Trump asema Marekani itaipa Ukraine silaha hatari na za kisasa huku akimkosoa Putin

Marekani haijawahi kusitisha Upelekaji wa Silaha Ukraine tangu vita vianze, licha kelele za Trump huenda ndiyo maana Putin hataki kusikia.
US ilichofanya ni kuendelea kufanya biashara ya silaha na nchi za NATO ambazo kwa sababu ni vibaraka wake zikapigane na Russia.
Hata hivyo hata US ingeisaidiaje Ukrain haitabadilisha cho chote sana sana itarefusha vita.
Mimi Ninaona hata ingekuwa Russia anapigana na marekani yenyewe asingefua dafu muamerika.
 
Kumbe hujui muundo na taratibu za silaha kwa Marekani. Marekani haitoi wala kuuza silaha za toleo la mwisho kabisa. Ukiona wanatoa silaha wanayoiita katest version kwa taifa jingine, lazima wao wawe na version iliyo bora zaidi.
Sasa si watoe tuone,maneno mengi mwisho wa siku wanatoa silaha hizo hizo hambazo haziwezi leta mabadiliko yoyote.
 
Rais wa Marekani Donald Trump ameashiria kauli "kuu" kuhusu Ukraine hii leo, huku kukiwa na kile kinachoonekana kuzidi kukasirishwa na Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Siku ya Jumapili usiku, Trump alisema kuwa vifaa vya kijeshi "vya kisasa" vitaelekea Ukraine, ikiwa ni pamoja na makombora ya ulinzi wa anga ya Patriot.

Na rais wa Marekani alionekana kukerwa na kutochukua hatua kwa Moscow kuelekea usitishaji mapigano nchini Ukraine, akiwaambia waandishi wa habari kwamba "Putin ... anazungumza vizuri na kisha anapiga kila mtu jioni".

Maoni yake yanafuatia mahojiano siku ya Alhamisi, ambapo aliahidi kutoa "taarifa kuu" leo.

Chombo cha habari cha Marekani Axios kiliripoti jana usiku kwamba rais anafikiria kutuma silaha za mashambulizi nchini Ukraine.

Kufikia sasa, Trump ametoa silaha za kujihami pekee kwa taifa - kama vile mfumo wa Patriot.

Trump atakutana na mkuu wa Nato Mark Rutte leo katika Ikulu ya White House, na mjumbe maalum wa Marekani nchini Ukraine, Keith Kellogg, yuko Kyiv wiki hii kwa mazungumzo.
Wakati mwingine sirahisi kumuelewa Trump - ni flip flopper kweli kweli, leo atasema hili kesho lile!!!

Trump huyu huyu si alikuwa anamulahumu sana Zelensky kwamba hataki amani ya kweli huko Ukraine, siku moja Trump na Zelensky walipishana kiswahili mpaka Zelensky akatimuliwa unceremoniously kutoka White House, baadae Trump akataka kufanya deal ya kuuziwa madini adimu kutoka Ukraine, alipo fanikiwa kufanya deal na Zelensky ndiyo sasa anajifanya kuwa karibu na Zelensky ili aendelee kuiba/chota madini adimu ya Ukraine wa bei nafuu sana baadae Trump anaiidhinisha Ukraine iendelee kuuziwa silaha za masafa marefu kutoka Merikani!!

Binafsi naona vita hii inavyo paliliwa na Merikani, Uingereza, Ufaransa pamoja na mataifa mengine ya EU kwa shinikizo LA Ufaransa na Uingereza Dunia hisipo kuwa makini basi vita hii ita anzisha WW3, kwa bahati mbaya sioni kama Viongozi wa EU na Merikani hilo wanaliona, badala yake wako overly obsessed/wanaota to destroy Russia completely!! Yaani hawana hata habari kwamba kuichezea Urusi unajitafutia balaa, wanayo yafanya huko Ukraine ni cha mtoto!! Urusi ikihamua kutoa makucha yake kamili Ulaya na Merikani hapatakalika.
 
Trump bwana alimuingiza Chaka Netanyau kachapika na Sasa anataka kumuingiza Chaka Zelensk Ili amalizwe

Huyu Trump ana lake jambo sio Bure au ameshachoka kuwasaidia anataka wamalizwe fasta Ili apumzike
Kuna sehemu nimesoma Trump huyu huyu akisema kwamba Ukraine itashindwa vita muda si mrefu kuanzia sasa - unawezaje kumchukulia seriously binadamu ambaye hatabiriki, leo ajifanya kuelewana na Putin na kuanza kuilahumu Ukraine na Zelensky - kesho anaelewana tena na Zelensky baada ya kuongwa vitalu vya madini adimu huko Ukraine!! Yote tisa lakini ukweli utabaki kwamba Urusi itashinda vita hii regardless ya muungano of the willing suicidal squad, vyote watachakazwa kweli kweli na URUSI.
 
