Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 10,509
- 16,734
Tofauti na waziri wake wa ulinzi,Hegeseth,Trump yeye hajivungi tena kuhusu kushindwa vita alivyovianzisha na Iran.
Wakati wa mahojiano hapo jana na mashirika ya habari.Trump amerudia kwa mara nyengine kusema kuwa nchi zinazounda umoja wa NATO ni kama chui wa karatasi tu.Akawapa mipasho kama ile ya mitaani,kwamba kama wao walivyoshindwa kumsaidia kupigana na Iran,na yeye hawezi tena kutoa msaada wa kuifungua Homurz peke yake,Kila mmoja akachukue mafuta yake.
Matamko hayo na mengine ameyatoa huku siku sita zikikaribia alizosema anatoa onyo kwa Iran kufungua mlango wa Homurz ili meli za mafuta na gesi zipite,bila hivyo angepiga vikali na kuviripua visima vyote vya mafuta pamoja na kushikilia kisiwa cha Kharg kinachosafirisha asilimia 90 ya nishati ya Iran kwenda nje.
Kabla ya onyo hilo kulikuwa na maonyo mengi ambayo Iran waliyapuuza na Marekani kila yakikaribia alibadilisha maneno na kurudi nyuma.
Alipotoa tamko la kwamba kila mtu akachukue mafuta yake pia alisema vita vitakwisha kati ya wiki 3 mpaka 4 zijazo.Hata hivyo kabla wiki hizo 4 leo usiku anatarajiwa kutoa tamko rasmi la kukimbia vita kabla ya kufikiwa kwa lengo lolote kati ya yale yaliyotajwa kama sababu za kuingia vitani akisaidiana na Israel.