Trump avalia njuga mauaji ya john Kennedy

Makonde plateu

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2022
Posts
1,443
Reaction score
3,480
𝐉𝐄! π‘π€πˆπ’ πŒππ˜π€ 𝐖𝐀 π“π€ππ™π€ππˆπ€ πŸπŸŽπŸπŸ“ ππ€π˜π„ π€π“π€π•π€π‹πˆπ€ 𝐍𝐉𝐔𝐆𝐀 π”π“π„πŠπ€π‰πˆ 𝐖𝐀 π€πŠπˆππ€ π’πŽπŠπ€ 𝐍𝐀 πŒπ€π”π€π‰πˆ π˜π€ πŒπ™π„π„ πŠπˆππ€πŽ?

Trump ametia saini amri ya kufichuliwa kwa nyaraka kuhusu kuuawa kwa Rais John F Kennedy, kaka yake Bobby Kennedy na Mwanaharakati mashuhuri Martin Luther King.

Kwa uelewa wangu na kusoma kwangu natambua kwamba shirika la kijasusi la Marekani CIA ndio waliohusika na mauaji haya.

Inadaiwa Rais Kennedy alikuwa na mgogoro mkubwa sana na CIA baada ya jaribio la kuangusha utawala wa Fidel Castro kule Cuba kushindikana. Kennedy aliamini CIA walimdanganya katika mpango huo huku CIA nao wakiamini kushindwa kwao tatizo ni Rais Kennedy.

Mtakumbuka kwamba CIA ilianzishwa mwaka 1947 baada tu ya kutamatika kwa vita kuu ya dunia. CIA ilitokana na kikosi kazi cha kitaifa kilichoundwa kukusanya na kuratibu vyema vita kuu ya dunia kilichojulikana kama Office of Strategic Services (OSS). Kwa kifupi ni kwamba kikosi kazi hiki cha OSS kilichokuwa na kazi ya kuratibu taarifa za kijasusi wakati wa vita kuu ya dunia kilisajiliwa na kuwa shirika ya kijasusi la Marekani kwa jina la Central Intelligence Agency (CIA).

Kama mnakumbuka baada ya vita kuu ya pili kutamatika kulikotea vita baridi inayoendelea mpaka leo kati Marekani na Umoja wa Kisoviet ambayo kwa sasa ni Urusi. Pamoja na kwamba Marekani na Urusi walikuwa upande mmoja katika vita kuu ya pili, lakini baada ya vita hiyo kutamatika maswahiba hao waligeuka maadui wakubwa na ugomvi wao huo wa vita baridi cold war ulipelekea kugawanyika kwa taifa la Korea na kutokea korea kusini ambayo ilifuata siasa za kibepari za marekani na Korea kaskazini kwa kiduku ambayo ilifuata siasa za kijamaa za usoviet.

Marekani wakipigia chapuo ubepari huku usoviet ukipigia chapuo ujamaa. Hii ilipelekea kila nchi kutafuta uungwaji mkono huku Urusi ikipata uungwaji mkono sana Africa kwani wakati huo nchi nyingi za Africa zilikuwa zinapigania uhuru. Marekani ilipata uungwaji mkono kutoka nchi za Ulaya ambazo automatic zilikuwa adui wa Africa kwa sababu za ukoloni.

Sasa turudi tukio la Kennedy. Kabla ya Kennedy kushinda uchaguzi tayari CIA walikuwa wameandaa mpango wa kuuangusha utawala wa Fidel Castro kwa sababu Fidel tayari alikuwa swaiba wa Usoviet ambao ni maadui wakubwa wa Marekani. Kwamba uswahiba huo ungeweza kuhatalisha usalama wa Marekani.

Kwa hiyo hakuna namna nyingine zaidi ya kuangusha utawala wa Fidel Castro. Kwamba Rais aliyekuwa anamaliza muda wake kabla ya Kennedy tayari alikuwa ameidhinisha dollar milion 13 kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi kwa raia wa Cuba waliokimbia utawala wa Fidel Castro ili kuangusha utawala huo. Kwa bahati mbaya Rais huyo aliondoka madarakani baada ya muda wake kuisha kabla ya kumaliza jukumu hilo na Kennedy akapokea kijiti.

Kwamba baada ya Kennedy kupokea kijiti CIA walimjulisha Kennedy mpango huo lakini hawakumpa mpango mzima kwa sababu ndio alikuwa anaingia madarakani kwa hiyo bado walikuwa hawamuamini. Kwa kuwa CIA walimficha Kennedy mpango mzima na kumpa kipande tu na Kennedy naye hakutaka Marekani ionekane kuivamia Cuba moja kwa moja. Kwa sababu ilikuwa ngumu kuangusha utawala wa Fidel Castro bila mashambulizi ya anga, CIA walimtaka Rais aidhinishe mashambulizi ya anga katika vita hiyo lakini Kennedy alikataa kwamba itaonesha marekani imehusika moja kwa moja. Mpango huo ulifeli na Fidel akaibuka mshindi.

Vita hiyo ilimpa umashuhuri Fidel Castro huku Marekani ikipata aibu duniani. Kennedy alichukia akiwalaumu CIA kwamba walimpa mpango mbovu ulioleta aibu kwa taifa huku CIA nao wakimlaumu Rais Kennedy kuwa ndio tatizo alipokataa kuidhinisha mashambulizi ya anga kwa awamu ya pili.

Rais Kennedy alimfuta kazi Mkurugenzi wa CIA na akaapa kuwa uongozi wake utalifuta kabisa shirika hilo, kabla ya kutimiza mpango huo akauawa. Inadaiwa CIA chini ya Mkurugenzi aliyefutwa kazi ndio walipanga tukio la kuuawa kwa Kennedy. Kwamba kuliko kuifuta CIA ni bora Rais auawe
.
 
Attachments

  • FB_IMG_1737730692720.jpg
    FB_IMG_1737730692720.jpg
    55.9 KB · Views: 3

TAL atutapatia nini hasa kilisababisha kifo cha JPM,kwa nini walificha ugonjwa wa Rais then watutangazie kifo ghafla...
 
Mleta mada umeacha details nyingi muhimu.

Umeacha taarifa za kuwepo kwa silaha za nyuklia za Urusi ndani ya Cuba. Umeacha pia uhusika wa Mafia waliopoteza biashara zao Cuba baada ya kuingia kwa Castro na hii ndiyo kubwa.
 
Back
Top Bottom