Trump aanza kwa kutaka kunyakua Greenland na mfereji bahari wa Panama

Trump aanza kwa kutaka kunyakua Greenland na mfereji bahari wa Panama

Vita ni uchumi pia, kama nchi ina uchumi mdogo hata misuli ya kijeshi nayo inakuwa midogo.
Uchumi,silaha,hali ya kisiasa,washirika,uimara wa mapigano

Option yoyote itakayo husu vita ambayo uta mobilise watu ili kupigana haina nguvu tena Tanzania.

Kwa hiyo chaguzi lolote la vita ni baya kwa CCM hawapo upande wowote wa kushinda vita bali upande hasi wa kuathirika na matokeo ya vita hii ilikuwa hata Uganda tuliyopigana nayo tulipata weak enemy aliyekuwa na hali mbaya ya kisiasa nchi mwake licha ya support ya washirika walio mpatia lakini haikumsaidia chochote.

Hata waganda wenyewe walishirikiana na adui kumtandika Amin pasipo kujali madai yake yalikuwa sahihi ama laaah.
 
Tanzania ziwa Nyasa tu kapigwa beat, mpaka ufukweni.
Wamalawi waungawana, sio aggressive halafu wepesi sana, sioni hata haja ya kuwakazia sana. Itakuwa wanapelekwa kwa kubembelezwa.
 
Uchumi,silaha,hali ya kisiasa,washirika,uimara wa mapigano

Option yoyote itakayo husu vita ambayo uta mobilise watu ili kupigana haina nguvu tena Tanzania.

Kwa hiyo chaguzi lolote la vita ni baya kwa CCM hawapo upande wowote wa kushinda vita bali upande hasi wa kuathirika na matokeo ya vita hii ilikuwa hata Uganda tuliyopigana nayo tulipata weak enemy aliyekuwa na hali mbaya ya kisiasa nchi mwake licha ya support ya washirika walio mpatia lakini haikumsaidia chochote.

Hata waganda wenyewe walishirikiana na adui kumtandika Amin pasipo kujali madai yake yalikuwa sahihi ama laaah.
Hakuna kitu huwa kinawaunganisha raia pamoja kama adui kutoka nje, halafu mgawanyiko wa siasa za Tanzania ni kivyama, aina hii ya mgawinyiko hana impact sana kwenye vita kwa sababu unakuta baba yuko CHADEMA na mama yuko CCM. Mgawawanyiko mbaya katika vita unaoweza kumpa adui wa nje fursa kubwa ni wa dini, ukabila au ukanda.
 
Rais mpya wa Marekani Donald Trump ameanza kipindi chake cha pili kwa mpango wa kutaka kunyakua Greenland ambalo ni eneo la nchi ya Denmark na mfereji wa Panama ambao ni eneo la nchi ya Panama.

Aliwahi kugusia jambo la US kuinunua Greenland katika kipindi chake cha kwanza cha uongozi watu wakafirkiri alikuwa anafanya utani tu au ni mjinga asiyejua anachokisema ila ameyarejea madai yake na akawajibu waandiashi wa habari yuko serious sana na pia hawezi kuwahakikishia hatatumia hata nguvu za kijeshi kuyachukua.

Anadai hayo ni maeneo muhimu kwa usalama na uchumi wa Marekani, amelalamika Wachina kujazana Panama.
Hili swala ninaendelea kulisoma ili kulielewa kwa undani wake na kupata mantiki.

Alitania kuhusu Canada kujiunga na US na kuwa jimbo la 51 la US, lakini naona na lenyewe sasa hivi limeshakuwa mjadala mkubwa watu wakiwa serious kwamba amepania kufanya hivyo.
Hili la Panama.

Kuhusu mfereji wa Panama, US ndiyo iliuchimba sababu za kiuchumi na kijeshi.

Kuhusu Greenland, Trump siyo wa kwanza, lilianzia kwa President Harry Truman mwaka 1946, ingawa Denmark iliiataa il ofa ya US$ 100. Trump alikuwa ni wa pili kuja na idea hiyo na sasa ni mara ya pili. Anapoongelea hilo mbali ya uhitaji wa US, pia tayari ndani ya Greenland kuna hilo vuguvugu.

Kwa sasa sina maoni, nahitaji muda zaidi kujifunza kuhusu haya ya Panama canal na Greenland.
 
Hakuna kitu huwa kinawaunganisha raia pamoja kama adui kutoka nje, halafu mgawanyiko wa siasa za Tanzania ni kivyama, aina hii ya mgawinyiko hana impact sana kwenye vita kwa sababu unakuta baba yuko CHADEMA na mama yuko CCM. Mgawawanyiko mbaya katika vita unaoweza kumpa adui fursa kubwa ni wa dini, ukabila au ukanda.
Haah

Tanzania tuliivamia Uganda hatukuwa adui kutoka nje ?

Huo muunganiko ulikuwa wapi huko Uganda ?

Nikupe mfano wa Asad asilimia kubwa ya waasi waliomuondosha Asad wala hawakuwa Wasyria huo muunganiko wa wasyria ulikuwa wapi wakati Asad anaondoshwa kipuuzi ?

Siasa za nchini na hali yake unafuatilia kweli ? Hali ya kisiasa ya hii miaka hapa nchi umeizingatia ?

Muunganiko gani utapatikana nchini huku asilimia kubwa ya wananchi wanamtambua adui yao kuwa CCM halafu huyo ndie awaunganishe wananchi kwa namna gani na kwa maslahi yapi ?

Unaungana vipi kumtetea na kumlinda adui yako CCM wakati vita ndio option ya wewe kuweza kumuangusha huyo adui yako

Nchi hii ni ya wachache ambao ni CCM kila mwananchi mwenye akili timamu nchi hii anatambua hili

Hao vijana wenyewe wa JKT huwezi kuwa mobilise labda kama haufahamu uozo unao endelea TPDF
 
Haya Mambo ukiwa na nguvu ni raha tupu .

Ndiyo maana Mimi nilijaribu nguvu zangu na kuogopeka kwangu mtaani wakati wa kujenga fensi nikazidisha miguu Kama mitatu makusudi ili nione jirani ananimudu au ataufyta 😀😀

Ila kilichonikuta sitaki kusema hapa Ila jua Kuna watu Wana roho mbaya Sana hapa Tanzania
 
Acha kuishi ufahari wa kale hakuna vita hapo Tanzania atashinda
Ni mtazamo wangu kaka; simuoni wa kuishinda Tanzania hapo; BTW hakuna ambaye hajawahi kuonja kichapo chetu, Burundi iliwahi kuomba poo miaka ya 1997/98, Rwanda JK alifanya yake vizuri tu na PK alipiga magoti kwake, Comoro hadi rais aliepo pale tulimuweka sisi
 
Kuna maelfu ya vijana wamepita JKT kwa mujibu wa sheria au kujitolea, hilo ni jeshi la akiba.
Vile vyuma chakavu vinavyo pitaga kwenye maonesho uwanja wa uhuru ndo vinakudanganya?
 
Hivi Tanzania hatuwezi kuzinyakua Rwanda na Burundi tukazirudisha?

Basi tukishindwa hata Comoro au Shelisheli tu
hao wakomoro na washelisheli ni waswahili tu, wanapenda kuwa sehemu ya tanzania. Kwa rwanda na burundi inajulikana ilikuwa koloni moja la mjerumani la germany east africa
 
Kwa hiyo denmark itakubali kuachia eneo hilo bila kupigana? Hii kali marekani kupigana vita na wazungu wenzao wa ulaya tena mwanachama mwenzake wa NATO
 
hao wakomoro na washelisheli ni waswahili tu, wanapenda kuwa sehemu ya tanzania. Kwa rwanda na burundi inajulikana ilikuwa koloni moja la mjerumani la germany east africa
Jaribu kwingine ila siyo Comoro, ushelisheli ni matajiri na wanajielewa huwezi kuwanyakuwa kifala.
 
Jaribu kwingine ila siyo Comoro, ushelisheli ni matajiri na wanajielewa huwezi kuwanyakuwa kifala.
mbona yule mpinzani wa abdallah sambi alipotwaa madaraka kinyemela alipata kifinyo laini toka jwtz chini ya mwamvuli wa jeshi la kimataifa la sadc?
 
Sio tu Panama na Greenland huyu Mzaramo wa U.S anataka na Canada.

Mashabiki zake walikuwa wana msifia kuwa sio mtu wa vita na chokochoko ila hii speed aliyo anza nayo atawavua nguo.

Na sababu nyingine anasema lengo la kutaka maeneo hayo ni kumdhibiti China
duh! Ataanzaje kuichukua canada iwe sehemu yake? Akifanikiwa marekani itakuwa na majimbo ya quebeck yanayoongea kifaransa. Kuna yale yanayoongea kihispania kama texas, hata ya kireno yatatakuwepo
 
mbona yule mpinzani wa abdallah sambi alipotwaa madaraka kinyemela alipata kifinyo laini toka jwtz chini ya mwamvuli wa jeshi la kimataifa la sadc?
Umeelewa lakini? Yule alikuwa amejisimika unahisi ufaransa atakubali Tanzania mchukue makoloni Yale?
 
Back
Top Bottom