwa. Sikukala!
Sasa nikawa mwenyekiti na majukumu ya uenyekiti wa dini yakaanza. Hapa life style inabadilika kidogo. Inabidi nijiweke kimwenyekiti. Ni kwamba kaunafiki kalikuwepo, yaani kuigiza kama mwenyekiti. Kuanzia kuongea, hutakiwa kujibishana vitu vya kijinga ambavyo tayari nilishajinoa na nilikuwa field ila nikakatishwa.
Joseph Msukuma(Mwenyekiti aliyeniachia kijiti) ananiachia jukumu jingine la kuwa Mwalimu wa Kwaya. Toba! Mimi! Mimi niwe Mwalimu wa kwaya. Unajua aliposema hivyo nilicheka sana. Kimoyomoyo nikasema hii imezidi sasa. Joseph Msukuma alikuwa mwenye busara nyingi sana. Akaniambia nitaweza na mpaka amenichagua tayari ameniona ninafaa. Nikamwambia hiyo kazi ni ngumu sana. Lakini akanisihi sana.
Kutokana na ile imani kuwa ninafanya kazi ya Mungu, na ninabariki watu nikaona kukataa haitakuwa jambo jema. Ni kama kupewa kazi ya Mungu na kuikimbia.
Nilikumbuka Mungu aliponitoa, Nilikumbuka mambo Mungu aliyonifanyia. Yote nilikumbuka. Sikusahau hata moja kwa sababu pia nilikuwa nayaandika. Leo nikatae! Leo napewa kazi tuu ya kuimbisha wengine nakataa! Mimi Robert Nakataa! Nilijikuta Nalia. Machozi yalinitoka. Nilikuwa pekeangu nikisutwa na nafsi yangu.
Labda utakuwa huelewi.! Labda haujatoka familia ya chini. Labda haujatoka maisha ya chini hata kama sio chini sana. Lakini Maisha ya kufukuzwa Ada. Maisha ya kukosa sabuni ya kufulia nguo za shule.
Maisha ya kusomea shule za kata, wanafunzi wengi waalimu hakuna, hujasoma tuition tangu ukiwa vidudu.
Mungu alikuwa pamoja na wewe na ulimwomba akufanikishe. Ukafanikiwa leo unapewa kazi ndogo tuu unakataa?
Unakataa nini Robert kama sio upumbavu? Unakataa nini Robert kama sio dharau na kutokuwa na shukrani?
Unakataa nini wewe?
Jambo gani Ulimwomba Mungu akakuzuilia ili leo ukatae?
Wewe ni msaliti..!!
Nilijikuta Nalia..! nalia...,! Kwa kutaka kujifunza tabia ngeni na mbaya. Usaliti!
Kisa tamaa za mwili, kisa warembo! Kweli Robert?
Basi nilipomaliza kuwaza na kulia, nikaamua nitakubali kuwa Mwalimu wa kwaya. Kama nilivyopewa na Joseph Msukuma. Kwani nilimwambia acha nikafikirie.
Kesho yangu kama kawaida Nilienda kuimba nikiwa nimefadhaika sana. Joseph alipokuja na kwa bahati alikuwa wa kwanza kufika. Nikamwambia nimekubali, nitakuwa Mwalimu wa Kwaya.
Robert kwa sasa ni Mwenyekiti wa ASSA, na Mwalimu wa Kwaya ya ASSA.
Joseph akatoa kauntabuku lenye nyimbo lukuki akanionyesha ambazo tulikuwa tunaimba. Na ambazo bado hatujajifunza alizozitunga yeye mwenyewe.
Akanikabidhi.
Nitaweza?
Mimi niliyekuwa na kithembe na kigugumizi leo ni mwalimu wa Kwaya! Haaa!
Joseph alikuwa amebakiza wiki chache wafanye mitihani yao ya kidato cha sita watuache. Hivyo alikuwa anatumia muda wake mwingi kujiandaa na mitihani huku akinisaidia kunifundisha kuimba na kuongoza Kwaya.
Hatimaye alihitimu na kuondoka. Nikabaki pekeangu.
Alipokuwepo nilikuwa na tumaini kwa sababu wakunisaidia alikuwepo. Iwe kwa utendaji au kwa ushauri. Leo nimebaki pekeangu.
Nilipata uzoefu wa kipekee sana. Kuachwa mwenyewe. Ni changamoto kubwa sana.
Mimi ndiye Mwenyekiti, mimi ndiye Mwalimu wa Kwaya! Wanachama wananitazama mimi kama kiongozi. Mimi ndiye niliyeshika maono ya chama kwa wakati huo.
Aiseeh! Sikuwahi kufikiria kuwa uongozi ni kitu kikubwa na kigumu kama wakati ule.
Chochote kikitokea utalaumiwa wewe!
Sikutaka chama kinifie Mikononi. Sikutaka Kwaya inifie Mikononi.
