Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Dakika chache tu zilizopita, Rais wa Marekani Bw. Donald J. Trump, katangaza kuwa shirika la madawa la Marekani, FDA, limeruhusu dawa ya malaria, ambayo wengi wetu tumeitumia sana, kuanza kutumika katika kutibu virusi vya Corona.
Chloroquin, ndo dawa yenyewe. Matumizi yatakuwa kwenye hatua ya clinical trial.
Idadi ya vidonge vya chloroquin nilivyovimeza maishani mwangu haihesabiki. Achilia mbali sindano zake. Dozi ya sindano ilikuwa ni 1x3.
Hats off kwa “mabeberu”.
Sisi tuna wachawi wengi sana na waganga wengi tu wa kienyeji.
Kama kweli hawa wataalamu wetu wana huo ujuzi ambao hudaiwa wanao, kwa nini washindwe kwenye hili la kutibu Corona?
Heko Marekani. Mchango wake kwenye advancement of humanity hauelezeki kwa maneno.

Nimemsikia Trump akiitaja dawa hii ya Korolokwini kama inauwezo mkubwa wa kufubaza au kutibu kabisa Ugonjwa wa Corona.
Kwa wale Watu wa Umri mkubwa kidogo mtakua mnaikumbuka Dawa hii kwa kipindi kile ndo Ilikua Dawa kuu ya Malaria. Mpaka hapo Baadae ilipoondolewa na Serikali kwenye orodha ya madawa Tanzania.
Dawa hii ni moja ya Dawa zenye nguvu sana zilizotumika kutibu Maralia japo kuna wengine walikuwa na allergy nayo yaani unaweza washwa balaa hasa ukioga maji ya baridi au ukienda Juaini ndo unaitambua kua hiyo ndo korolokwini.
Na ilikuwa ikiona upo na Watu ndio sasa inahamishia Mashambulizi ya Kukuwasha Sehemu mbayambaya tena Nyeti.
Kingine ni Dawa moja Chungu sana haijawahi tokea Duniani. Ukiindumbukiza kwenye Mtungi wa Maji basi huo mtungi hata uoshejwe maji yake lazima yawe Machungu kwa Siku kadhaa.
Mi naiamini inaweza ikawa Dawa ya Corona.
Hongera sana Korolokwini umerudi kivingine
Naamini hutatuangusha na Hujawahi Kutuangusha.
"Wellcome Back Home"