Trump apewe nuclear codes

Trump apewe nuclear codes

Kwanza mimi sina wivu na The bold namkubali

Lakin leo sija muunga mkono, kwani hizi info zipo hata wikipeidia na kwenye websites za congress au za ikula ya Marekani, na dogo alicho kosea ni kuto sema tu labda imetoka kwa the bold, ila otherwise hizo information ni za public, na acknowldge katumia muda wake kuziunganisha na kutafsiri but, kwa kuwa haja i publish popote, na hata yeye haja acknowldge source zake ni zipi, ni jambo la kawaida tu. Ingekuwa ni hadithi mnyama umejiumiza kuitunga hapo ningesema uko sahihi, au ungekuwa uli take time ukaenda US ukafanya uchunguzi hapo ningesema pia its a big deal.

Mbona watu wanatumaga makala za washington post humu au NY times Na hawasemi, hii jf ni public realm kama kuna knowldge wacheni watu tushare, labda tu anaye share aseme kaitoa kwako.

Halafu kwa the bold na mashabiki wake na wapenzi wake, the bold naye anaweza kukosolewa tu. Na si kila anaye mkosoa ni hater. Kubalini kushangiliwa na kuzomewa pia ndio life.

Naruhusu masahihisho.
Mkuu ukitaka kuelewa kwa nini analalamika, nenda katafute source aliyoipata hiyo habari, isome na uilewe afu itafsiri kwa lugha nzuri ya kiswahili, kisha ipost humu afu unitag. Ukiona hayo yote au mojawapo huwezi kulifanya basi jua hiyo ndo sababu inayomfanya The bold alalamike.
 
Mkuu, the thing is mimi na wewe tunajua kuhusu mfano ishu 'A'. Wewe ukaifanyia kazi mfano deeper research, ukaitranslate na ukaipangilia na kuipost katika group lako la whatsapp or wherever.

Mimi hapa Karucee nichukue makala yako 'A' niikopi na kuipesti tena word by word humu ama sehemu ingine ile kama vile ya kwangu. Na inajulikana kabisa ile makala ni ya kwako. Nitakua nimekutendea haki?


Kama na mimi najua chochote ningechangia makala yako kwa kuiongezea nyama, kuikosoa ama kui challenge. Am telling you ingekuwa tamu. Heated debates but intellectual ones.

I hope umeelewa. Samahani kwa kuboreka na ushinde salama.
Hiyo kazi anayoclaim anayo patent, copyright? Isije kuwa kama ile kujiita simba?

Nahitaji The bold atuoneshe registration ya hiyo kazi yake kabla sijaanza kumsaidia kutoa povu pamoja naye.

Maana povu analotoa sio la nchi hii
 
Sipendi kuona MTU akitetea haki yake.alafu kuna watu wanampinga.jamaa alikuwa sahihi kulalamika.kama mleta mada angeileta hii mada kwa kiingereza jamaa asingelalamika.ila jamaa amekopi kitu cha mwenzie.alaf amekaa kimya sio fair.
Hata hao wanaomlalamikia The bold kwa kulalamika kwake, wangetuletea basi hiyo ya ki english ili waonekane hata wana point robo, lakini wamekalia kulalamika tu bila sababu za msingi.
 
Kila information tunazo pata duniani someone somewhere alijitutumua ndio na sie tuka pata.

Yaan namkubali sana bold kuwa huwa ana anaandika ila sasa info kama za leo kosa ni kuwa jamaa hajasema tu kuwa katoa kwa bold.

Pia ni mpaka ujue kuwa jamaa naye hii makala kaipata wapi, uskute hata hayuko kwenye hilo group, uskute alifowardiwa naye.

Sijapinga kazi yake ila napinga hii kitu imefanywa big deal wakati si big deal hata. Ni taarifa tu hizi tunashare.
Ukitaka kujua kama ni big deal au sio big deal, siku ukiwa chuo hasa chuo kikuu either degree au master, copy reseach ya mtu bila kucredit uliyemcopy, hapo ndo utajua kama ku copy ni big deal au small deal. Tena atakayekutoa machozi sio aliyeandika hicho ulichocopy bali aliyegundua kuwa umecopy somewhere tena kwa mtu ambaye hata yeye hajawahi kumuona.
 
Sina chuki yoyote usilete mapenzi kwenye maswala ya msingi ,
Mimi silali naye kitandani huyo kwamba kila anachosema lazima nikubaliane naye
Ya kwamba kwa kuwa niffah k yake inakuwa operated daily na mkuu The Bold basi kila kisemwacho ni ndioooooooooooo kama wale wabunge wa wanaopata command kutoka Lumumba
 
Walio anzisha JamiiForums ni positive great thinkers,

Maana walikuwa na ndoto ya kuwaunganisha watu wote bila kujali utofauti wao kwa lengo la kujifunza na kushea habari.......Hawatofautiani sana na wale African Elites.
Si lazima tukubaliane wote kwenye mada zote zitakazoletwa hapa, lakini kikubwa ni kwamba kupitia JF watu wote wanaopingana ama kukubaliana jambo wameunganishwa.

Sasa leo mtu anakuja kuleta mgawanyo wa wajumbe kwa vitu vidogo kama vile vistori vya kutafsiri kutoka google.....Eti kuna kakikundi ka wajumbe ndo watakaohusika tu.

Kuna watu kama wangekuwa wamiliki/waanzilishi wa JF, kungekuwa na kiingilio na ada za kila mwezi kwa members wote. Uzuri ni kwamba akili siyo makalio kila mtu awe nazo, zinaangukia penye utu.
Hebu kuwa open minded halafu uone kama hii mada ina nguvu ya kumtoa mtu povu kama siyo gubu na kuwa akili za kiubinafsi?
Mkuu Kama uko Bar ita waitress akupe kinywaji ntapita kulipa, jamaa ni mbanafsi too much utadhani hizi makala hajazitoa Internet na kuzitafisiri tu
 
Haya, ni hivi:

Mgelezeaji anamlaumu mwenzake/ mwingine kwa kumgelezea.

Ni wakati muafaka sasa somo la ugelezeaji kuanza kufundishwa mashuleni na lifundishwe kuanzia ngazi ya elimu ya upili hadi vyuoni.

Na liwe ni somo kamili kabisa ambalo mtu anapaswa kulifaulu.

Mtu unaponakili mawazo au maandiko ya wengine ni lazima useme umeyatoa wapi, hata kama utayaweka katika lugha tofauti.

Usiposema umeyatoa wapi utakuwa umetenda kosa.

Sasa haya mambo kuhusu siri za Marekani, silaha zake, na kadhalika ni mambo ambayo yapo kwenye public domain.

Kuna mi documentaries kibao tu. Sisi wanazi wa Discovery Channel tunayajua hayo.

Hata huko kwenye ma encyclopedia hayo mambo yapo.

Kwenye Library of Congress huko ndo usiseme kabisa.

Hivyo ni vyema mtu kuweka vyanzo vya ulikopatia taarifa unazoziweka.
Kwa hiyo hata the bold anakopy sehemu na kututafsiria sisi wavivu si ndio [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] maana wengine hata hatuyajuiii
 
Alafu huyu jamaa yuko fair sana humu ndani mpaka AME maindi ujue ime mtach.yeye ni sawa na mwalimu mmoja anayefundisha darasani na tuition. Haiwezekani wanayopata tuition na wanayoyapata darasani yawe sawa.kama unataka nenda tuition.ila naamini jamaa haishi kwa kutegemea hela za tuition.ila anachotaka haki miliki.
Kuna vitu navichunguza kubaini uhusiano wako na The Bold, kuna fact naikosa ili kuhitimisha kuwa wewe ndio yeye
 
The Bold,bora ungekaa kimya kuliko ulichokifanya,usipende kulaumu tu sometimes uwe unashukuru pia,mimi nimtu ambae waga nakuona upo smart sana,bt kwa majibu yako ya leo nimekushusha vyeo,unaonekana kama kasichana ka kiswahili,ukikaita tu kanatoa matusi bila kujua ulitaka kusema nn.
Na tumejua rangi halisi ya mkuu the bold, kitabia cha Leo alichokionesha ni Sawa kabisa na ulivyosema
 
Jibu rahisi tu mimi ndie niliependekeza hilo group liundwe ili angalau arosto ya kusoma ipungue coz kule anatoa 4episode kwa wiki, wakati huo hapa ile itaendelea kama ilivokuwa mwanzo tofauti ipo kidogo tu nyie mkiwa na ep 10 , sisi tuna 30 lakini mtatufikia Tu.
hata makanisani kuna VIPs wao wanapata huduma popote mchungaji anamfata wakati huo waumini wengine mnaendelea kumsubiri,
ukiandaa kitu kikaungwa na wengi matunda yake ndo haya wakuu jaribuni na nyie kucreate vitu kama hivi neema itawadondokea,
Haina haja ya mabeef kama watoto wa kike, hata mwalimu anapofundisha darasani huwa anatumia vitabu vilevile kama wengine wanavotumia lakini akifaulisha sifa zinamwendea yy peke yake badala ya waandishi wa hivo vitabu, kutransilate lugha hasa ya kiintelejensia au kidaktari ni shuhuli mkuu tusidanganyane,,,
NB:
nimecheka jamaa alivoanza eti nimetumia siku nzima kufatilia kiapo cha trump,
Hv wikipedia pia walianzia hapo???

Mkuu wewe inaezekana ulikuwa na nia njema tu ya kumchangia The bold ili anapoandaa makala zake awe anapoza hata kwa sharubati lakini kitendo cha kuanzisha group na wengine kulipia ili wapate makala mie naona kinanyima fursa ya wale wasio na fedha/shekeli kupata hizo makala.

Na huu ndiyo ugomvi unaoonekana humu, wengine wanabeza kwamba wanazijua hizi makala lakini kwanini nao hawaziweki humu ili watu wazisome pia? Lakini hawa wanaona tu kuwa wamekosa hiyo fursa ya kuendelea kusoma makala ambazo sasa zinalipiwa huko kwa group.

Mie sio muumini wa fedha lakini ni MUUMINI WA UTU NA HAKI na nafahamu kuwa fedha sio kila kitu katika maisha ya binadamu.

Ushauri wako wa kuchangia fedha umeleta tafrani humu sasa kwani kama shida ya The bold ni pesa mie nipo tayari kumchangia ili aendelee kutuletea makala humu.
Kupitia makala zake tunajifunza na tunaburudika.
 
Kwa hiyo hata the bold anakopy sehemu na kututafsiria sisi wavivu si ndio [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] maana wengine hata hatuyajuiii

Oh yeah...hayo mambo yapo kwenye public domain [kiasi fulani tu ambacho wanaweza kuachia/ kuweka hadharani].

Ona kwa mfano hii documentary ya History Channel....



Cheki hiki kipande cha PBS News Hour...



MSNBC majuzi tu hapa wameliongelea hilo la nuclear codes...

 
Back
Top Bottom