Trump apigwa tobo na China mbele ya kizuizi chake

Niaje waungwana

Meli zilizowekewa vikwazo na Marekani zimeonekana kupita katika mlango wa bahari wa Hormuz licha ya kizuizi kilichowekwa na Washington, jambo linaloibua maswali kuhusu ufanisi wa hatua hiyo.

Kwa mujibu wa takwimu za ufuatiliaji meli, meli ya China iitwayo Rich Starry ilivuka mlango huo mapema siku ya leo Jumanne na kuwa ya kwanza kufanya hivyo tangu kuanza kwa kizuizi hicho. Pia ilifanikiwa kutoka katika eneo la ghuba, hatua inayoashiria uwezekano wa kupenya kwa usafirishaji licha ya vizuizi.

Meli hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Shanghai Xuairun Shipping Co Ltd, iliwekewa vikwazo na Marekani kutokana na uhusiano wake wa kibiashara na Iran. Hata hivyo haikuweza kupatikana mara moja kwa maelezo zaidi.

Taarifa kinaonesha kuwa Rich Starry ilikuwa imebeba takribani mapipa 250,000 ya methanol.

Katika maendeleo mengine, meli nyinyine iliyowekewa vikwazo Murlikishan nayo iliingia katika mlango wa Hormuz siku hiyo hiyo ya leo Jumanne.
Kisha kimbia kaogopa Al Houthi wasiwatandike kwa nyuma USA kwisha habari yake hata USA wenyewe wanasema Iran kaidhalilisha sana USA kwa sasa hatuwezi kumshinda vita tena ya anga China siku wakipigana na China ndio walicho kuwa wanajitambia USA na zile Carriers zao zote zimeonekana ni mayai tu 😆
 
Kivipi fafanua kidogo. Mana iyo meli ya China Iranian toka wanzo hawajawahi kuzuiya Meli ya China kwenda popote iwe kwao au Gulf States!!!
Meli za china na Russia zimekwama zaidi ya mwezi haziendi Cuba

Sijafuatilia Kwa ukaribu kama kweli Marekani ashaanza kuzuia meli kutoka au kuingia Iran

Ila Nina uhakika kaka mkuu wa Dunia Marekani akizuia hakuna mbwa yeyote atapeleka uso wake hapo
 
Cuba wamepokea mafuta kutoka Russia juzi tu na kwasasa Umeme upo Cuba!!!

japo waumini wenzio w Kikristo wenye Cuba yao wanafanya Ibada kwa utulivu Kwenye Makanisa Ktk Dunia omba sn mungu akupe Akili,,,

Mkristo wa TZ anashangilia Wakristo wenzeke watoto kinababa kinamama wagonjwa maospitalini ndani ya Cuba wanaoteshwa na Marekani pasi na kosa lolote😇😇😇
 
Lazima wahuni wakipate
Bado naomba Mungu Trump atue huku atunyoshee hawa madikteta wa sisiem
 
Meli za china na Russia zimekwama zaidi ya mwezi haziendi Cuba

Sijafuatilia Kwa ukaribu kama kweli Marekani ashaanza kuzuia meli kutoka au kuingia Iran

Ila Nina uhakika kaka mkuu wa Dunia Marekani akizuia hakuna mbwa yeyote atapeleka uso wake hapo
Uhakika kufa tu
Kama unamuamini marekani kwa mwaka huu wa 2026 pole
Hata T14 Armata anaona aibu kuja kuzitetea zile kariya
 
Kisha kimbia kaogopa Al Houthi wasiwatandike kwa nyuma USA kwisha habari yake hata USA wenyewe wanasema Iran kaidhalilisha sana USA kwa sasa hatuwezi kumshinda vita tena ya anga China siku wakipigana na China ndio walicho kuwa wanajitambia USA na zile Carriers zao zote zimeonekana ni mayai tu 😆
Marekani ni super power wa media tu, lkn kiuhalisia hata anachapika vibaya sana sasa hivi.
 
Kivipi fafanua kidogo. Mana iyo meli ya China Iranian toka wanzo hawajawahi kuzuiya Meli ya China kwenda popote iwe kwao au Gulf States!!!
Achana nae huyo myahudi wa gongo la mboto. Atakuchosha bure.
 
Mr Bean ana akili na uwezo mkubwa wa kufikiri zaidi ya Trump.

Trump angekuwa Afrika, hakuna nchi ambayo ingempa uraisi.
Ukitoa traore, kiongozi gani mwinge kusini kwa jangwa la Sahara ana akili?
 
Trump yeye angekuwa zaidi ya hao unaoona hawana akili. Kidogo angechuana na hayati mzee Majuto kwenye fani ya uchekeshaji.
 
Ni kweli kwamba mlango huo sasa unadhibitiwa na Marekani badala ya Iran?
Unauliza swali ama vipi, mkuu Marekani anadhibiti mlango hewa, US wamenda kujitega maeneo ya mbali huko bahari kuu International water wamekimbia moto wa Iran karibu na mlango wa Homorz, ni kama wewe upo Dodoma unayazuia mabasi ya abiria yasiende mikoa mingine
 
Wanajeshi wa Marekani wanaogopa kufa na kuzamishwa majini 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom