Trump asema Marekani itaudhibiti kijeshi Mlango-Bahari wa Hormuz

Trump asema Marekani itaudhibiti kijeshi Mlango-Bahari wa Hormuz

Usimlinganishe magufuli na vitu vya kipuuzi, huyu mzee ni mropokokaji aliye muongo sana, mwanzoni alisema vita itaisha mda mfupi sana, na lengo kubwa ni regime change vipi ameshafanikiwa mpaka sasa kuondoa mfumo unaotawala irani.
Trump ni tapeli, pressure nyumbani inazidi na zikipita siku 60 tangu mapigano yaanze, ni ama apate approval ya bunge kuendelea na vita au asitishe vita.

Yuko njia panda baada ya kushindwa kufikia malengo ya vita.
 
Muda mfupi alisema ni masaa Siku miezi au mwaka?
alisema vita itaisha "shortly" (ndani ya muda mfupi),alisema itachukua wiki 2 hadi 3 za mashambulizi makali kabla ya kumaliza operesheni.

Alisisitiza pia:
“Any time I want it to end, it will end”
Al Jazeera.

Aiya niambie hii vita imechukua mda gani? Napia malengo ya vita hii yametimizwa? ndioo maana tukisema huyu mzee ni mtu wa mikwala,mpenda sifa na mlopokoji muwe mnaelewa.
 
China na India ndiyo wanunuzi wakubwa wa mafuta ya Iran huyu Russia sio mnunuzi wa mafuta ya Iran.
China kama kawaida hawa ni watu wa diplomatic, Kwakifupi kama hii mbinu mpya ya marekani itatiki basi tutegemee Iran kuanguka yenyewe.

Tukumbuke hapa hakuna kurushiana mabomu wala mizinga hapa imetumika Akili kubwa ya Kiuchumi...Acha tusubiri tuone itakuaje
Cha kwanza ni uongo India ilisha acha kununua mafuta ya Iran muda mrefu sana.
Alafu kingine meli zinazo tegemea kupita hapo si za Iran tu tena watumiaji wakubwa wa mfereji huo ni maswahiba wa marekani.
Apa alicho kifanya marekani ni ile tukose wote.
 
China na India ndiyo wanunuzi wakubwa wa mafuta ya Iran huyu Russia sio mnunuzi wa mafuta ya Iran.
China kama kawaida hawa ni watu wa diplomatic, Kwakifupi kama hii mbinu mpya ya marekani itatiki basi tutegemee Iran kuanguka yenyewe.

Tukumbuke hapa hakuna kurushiana mabomu wala mizinga hapa imetumika Akili kubwa ya Kiuchumi...Acha tusubiri tuone itakuaje
Mkuu PureView zeiss huku bado ni pakubwa sana kwako cha kukushauri jikite tu kwenye uchambuzi wa magari hasa ya subaru forester maana ndipo ulipo bobea sana.
 
ila Iran anayefadhili makundi ya kigaidi kama Hezbollah,na anayetishia kila mara kuifuta Israel sio mleta vita

Gaidi kubwa ni HILI HAPA:

Hii ni orodha ya baadhi ya nchi ambazo zimewahi kuripotiwa kuathiriwa na shughuli za Central Intelligence Agency , CIA , kulingana na tafiti za kihistoria, ripoti zilizofichuliwa, na wanahistoria:

Amerika ya Kusini & Kati​

Guatemala (1954 – mapinduzi dhidi ya serikali)
  • Chile (1973 – kuangushwa kwa Salvador Allende)
  • Cuba (jaribio la Bay of Pigs 1961)
  • Nicaragua (Contra War)
  • Honduras (kituo cha operesheni za Contra)

Mashariki ya Kati​

  • Iran (1953 – mapinduzi dhidi ya Mohammad Mossadegh)
  • Iraq (miaka ya 1960–2000s, msaada na uingiliaji mbalimbali)
  • Syria (majaribio ya mapinduzi 1949+)

Asia​

  • Afghanistan (Operesheni Cyclone dhidi ya USSR)
  • Vietnam (Vita ya Vietnam)
  • Indonesia (1965 – purge dhidi ya wakomunisti)

Afrika​

  • Congo (DRC) (kuhusishwa na kuuawa kwa Patrice Lumumba)
  • Angola (vita vya wenyewe kwa wenyewe)

Ulaya​


Italy (Operesheni Gladio – vita baridi)
Greece (mapinduzi ya kijeshi 1967)
 
Rais wa Marekani Donald Trump amesema Marekani itaweka “kizuizi cha kijeshi” na kuudhibiti Mlango Bahari wa Hormuz, njia muhimu ya usafirishaji wa mafuta duniani, kufuatia kushindwa kwa mazungumzo kati ya Marekani na Iran.

Trump amesema kupitia ujumbe wake katika mtandao wa Truth Social kuwa Jeshi la Wanamaji la Marekani litachukua hatua hiyo baada ya mazungumzo ya ngazi ya juu yaliyofanyika Islamabad, Pakistan, kushindwa kufikia makubaliano pamoja na mambo mengine, kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.

Ameongeza kuwa mazungumzo hayo yalivunjika kwa sababu Iran “haiko tayari kuachana na malengo yake ya nyuklia,” akisisitiza kuwa Washington ilihudhuria mazungumzo hayo kwa nia ya kutafuta suluhu ya kudumu.

