Trump asema Marekani itaudhibiti kijeshi Mlango-Bahari wa Hormuz

Wakusoma 12

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2017
Posts
5,503
Reaction score
15,858
Rais wa Marekani Donald Trump amesema Marekani itaweka “kizuizi cha kijeshi” na kuudhibiti Mlango Bahari wa Hormuz, njia muhimu ya usafirishaji wa mafuta duniani, kufuatia kushindwa kwa mazungumzo kati ya Marekani na Iran.

Trump amesema kupitia ujumbe wake katika mtandao wa Truth Social kuwa Jeshi la Wanamaji la Marekani litachukua hatua hiyo baada ya mazungumzo ya ngazi ya juu yaliyofanyika Islamabad, Pakistan, kushindwa kufikia makubaliano pamoja na mambo mengine, kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.

Ameongeza kuwa mazungumzo hayo yalivunjika kwa sababu Iran “haiko tayari kuachana na malengo yake ya nyuklia,” akisisitiza kuwa Washington ilihudhuria mazungumzo hayo kwa nia ya kutafuta suluhu ya kudumu.

Hatua hiyo inakuja wakati mvutano kati ya Marekani na Iran ukiendelea kuongezeka, huku juhudi za kidiplomasia za muda mrefu zikishindwa mara kadhaa kufanikisha makubaliano kuhusu mpango wa nyuklia wa Tehran.

Mlango Bahari wa Hormuz ni njia muhimu ya kimkakati inayopitisha sehemu kubwa ya mafuta ya dunia kutoka Mashariki ya Kati, na hatua ya Marekani inaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa masoko ya nishati na usafirishaji wa kimataifa.
 
Tafsiri rahisi ya kufunga mlango bahari wa Hormuz.,..

Rais Donald Trump ameshiriki makala kwenye Truth Social inayoelezea mkakati unaowezekana wa Marekani wa kuizingira Iran kwa jeshi la majini (naval blockade), baada ya mazungumzo kati ya Marekani na Iran mjini Islamabad kumalizika bila kufikiwa makubaliano.

Blockade ni Nini Kijeshi?

Tofauti na vikwazo vya kawaida vya kiuchumi, Naval Blockade ni kitendo cha kivita ambapo Marekani itatumia meli zake za kivita kuzuia kitu chochote kuingia au kutoka nchini Iran kupitia baharini. Vitu vinavyozuiliwa:

1. Hakuna Mafuta

Iran haitaweza kuuza hata pipa moja la mafuta nje.

2. Hakuna Chakula wala Dawa

Kila meli inayoelekea bandari za Iran (kama Bandar Abbas) itasimamishwa, kukaguliwa, au kugeuzwa na jeshi la Marekani.

3. Kukata Mapato

Hii itaiyeyusha ile akiba ndogo ya fedha ambayo Iran imebaki nayo ndani ya wiki chache.

Mkakati wa "Mtego wa Chuma"

Makala aliyoishiriki Trump inadokeza kuwa Marekani inaweza kutumia:

Meli za Kubeba Ndege (Aircraft Carriers): Zitalinda Mlango-bahari wa Hormuz na Bahari ya Oman.
Nyambizi (Submarines): Zitafuatilia meli yoyote ya siri inayojaribu kupita chini ya rada.

Droni za Majini: Zitafanya doria saa 24 kuhakikisha hakuna mashua ya Iran inayothubutu kutega mabomu mapya baada ya zile 28 za mwanzo kuzamishwa.

Kwanini Sasa?

Trump anatumia mbinu yake ya zamani ya "Maximum Pressure": Baada ya Iran kukataa masharti ya Marekani usiku kucha, Trump anataka kuwaonyesha kuwa "Gharama ya kusema HAPANA ni kubwa."

Ujumbe kwa China

Blockade hii pia ni onyo kwa China, ambayo ndiyo mnunuzi mkuu wa mafuta ya Iran. Marekani inasema, "Kama mnataka mafuta ya Iran, itabidi mpambane na jeshi letu la majini."
 
Hili likitokea basi tutashuhudia vita ya 3 ya dunia!kwani washirika wa IRAN hawatakubali rafiki yao IRAN afe kwa njaa!
AFRICA SIYE TUJIANDAE KWA UCHUMI MGUMU HAIJAWAHI SHUHUDIWA.
 
Back
Top Bottom