P
Usiwe unaandika vitu usivyo na uelewa navyo. Jibu maswali yafuatayo:

1. Ukraine imeomba lini kuwa mwanachama wa NATO?

2. Urusi ilianza lini kuyateka maeneo Ukraine?

Kama hujui Urusi kwa mara ya kwanza iliyachukua maeneo ya Ukraine, Crimea, Donetsk na Luhansk mwaka 2014. iliivamia Ukraine kwa mara ya kwanza mwaka 2014.

Kama hujui, Ukraine iliomba kujiunga na NATO ili kujilinda na uvamizi wa Putin, baada ya kudhihirika wazi kuwa Putin baada ya kuyachukua maeneo ya Crimea, Donetsk na Luhansk, bado alikuwa na tamaa ya kuchukua maeneo mengine ya Ukraine.

Chanzo cha tatizo ni Putin kuyachukua maeneo ya Ukraine na kuyafanya sehemu ya Urusi.
Pumba tupu
 
Kwani tokea mwanzo Ukraine haikua na ulinzi wa anga?
Kama haikua nao walikosea sana maana wanakuja kuleta Leo wakati Ukraine imekwisha chakazwa mno.

Ok hebu tufanye kwamba ilikuanao ulinzi wa anga ,je ulienda wapi?.

Je huo watakao leta safari hii ni tofauti na ule wa mwanzo?

Nimesikia watapeleka Patriots,je ni toleo jipya?

Tujikumbushe:
Juveline
Bradley
Himars
Challenger
Leopard
Abraham's
Storm shadows
Atacms
Patriots
F-16
.
.
.
Chuck Norris
Anold Schwarzenegger
Sylvester Stallone(Rambo)
Jean Claude van Damme
Bruce Willis
James Bond 007
 
Mimi Ninaona hata ingekuwa Russia anapigana na marekani yenyewe asingefua dafu muamerika.
Hao USA wenyewe wanakwambia "the only battle US won independently and accurately is operation Cabanatuan" Ile ya 1944 kama sijakosea,baada ya hapo hakuna vita USA alishinda akiwa mwenyewe.
USA hana ubavu wa kupambana na jeshi korofi kama Urusi wee hana.
 
Wakati mwingine sirahisi kumuelewa Trump - ni flip flopper kweli kweli, leo atasema hili kesho lile!!!

Trump huyu huyu si alikuwa anamulahumu sana Zelensky kwamba hataki amani ya kweli huko Ukraine, siku moja Trump na Zelensky walipishana kiswahili mpaka Zelensky akatimuliwa unceremoniously kutoka White House, baadae Trump akataka kufanya deal ya kuuziwa madini adimu kutoka Ukraine, alipo fanikiwa kufanya deal na Zelensky ndiyo sasa anajifanya kuwa karibu na Zelensky ili aendelee kuiba/chota madini adimu ya Ukraine wa bei nafuu sana baadae Trump anaiidhinisha Ukraine iendelee kuuziwa silaha za masafa marefu kutoka Merikani!!

Binafsi naona vita hii inavyo paliliwa na Merikani, Uingereza, Ufaransa pamoja na mataifa mengine ya EU kwa shinikizo LA Ufaransa na Uingereza Dunia hisipo kuwa makini basi vita hii ita anzisha WW3, kwa bahati mbaya sioni kama Viongozi wa EU na Merikani hilo wanaliona, badala yake wako overly obsessed/wanaota to destroy Russia completely!! Yaani hawana hata habari kwamba kuichezea Urusi unajitafutia balaa, wanayo yafanya huko Ukraine ni cha mtoto!! Urusi ikihamua kutoa makucha yake kamili Ulaya na Merikani hapatakalika.
Bahati mbaya maeneo yenyewe ya madini mkakati/adimu ameyateka Russia 😂😂😂😂.
Tuone US akipeleka jeshi kuyakomboa.
 
Hio hasira yote ni kisa Russia kuomba kuisaidia Iran dhidi ya Israel..
Tokea lini Mrusi alimsaidia Iran, sa ndio ataipata, Iran alikuwa anamsaidia yeye hakumsaidia kabisa Iran, na Trump kisha lijua hilo. Mrusi atapigika kama mtoto sasa. Hizo drones anazo tumia ni technology kaiba kwa Iran na zingine ni drones za Iran. Safari hi Iran atakaa pembeni tu akitazama.
 