Kumbuka vyama vya kidini shuleni unatumia zaidi neno la Mungu kuteka mioyo ya watu alafu wao kwa hiyari yao ndio waamue kuabudu. Huwezi tumia mabavu.
Kuabudu na kuamini sio lazima.
Siku ya kwanza pekeangu,
Nipo mbele ya wanaASSA, Wananitazama kwa jicho la kunitathmini nitaweza, je waniamini. Nikajikaza, nikaongea na kutoa mwelekeo wa uongozi wangu, mambo ninayotarajia kuyafanya ikiwepo na mikakati na mbinu, na mambo ninayotarajia kutoka kwa members.
Kumbuka kuna wasichana wa O' Level ambao wapo kwenye foolishage. Joseph alinionya kuhusu kushughulika nao. Kwani wengu walikuwa na mitego na wakionyesha hisia zao za kingoni.
Na kama nitafanya kosa kutoka na mmoja wao ningejiwekea mazingira magumu kuongoza.
Mungu alinisaidia, nilifanikiwa. Sio tuu kwenye ASSA. Bali hata katika shule ile.
Siku moja isiyo na jina, Mwalimu wa michezo alikuja darasani kipindi hicho nipo kidato cha sita. Na kidato cha tano wamesharipoti.
Akaniambia, MWENGE unakuja wiki mbili zijazo, nataka uandae nyimbo na itafute wanafunzi uwafundishe nyimbo hizo zitakazoimbwa kwenye shughuli za Mwenge. Haaa! Nilimaka( kushangaa) kimoyomoyo. Mimi niliyekuwa na kithembe na kigugumizi leo ninaenda kutunga nyimbo, kufundisha na kuimbisha Kwaya ya shule itakayoimba kwenye Mwenge?
Nilikubali lakini nilifurahi. Pia hofu ilikuwepo. Hasa hofu ya itakuwaje?
Fikiria sasa ningekataa siku ile kuwa mwalimu wa Kwaya, Fikiria..! Je hii nafasi ningeipata? Kwa haraka haraka jibu ni hapana. Nisingeipata.
Kuchaguliwa kuwa Mwalimu wa kwaya ya wanafunzi katika shule ile katika tukio la mwenge lilinitia Moyo na kuniongezea ujasiri.
Lakini pia hiyo ilikuwa ni feedback nzuri kuwa kumbe inawezekana ninajua kuimba, na ninaimbisha vizuri, na mpaka waalimu wameona. Zaidi Jina langu linatambulika kwenye ofisi ya waalimu kwa jina la heshima.
Nikatunga nyimbo tatu.
Tayari nina ushawishi kwani tayari nilikuwa kidato cha sita, mwenye wadhifa ufuatao
Mwenyekiti wa ASSA
Mwalimu wa Kwaya ya ASSA
Kiranja wa nidhamu(huo nilisimulia)
Mwenyekiti wa Jiografia Club.
Na sasa Mwalimu wa kwaya ya shule katika nyimbo za kuupokea Mwenge.
Good move!
Wavulana kwa wasichana walifurika sana katika darasa langu. Hiyo ilimaanisha kubwa ninamvuto wa kipekee.
Kimoyomoyo nilimshukuru Mungu. Kwani programu zingine Waalimu walitumia viboko na nguvu kulazimisha wanafunzi waandae programu za mwenge. Lakini kwangu mambo yalienda kiwepesi na kwa namna rahisi sana kama nakunywa uji.
Nilikuwa na simu ya magendo ambayo nilikuwa naitumia kurekodi sauti kutafuta melody nzuri kwaajili ya nyimbo za Mwenye. Nikapata melody tatu. Kisha nikazitungia maneno na sauti.
Moja ya nyimbo bora zilizoacha alama bora na kumbukumbu isiyofutika ni ule wenye TiTle isemayo "TANZANIA"
Moja ya neti
*Tanzania aah Tanzania × 2"
Tanzania aah Tanzania × 2
Mwenge wetu huo umekuja...
Kuimarisha amani upendo,
Nuru yake inaunganisha,
Utaifa na uzalendo
Tuilinde jama Tanzania,
Tanzania, aah Tanzania.."
Hicho ni sehemu ya kipande.
Basi siku ya tukio ikafika.
Usiku wake nilijiandaa vyema kama Mwalimu wa Kwaya
Hofu kidogo ilikuwepo. Tayari niliambiwa kuna wageni wa kiserikali na viongozi walikuwepo.
Hapo ni kufua nguo, kuzionyoosha, na kuvifuta viatu. Nywele nilienda Kuzikata saluni. Unajua ukishakuwa kiongozi kuna mambo yanaenda kirahisi hivyo huna haja ya kuomba ruhusa ukitoka nje ya shule kwenda mjini.
Sasa nimejiandaa vya kutosha.
Siku ya tukio nimeita wana kwaya wangu. Kwaya ilisheheni vijana barubaru na wasichana warembo. Kwa hilo nilifanikiwa.
