Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza agizo rasmi la kuongeza ushuru wa ziada wa asilimia 25 kwa bidhaa zinazoingia Marekani kutoka India, kutokana na India kuendelea kununua mafuta kutoka Urusi.
Hatua hiyo itafanya jumla ya ushuru kwa bidhaa za India kufikia asilimia 50 – moja ya viwango vya juu kabisa kuwahi kutozwa na Marekani dhidi ya nchi yoyote.
Kwa mujibu wa agizo hilo la urais, ushuru mpya utaanza kutumika ndani ya siku 21, yaani kuanzia tarehe 27 Agosti.
Wizara ya Mambo ya Nje ya India ilijibu kwa tamko fupi Jumatano, ikisisitiza kuwa tayari imeeleza msimamo wake kuhusu uagizaji wa mafuta kutoka Urusi. Tamko hilo lilisema ushuru huo mpya ni "usiokuwa wa haki, usio na msingi, na wa upendeleo."
"Ni jambo la kusikitisha sana kwamba Marekani imechagua kuiwekea India ushuru wa ziada kwa hatua ambayo pia inafanywa na mataifa mengine kwa maslahi yao ya kitaifa," ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.
India pia iliongeza kuwa itachukua hatua zote muhimu kulinda maslahi yake ya kitaifa.
Awali, Trump alikuwa tayari ameonya kuwa angeongeza ushuru huo, akidai kuwa India haijali watu wangapi wanauawa nchini Ukraine kutokana na "Mashine ya Vita ya Urusi".
Trump orders India tariff hike to 50% for buying Russian oil US President Donald Trump has issued an executive order hitting India with an additional 25% tariff over its purchases of Russian oil. That will raise the total tariff on Indian imports to the United States to 50% - among the highest rates imposed by the US. The new rate will come into effect in 21 days, so on 27 August, according to the executive order.
A response from India's foreign ministry on Wednesday said Delhi had already made clear its stance on imports from Russia, and reiterated that the tariff is "unfair, unjustified and unreasonable". It is therefore extremely unfortunate that the US should choose to impose additional tariffs on India for actions that several other countries are also taking in their own national interest," the brief statement read." India will take all actions necessary to protect its national interests," it added. The US president had earlier warned he would raise levies, saying India doesn't "care how many people in Ukraine are being killed by the Russian War Machine".
SOURCE: BBC

==============For English Audience====================