Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Rais Donald Trump wa Marekani ametishia kusitisha mahusiano na China kutokana na dhima ya taifa hilo katika kusambaa kwa virusi vya corona ambavyo hadi sasa vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 300,000 duniani.
Katika mahojiano yaliyorushwa jana Alhamis Rais Trump amerejea shutuma zake dhidi ya China akisema ilificha ukweli kuhusu ukubwa wa janga hilo wakati virusi vilipozuka mjini Wuhan mwishoni mwa mwaka uliopita.
Akuzungumzia hatua ambazo nchi yake inaweza kuchukua dhidi ya China, Rais Trump amesema Washington inaweza kusitisha uhusiano wote uliopo na Beijing.
Hadi sasa Marekani imerikodi zaidi ya vifo 86,000 kutokana na virusi vya corona, ambayo ni idadi kubwa zaidi kuliko taifa jingine lolote huku ikiwa na karibu theluthi ya maambukizi ya virusi hivyo duniani.
DW