Russia kupigika ni ngumu kwasababu North Korea amepeleka jeshi na silaha pia.
Russia kupigika ni nearly impossible mkuu.
Hiyo Kursk imekombolewa kwa nguvu ya askari wa Pyongyang.
 
Rais wa Marekani Donald Trump ameashiria kauli "kuu" kuhusu Ukraine hii leo, huku kukiwa na kile kinachoonekana kuzidi kukasirishwa na Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Siku ya Jumapili usiku, Trump alisema kuwa vifaa vya kijeshi "vya kisasa" vitaelekea Ukraine, ikiwa ni pamoja na makombora ya ulinzi wa anga ya Patriot.

Na rais wa Marekani alionekana kukerwa na kutochukua hatua kwa Moscow kuelekea usitishaji mapigano nchini Ukraine, akiwaambia waandishi wa habari kwamba "Putin ... anazungumza vizuri na kisha anapiga kila mtu jioni".

Maoni yake yanafuatia mahojiano siku ya Alhamisi, ambapo aliahidi kutoa "taarifa kuu" leo.

Chombo cha habari cha Marekani Axios kiliripoti jana usiku kwamba rais anafikiria kutuma silaha za mashambulizi nchini Ukraine.

Kufikia sasa, Trump ametoa silaha za kujihami pekee kwa taifa - kama vile mfumo wa Patriot.

Trump atakutana na mkuu wa Nato Mark Rutte leo katika Ikulu ya White House, na mjumbe maalum wa Marekani nchini Ukraine, Keith Kellogg, yuko Kyiv wiki hii kwa mazungumzo.
Ameshindwa kuvimaliza hivyo vita kama alivyoahidi.
 
Nadhani mleta mada, hili tamko lilikuwa hyped kuliko kilichotokea na ujalifafanua vizuri.
Watu hasa Ukraine na Ulaya walitegemea vikwazo zaidi dhidi ya Urusi, kitu ambacho hakijafanyika.

Mbili, marekani hatopeleka msaada, bali zitanunuliwa na Ulaya kwenda Ukraine (Ulaya ndio italipa cost ya hizo silaha) sio free.

Pia kaponda muundo wa NATO uliopo, kuwa umepitwa na wakati
 
Tokea lini Mrusi alimsaidia Iran, sa ndio ataipata, Iran alikuwa anamsaidia yeye hakumsaidia kabisa Iran, na Trump kisha lijua hilo. Mrusi atapigika kama mtoto sasa. Hizo drones anazo tumia ni technology kaiba kwa Iran na zingine ni drones za Iran. Safari hi Iran atakaa pembeni tu akitazama.
Acha uongo, mrusi hakukataa kumsaidia Iran. Iran ndio ilitaka hiachwe yenyewe kwani ilikua na uwezo wa kumchakaza adui. Ilikua ni mapema sana kwa mrusi kwenda kutoa msaada
 
Usiwe unaandika vitu usivyo na uelewa navyo. Jibu maswali yafuatayo:

1. Ukraine imeomba lini kuwa mwanachama wa NATO?

2. Urusi ilianza lini kuyateka maeneo Ukraine?

Kama hujui Urusi kwa mara ya kwanza iliyachukua maeneo ya Ukraine, Crimea, Donetsk na Luhansk mwaka 2014. iliivamia Ukraine kwa mara ya kwanza mwaka 2014.

Kama hujui, Ukraine iliomba kujiunga na NATO ili kujilinda na uvamizi wa Putin, baada ya kudhihirika wazi kuwa Putin baada ya kuyachukua maeneo ya Crimea, Donetsk na Luhansk, bado alikuwa na tamaa ya kuchukua maeneo mengine ya Ukraine.

Chanzo cha tatizo ni Putin kuyachukua maeneo ya Ukraine na kuyafanya sehemu ya Urusi.
upo sahihi ndugu huu uchambuzi wako upo sawa ndio ukweli ila kuna makobazi wenye mahaba na Putin wanajichetuaga kumsukumia lawama zote Zelesky ndio chanzo cha hii vita vya uvamizi wa shetan Putin Sasa sijui Zelesky anakuwaje chanzo wakati mvamizi anajulikana na anaendelea kuua waukraine na kuteka ardhi ya ukraine

Sent from my Infinix X663 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom