Trump atishia kuichukua Cuba, anadai nchi haina hela wana hali tete

Trump atishia kuichukua Cuba, anadai nchi haina hela wana hali tete

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Rais wa Marekani, Donald Trump, ameashiria kuwa serikali yake bado inalenga kuiondoa madarakani serikali ya Cuba, licha ya vita vinavyoendelea kati ya Israel na Marekani dhidi ya Iran kuingia wiki ya pili sasa tangu Februari 28, 2026. Akizungumza Jumatatu, Trump alisema Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani bado inashughulikia suala la Cuba na kwamba mpango wa Ikulu unaweza kujumuisha kile alichokiita “uchukuaji wa kirafiki” wa kisiwa hicho. Aliongeza kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Marco Rubio, anaendelea kushughulikia suala hilo.

Trump alisema hatua hiyo inaweza kuwa ya kirafiki au isiwe ya kirafiki, akidai kuwa Cuba iko katika hali ngumu kiuchumi na kibinadamu kwa kuwa haina nishati wala fedha za kutosha. Alisisitiza kuwa nchi hiyo italazimika kufanya makubaliano na Marekani au Marekani inaweza kuchukua hatua zake kwa urahisi.

Kwa upande mwingine, Cuba imekuwa ikikabiliwa na mgogoro wa nishati tangu Januari baada ya kusitishwa kwa usafirishaji wa mafuta kutoka Venezuela, ambayo ilikuwa mshirika muhimu wa kiuchumi.

Serikali ya Cuba imekanusha kuwepo kwa mazungumzo ya ngazi ya juu na Washington, ingawa haijakanusha kabisa taarifa za kuwepo kwa mazungumzo yasiyo rasmi kati ya maafisa wa Marekani na Raul Guillermo Rodriguez Castro, mjukuu wa rais wa zamani Raul Castro.




​
==========
​
United States President Donald Trump has signalled that his administration is still pursuing a government overthrow in Cuba even as the US-Israeli war on Iran enters its second week.

Trump said on Monday that the US Department of State is still focused on Cuba, where plans by the White House may or may not include “a friendly takeover” of the island, according to the Reuters news agency. US Secretary of State Marco Rubio is “dealing” with Cuba, the president told reporters in Florida.

“He’s dealing [with it], and it may be a friendly takeover, it may not be a friendly takeover. Wouldn’t really matter because they’re really down to … as they say, fumes. They have no energy, they have no money,” Trump said.

“They are going to make either a deal or we’ll do it just as easy, anyway,” he said.

Cuba has been grappling with an energy crisis since January, when US forces abducted Venezuelan President Nicolas Maduro and halted fuel exports from Caracas to Havana, cutting the country off from one of its few allies and a key source of oil for the Cuban economy.

White House officials have suggested that Cuba is facing an economic collapse and that its government is ready to negotiate with Washington.

Trump has said on multiple occasions that Cuba’s government is ready to “fall” and that its leaders want to “make a deal” with Washington, according to NBC News.

Cuba has denied reports of high-level talks, according to Reuters, but it has not “outright” denied US media reports of “informal talks” between Raul Guillermo Rodriguez Castro, the grandson of former Cuban President Raul Castro, and US officials.

Trump’s attacks on Venezuela and Cuba are in line with his revival of the “Monroe Doctrine”, a 19th-century policy that states the Western Hemisphere should be solely under the sway of the US and no other foreign power.

Source: Al Jazeera
 
Cuba hawana namna, kama hawana mafuta wala fedha za kigeni ni wazi kwamba uchumi wao utasambaratika kabisa na kama kawaida wasanii wa Russia na China hawawezi katu kuwasaidia.

Wajisalimishe ili wapate wokovu na wakijisalimisha ndani ya miaka mitano tu watakuwa wanashindana na Mexico.

Cuba toka ilipotwaliwa na dikteta Fidel Castro ndipo pepo la umaskini lilipoanza kuwanyemelea na matokeo yake mamilioni ya watu wake wamekimbilia Marekani kutafuta maisha mazuri.
 
Sijawahi kuona RAHISI ***** kama huyu mwanzon nilimuona kama yupo timamu kwasasa huyu n chizi
 
Dah! Inasikitisha sana kama wataichukua kinguvu watu wengi wa mbolea wamesomea Cuba Enzo hizo za vuguvugu la ukombozi
Nalog off Z
 
Back
Top Bottom