Baada ya kuona wako sawa.
Na kuwakagua kwamba wamevaa vizuri, safi kwa nidhamu. Kumbuka pia ni Kiranga wa nidhamu.
Hivyo majina yao walishajiandikisha kwenye kauntabuku nililowapa waandike na kusaini wenyewe. Na nilishawapa sheria kuwa kujiunga watajiunga kwa hiari lakini kutoka haitakuwa hiyari. Na akitokea mtu hayupo ningemshughulikia kinidhamu. Huku kidogo unatumia mamlaka ya kiuongozi kwani unaweza kumpa adhabu za kishule.
Lakini niliweka sheria ile mwanzoni wakaikubali ili kuepuka ule mwamko waliokuja nao siku ya kwanza ukiisha katikati wasije kuniacha Solemba.
Ilikuwa kwaya kubwa ya wanafunzi kama hamsini hivi. Tulikuwa wengi.
Tukapiga mzigo darasani kama final touch wanafunzi wengine wakituchungulia madirishani ungedhani sisi ni wageni hawatujui.
Mbele ya jukwaa tunaingia kwa ngoma. Umati mzima umetulia tuliiii. Viongozi wa serikali, wageni waalikwa, wakimbiza mwenge wakiwa na Sare zao huku Mwenye ukiwa Unawaka, baraza la shule na waalimu, Wazazi na Wanakijiji, wanafunzi wa A'Level na O'Level wote walikaa kimya kututazama tukiingia kwa manjonjo.
Mimi nikiwa kiongozi Wao. Nikiwa nimevaa tofauti kidogo na wao. Si unajua mambo ya sanaa.
Hofu ilikuwepo lakini kadiri nilipokuwa nalikaribia jukwaa ilizidi kupungua.
Tulifika Jukwaani. Kisha kukawa kimya.
Hatimaye zoezi linaenda kuanza.
Nikachukua Maiki, nikasalimia, nikakaribisha wote, kisha nikajitambulisha mwisho nikaitambulisha kwaya yangu.
Watu wakapiga makofi nafikiri walitarajia jambo kubwa. Na huu ilinifanya nishukuru kwa jinsi nilivyokuwa nimejiandaa na kuiandaa ile kwaya.
Tukaanza kuimba, tuliimba! Tuliomba sana.
Mungu awabariki wale vijana huko waliko.
Wakati wanaimba mimi nikiwa kiongozi wao. Mawazo yangu yakanichukua yakinurudisha nyuma kabisa kipindi nikiwa kijijini kwetu.
Nikiwa naongea kithembe na kigugumizi.
Yote nilikumbuka.
Unajua waliimba mpaka hisia zangu zikavunja mhimili. Nilishindwa kujizuia. Nilikuwa natoa machozi huku nikiimba. Haikuishia kwenye machozi kwikwi ilianza kunisonga sasa nikawa nashindwa kuimba vizuri.
Viongozi wa serikali waliokuja walisimama wakipiga makofi, waalimu na wageni na wanafunzi walishangilia. Mimi pekee huenda ndiye niliyekuwa nalia kwa furaha iliyopitiliza.
Baadaye tulimaliza kwa ushindi.
Historia hiyo haitafutika katika maisha yangu. Ilikuwa mwanzo mpya wa badiliko la ndani ambalo nilisema sitabadilika pekeeangu. Nitabadilisha na wengine kwa gharama ileile ambayo nilibadilishwa. Nayo ni Bure!
Hivi leo wapo wengi wamebadilika kwa namna nyingi kutoka kuwa dhaifu kubwa bora kutokana na mimi. Hiyo kwangu ni baraka.
Hata wewe unaweza kubadilika. Yale unayoyaona kwako ni udhaifu usiruhusu yawe kikwazo kwako.
Angalia uliyobarikiwa yatumie kukupa uhodari na ujasiri.
Na yale madhaifu kama kile kithembe changu na kigugumizi yatumie kuyageuza maisha yako yawe ushuhuda.
Nikiwa namaliza, na kukumbusha kubwa safari ya badiliko inahitaji Muda, nia, ujasiri, na subira huku Mungu akikuongoza.
Nakumbuka wakati nawaambia wazazi wangu na ndugu zangu ati nimekuwa mwalimu Kwaya walicheka sana. Waliona kama mzaha, waliona walionichagua hawako Serious. Sikuwalaumu kwani hakuwajua Mungu huweza kukubadilisha na kuwa mtu mwingine bora zaidi yule ambaye hawakutarajia.
Mwisho uliongea.
Hivyo watu wako wa karibu, rafiki, wazazi na ndugu wasijewakakukatisha tamaa. Unaweza sio kwamba nakupa Moyo bali nina uhakika na kile ninachokisema.
Stori kati ya kichale kidogo katika stori za maisha yangu
Kufikia hapa sina la ziada.
Wote mbarikiwe.
Robert Heriel
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam