ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Bilionea Elon Musk ameonyesha kuunga mkono wazo la Marekani kujiondoa katika Umoja wa Mataifa (UN) na Muungano wa Kijeshi wa NATO.
Akijibu chapisho la mtandaoni jana Jumapili lililohimiza hatua hiyo, Musk, ambaye anaongoza Idara ya Ufanisi wa Serikali ya Marekani (DOGE), aliandika kwa ufupi: "Ninakubaliana."
Rais wa Marekani, Donald Trump, na wabunge wa chama cha Republican wameahidi kutathmini upya ushiriki wa Washington katika UN na NATO.
Mnamo Februari, Seneta Mike Lee wa Utah aliwasilisha mswada wa DEFUND Act, unaopendekeza Marekani ijiondoe kabisa kutoka UN. Lee alikosoa Umoja wa Mataifa kama “jukwaa la madikteta” linalopinga Marekani na washirika wake, akisema licha ya ufadhili mkubwa, UN imeshindwa kuzuia vita, mauaji ya kimbari, ukiukwaji wa haki za binadamu, na majanga ya kiafya.
Nipashe
====
My Take
Sawa tuu ajitoe kwani lazima awepo? Dunia inakoelekea ni kutamu. Na chawa wake bwana Musk yeye Huwa ni kusema ndio Mzee tu.