Trump Asema Anamheshimu Sana Zelensky, ni Kiongozi Jasiri. Haamini Alimwita Dikteta

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,362
Reaction score
48,879
Rais Trump wa Marekani anatarajiwa kukutana na Rais Zelensky wa Ukraine, siku ya leo, ikulu ya Marekani White House.

Jana, Rais Trump akisubiria ujio wa Rais Zelensky, alimsifia kiongozi huyo kuwa ni kiongozi jasiri, na kwamba anamheshimu sana.

Rais Trump, alipoulizwa kama yupo tayari kumwomba msamaha kwa kumwita dikteta, Trump alisema kuwa kwanza haamini kama aliwahi kutamka hivyo.

Rais Trump amesema kuwa anatarajia kikao chake cha leo na Zelensky kitakuwa kikao kizuri, na kwamba mipango ya kuleta amani inakwenda vizuri.

Habari kamili toka BBC, hii hapa:


  • BBC News
US President Donald Trump has said he has a "lot of respect" for Ukrainian President Volodymyr Zelensky, on the eve of their talks at the White House.
Asked by the BBC if he would apologise for recently calling him a "dictator", he said he could not believe he had said this. He also called Zelensky "very brave".
Trump was speaking after talks with UK Prime Minister Sir Keir Starmer about ending the war between Ukraine and Russia.
He predicted a "very good meeting" with Zelensky on Friday, saying efforts to achieve peace were "moving along pretty rapidly".
 
Trump uropokaji sana, haelewi namna diplomacy inafanya kazi
 
Trump kama malaya wa Kimboka. Anaweza kukutukana ila ukimuonyesha kibunda tu anakuita baby hapo hapo.
 
Trump labda anaumwa akili. Moja ya dalili za magonjwa ya akili kwa wazee ni kusahausahau, labda kashasahau kwamba alimwita Zelensky dikteta.

Au pengine ni muongo tu anajifanya kasahau.

Yote mawili ni majanga.
 
Mzee wa win win situation
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…