Trump amteua mkwe wake mwingine kama mshauri kwenye utawala wake mpya!

Trump amteua mkwe wake mwingine kama mshauri kwenye utawala wake mpya!

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu.

Hata baada ya kusema kuwa this time around hatohusisha wanae kwenye uongozi wake, Trump inaonekana ameendelea kuteua watu wake wa karibu.

Hivi karibuni Donald Trump amemteua Massad Boulos, baba mkwe wa binti yake Tiffany, kuwa mshauri wa masuala ya Waarabu na Mashariki ya Kati.

Mfanyabiashara huyo mwenye asili ya Kilebanoni na Kimarekani ni mkwe wa pili wa Trump kuteuliwa kushika wadhifa katika utawala wake unaokuja, baada ya kumchagua Charles Kushner, baba mkwe wa binti yake Ivanka, kuwa balozi wa Ufaransa.

Ikumbukwe kuwa Bwana Boulos alihusika katika kampeni ya Trump kwa jukumu lisilo rasmi, akimsaidia Trump kushawishi wapiga kura wa Kiarabu na Waislamu waliokuwa wakilalamikia utawala wa Biden kutokana na vita vya Israel na Gaza.

Akitangaza uteuzi huo kupitia mitandao ya kijamii, Trump alisema Bwana Boulos alikuwa “na mchango mkubwa katika kujenga ushirikiano mpya wa kipekee na jamii ya Wamarekani wenye asili ya Kiarabu.”

Trump aliongeza kwenye Truth Social kuwa Bwana Boulos alikuwa “mtetezi wa muda mrefu wa maadili ya Republican na Conservative” na ni “rasilimali muhimu” kwa kampeni yake.

Wakati wa kampeni, Bwana Boulos aliwashawishi wapiga kura wa Kiarabu na Waislamu kwa kuwaahidi kwamba Trump atarejesha amani katika Mashariki ya Kati.


Trump.png

Mossad Boulos ni nani?

Mossad alizaliwa nchini Lebanon na anajulikana na ni mtu maarufu baina vikundi kadhaa vya kisiasa nchini humo.

Aliliambia shirika la habari la Associated Press mwezi Juni kwamba yeye ni “rafiki” wa Sleiman Frangieh, mwanasiasa wa Kikristo wa Kilebanoni aliye mshirika wa chama cha Kisiasa cha Kishia na kikundi cha wanamgambo cha Hezbollah.

Baada ya kumaliza masomo yake, Boulos alirudi kwenye biashara ya familia na kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa SCOA Nigeria, kampuni kubwa yenye thamani ya mabilioni inayosambaza magari na vifaa katika Afrika Magharibi.

Wakati wa uchaguzi wa rais wa Marekani mwaka 2024, Boulos alifanya kampeni kwa ajili ya Trump katika jamii za Waislamu na Waarabu, akishirikiana na Bishara Bahbah, mwanzilishi wa Arabs for Trump, na Richard Grenell.

Bahbah alisema kuwa Boulos alijaribu kumwonyesha Trump kama kiongozi anayesaidia "amani ya dunia."
Mwaka 2022, mwanawe Michael alimuoa Tiffany Trump, binti wa Donald Trump. Pia ana mtoto mwingine aitwaye Fares, ambaye ni mwigizaji aliyecheza katika The Crown.

Boulos ana uraia wa Lebanon, Nigeria, Ufaransa, na Marekani. Ameoa Sarah Boulos, mfanyabiashara na mwanzilishi wa Society of the Performing Arts in Nigeria na mmiliki wa franchise ya Cred International Lagos Island. Wawili hao wana watoto wanne.

=====================================================================
Donald Trump has named his daughter Tiffany's father-in-law, Massad Boulos, as an adviser on Arab and Middle Eastern affairs.

The Lebanese American businessman is the second in-law to be offered a position in the incoming administration, after Trump picked Charles Kushner, his daughter Ivanka’s father-in-law, to serve as ambassador to France.

Mr Boulos played a key unofficial role in the Trump campaign, helping him court Arab American and Muslim voters as many of them grew frustrated with the Biden administration over the Israel-Gaza war.

Announcing the appointment on social media, Trump said Mr Boulos was “instrumental in building tremendous new coalitions with the Arab American community".

“He has been a longtime proponent of Republican and Conservative values,” Trump said on Truth Social, adding that Mr Boulos was an “asset” to his campaign.

On the campaign trail, Mr Boulos appealed to Arab American and Muslim voters by promising them that Trump would restore peace in the Middle East.

His efforts exploited a big vulnerability for the Harris campaign, who struggled to win support from Arab and Muslim Americans due to US support of Israel during the ongoing Israel-Gaza war.

“Those massacres would not have happened if there was a strong president at the White House,” Mr Boulos told Trump supporters in Arizona earlier this year, referring to the mounting civilian deaths in Gaza. “The entire war wouldn’t have happened.”

It is unclear how Mr Boulos intends to leverage his advisory role. Born in Lebanon, he is known to have forged ties with several political factions in his birth country.

He told the Associated Press in June that he is a “friend” of Sleiman Frangieh, a Christian Lebanese politician who is allied with the Shia Muslim political party and militant group Hezbollah.

Mr Boulos has already served as something of an informal liaison between Trump and Middle Eastern leaders, the New York Times reported.

He is also reported to have met Mahmoud Abbas, the leader of the Palestinian Authority, on the sidelines of the United Nations General Assembly in September.

At that meeting, Mr Boulos reportedly conveyed Trump’s desire to end the Israel-Gaza war and other conflicts around the world.

Source: BBC
 
Utawala wa Trump ni kihoja kitupu kwa America
 
Kheeeh had [emoji631] nako kuna kupeana madaraka kwa wayemba.
Makubwaaa!! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom