Trump asitisha misaada ya ARV na dawa za Malaria kwa muda

Mpigania uhuru wa pili

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2023
Posts
3,380
Reaction score
6,376
Utawala wa Rais Donald Trump umeamua kusitisha usambazaji wa dawa muhimu za kuokoa maisha kwa magonjwa ya VVU, malaria, na kifua kikuu, pamoja na vifaa vya matibabu kwa watoto wachanga, katika nchi zinazosaidiwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID).

Hatua hiyo ni sehemu ya kusimamisha kwa muda msaada wa Marekani duniani kote ili kupitia upya programu hizo. Taarifa hiyo imetolewa kwa wakandarasi na washirika wanaofanya kazi na USAID, ikiwa ni pamoja na kampuni ya Chemonics, ambayo inashirikiana na USAID kusambaza dawa hizo muhimu duniani kote.
 
Trump hacheki na wowote. Na condom zitaadimika.

Trump kapewa urais 🔥, kila mtu ashinde mechi zake. Subiri azuie hela kwenye misaada na benki ya dunia na IMF.

Kila nchi itakula ilipopeleka mboga. Kama hela zinaenda kuwalipa machawa na kununua maV8 ndio balaa
 
Utawala wa Rais Donald Trump umeamua kusitisha usambazaji wa dawa muhimu za kuokoa maisha kwa magonjwa ya VVU, malaria, na kifua kikuu, pamoja na vifaa vya matibabu kwa watoto wachanga, katika nchi zinazosaidiwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID).

Hatua hiyo ni sehemu ya kusimamisha kwa muda msaada wa Marekani duniani kote ili kupitia upya programu hizo. Taarifa hiyo imetolewa kwa wakandarasi na washirika wanaofanya kazi na USAID, ikiwa ni pamoja na kampuni ya Chemonics, ambayo inashirikiana na USAID kusambaza dawa hizo muhimu duniani kote.
Tushauza maji, miti na madini yoote. Sasa mwaka huu tutauza hadi Oxygen ili tupate hela za kuendeshea bajeti za kula bata na kufanya chaguzi za maigizo
 
Hii kitu sio ya kushangilia, wakati tunasema ni bora ili Serikali ijitegemea ila tuelewe sio Tanzania peke yake inayotegemea hiyo misaada, zipo Nchi zilizoathiiriwa sana na zinauhitaji mkubwa sana wa hizo dawa, so tutarajie vifo vingi vya watoto wachanga, watoto njiti na watu wenye maambukizi ya ukimwi maana imekuwa ghafla. Naamini hakuna Nchi ilitarajia hili
 
Kila mtu apambane na hali yake.

Convoy Moja ya Rais wa Afrika inazidi inqsafiri kwa gharama Kubwa kuliko ya Rais Biden harafu unasena we maskini upewe misada?
 
Back
Top Bottom