Hatua hiyo inakuja wakati mvutano kati ya Marekani na Iran ukiendelea kuongezeka, huku juhudi za kidiplomasia za muda mrefu zikishindwa mara kadhaa kufanikisha makubaliano kuhusu mpango wa nyuklia wa Tehran.

Mlango Bahari wa Hormuz ni njia muhimu ya kimkakati inayopitisha sehemu kubwa ya mafuta ya dunia kutoka Mashariki ya Kati, na hatua ya Marekani inaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa masoko ya nishati na usafirishaji wa kimataifa.
Walokole wa tz ni mabumunda, vitu vya kijinga na ambavyo haviwezekani kwasababu vimetamkwa na marekani mnavisapoti na kuvifurahia

Hiyo plani ya ukichaa anataka kuiweka Trump, haitawezekana kwa sababu ya uchumi wa dunia. Ni taahira pekee anayeweza kusema jambo hilo litawezekana
 
Walokole wa tz ni mabumunda, vitu vya kijinga na ambavyo haviwezekani kwasababu vimetamkwa na marekani mnavisapoti na kuvifurahia

Hiyo plani ya ukichaa anataka kuiweka Trump, haitawezekana kwa sababu ya uchumi wa dunia. Ni taahira pekee anayeweza kusema jambo hilo litawezekana
Wapuuzi wanafikiri kiongozi wa marekani ndiye mungu.
 
Duniani kwa sasa Kuna viongozi Hawa ndio waleta chokochoko
Dornad Trump
Benyamin Netanyahu
Viladmil Putin
Kim jong UN
Xi Jinping
Dunia haitakuja kutulia kama hv vichwa vipo madarakan
 
ila Iran anayefadhili makundi ya kigaidi kama Hezbollah,na anayetishia kila mara kuifuta Israel sio mleta vita
Dogo naona huiamini bibilia ya Paulo si alisema atakaye igusa nchi ya israel atamdhuru mbona hilo taifa teule lenu linasaidiwa na America sasa

Nyie semeni ukweli tu Mungu alimkusudia Yakobo sio taifa fake na mungu fake mnaye muabudu.
 
China na India ndiyo wanunuzi wakubwa wa mafuta ya Iran huyu Russia sio mnunuzi wa mafuta ya Iran.
China kama kawaida hawa ni watu wa diplomatic, Kwakifupi kama hii mbinu mpya ya marekani itatiki basi tutegemee Iran kuanguka yenyewe.

Tukumbuke hapa hakuna kurushiana mabomu wala mizinga hapa imetumika Akili kubwa ya Kiuchumi...Acha tusubiri tuone itakuaje
Acha kudanganya watu
 
Baada ya kushindwa regime change nk kaona aje na hiki kituko chengine huyu super power wa mchongo
Iran imeishi na vikwazo kwa miaka 47
Tulikua tunawaambia kama iran sio waarabu mukawa munajitoa akili haya sasa
Na iran akikipita hiki kipindi salama hiiiiiiiii
 
Rais wa Marekani Donald Trump anasema Jeshi la Wanamaji la Marekani litaanza mara moja kufunga Mlango wa Hormuz na pia litazuia kwa nguvu kila meli katika maji ya kimataifa ambayo yaliisababishia Iran hasara.

Hatua hiyo inafuatia mazungumzo yasiyofanikiwa kati ya Marekani na Iran jana nchini Pakistan, ambapo pande hizo mbili zilishindwa kufikia makubaliano ya kukomesha vita vya wiki sita katika Mashariki ya Kati.

Trump, katika chapisho kuhusu Ukweli wa Jamii, anadai kwamba mazungumzo ya kihistoria "yalienda vizuri" kwa sehemu kubwa, lakini "jambo pekee lililokuwa muhimu sana, NUKLIA, halikukubaliwa" na Iran.

"Kuanzia sasa mara moja," anasema, Jeshi la Wanamaji la Marekani "litaanza mchakato wa KUZIBA na kuzuia Meli zozote zinazojaribu kuingia, au kuondoka, Mlango wa Hormuz."

Trump anadai "nchi zingine" pia zitahusika katika kizuizi chake, lakini hazitaji kwa majina.

Anaishutumu Iran kwa "ulaghai wa dunia" kwa kusema kwamba ilikuwa imechimba Mlango wa Hormuz, na anarudia tangazo lake kwamba Marekani itaanza hivi karibuni kuondoa mabomu kwenye mlango huo.

"Pia nimewaagiza Jeshi letu la Wanamaji kutafuta na kusimamisha kila meli katika Maji ya Kimataifa ambayo imelipa ushuru kwa Iran. Hakuna mtu anayelipa ushuru haramu atakayepitia salama baharini," Trump anatangaza.

Akirudia lugha ya uchochezi aliyotumia katika siku zilizotangulia usitishaji mapigano dhaifu wa wiki mbili uliosimamiwa na Pakistan, Trump anasema: "Mwirani yeyote anayetufyatulia risasi, au meli za amani, atapigwa jehanamu! Iran inajua, bora kuliko mtu mwingine yeyote, jinsi ya KUKOMESHA hali hii ambayo tayari imeharibu Nchi yao."
 

Attachments

  • IMG_20260413_005451_953.jpg
    IMG_20260413_005451_953.jpg
    244.4 KB · Views: 20
Back
Top Bottom