Trump: Harris Kamala ameamua "kugeuka mtu mweusi" kwa manufaa ya kisiasa

Alianza lini kujitambua na kujitambulisha kwamba yeye ni mweusi/mwafrika?Katika nchi za Afrika,ana asili ya nchi gani?Anatafuta sympathies?
Kama wewe ni mwanaume ni mwanaume tu haijalishi ulianza kujitambua au kujitambulisha lini kuwa mwanaume, hata hivyo Kamala Harris akiwa chuoni alikuwa mwanachama wa chama cha weusi cha Alpha Kappa Alpha sorority, akiwa seneta alikuwa ni member wa Congressional Black Caucus.

Pia uthibitisho wa u Black American hauhisiani kwa vyovyote na nchi ya Africa mtu anayotoka, Jamaica na Haiti wamejaa Blacks ambao ukiwauliza wametoka nchi gani za Africa utaonekana mwehu tu.
 
kwanini weusi wake iwe hoja ya kutaka kuchaguliwa?.

siku hizi ukitaka kuonewa huruma egemea upande wa WEUSI.
Kwa sababu weupe wa Trump ni hoja katika kuchaguliwa, kwa sababu pia weusi ni hoja katika kutochaguliwa.
 
Maneno ya trump hayahitaji uwe profesa kuyaelewa.

Anachoelezea trunp ni kwamba yule mam anajifanya mweusi wakati huu ili apate kura za watu weusi,na hilo trump ndio anawasanua watu kwamba kwa nini ajifanye ni mtu mweusi.

Sijaona uchochezi hapo
Hajifanyi, ni mweusi.
 
Sentensi yako ya mwisho umeonesha taharuki sana.Black Americans wengi siku hizi hawaishii kujitambulisha/kujitambua tu.Wanaenda mbali zaidi na kuzitambua nchi za asili yao.Labda,wewe mgeni wa hilo.
 
Uislam mwema sana.

Mboora kati yao ni mcha Mungu.
Waarabu walipoanza kuja Africa walikuwa wanawauza babu zetu kama bidhaa na waliwahasi babu zetu wengi tu waliowachukua utumwani.
 
Uislam haujanifundisha kufatilia rangi ya mtu.

Kwani weupe au weusi wa mtu ndiyo kigezo cha ubora wake?
🤣🤣🤣🤣Unakacha ukweli.Huwa mnaupaisha weupe sana.Utasikia mtu anasema..."mzuri kama mwarabu"..."pua yake nzuri kama msomali"..."tunapika mapishi safi ya Kiajemi"...na kadhalika.
 
Sentensi yako ya mwisho umeonesha taharuki sana.Black Americans wengi siku hizi hawaishii kujitambulisha/kujitambua tu.Wanaenda mbali zaidi na kuzitambua nchi za asili yao.Labda,wewe mgeni wa hilo.
General Lloyd Austin amejitambulisha ametoka nchi gani ya Africa?
 
General Lloyd Austin amejitambulisha ametoka nchi gani ya Africa?
Bado sijamfuatilia.Ila,ukumbuke na kuelewa;Wale weusi wa Haiti,Jamaica,Trinidad&Tobago nk wote asili yao ni nchi za Afrika.
 
Kwa sababu weupe wa Trump ni hoja katika kuchaguliwa, kwa sababu pia weusi ni hoja katika kutochaguliwa.
Naona hamuelewi kuwa Rais wa Marekani hapatikani kutokana na sanduku la wapoiga kura.

Hivi hamuelewi kuwa USA ni Republic?
 
Trump ni mpuuzi sana, ila ana kundi kubwa la Wamarekani wajinga wajinga MAGA ambao wana mkubali sana.
Mtu uko hapo mbalizi umeshiba viazi mbatata vya kuchemsha,unaita wenzio wapuuzi?
 
Kwa sababu weupe wa Trump ni hoja katika kuchaguliwa, kwa sababu pia weusi ni hoja katika kutochaguliwa.
Trump hana hizo za Uzungu,Demo ndiyo wanampaint bad.
Nb.Marekani ni multicultural Country...
sijui ni kwanini tudhani US iko monopolized na jamiii mbili tu,kila chaguzi hoja ni wao tu.
Kuna walatino,Indians,local dynamics (Cherokee) waarabu etc lakini hatujawai wasikia wakitaka waaangaliwe kwa jicho la pekee kama weusi watamanivyo.
Democrats wanajua kucheza na akili za mtu mweusi,they actually know..When it comes to presidential voting or anything else ,all blacks will definitely vote along their colour lines sio uwezo wa mtu.

Nb: sitaki Trump ashinde uRais kwa sababu moja tu ;mstakabali wa Ukraine.
haonyeshi Dalili njema ila kwa mambo mengine nataka ashinde
 
Trump ni mpuuzi sana, ila ana kundi kubwa la Wamarekani wajinga wajinga MAGA ambao wana mkubali sana.
Hoja za ubaguzi, uhamiaji, kuilinda Israel zinalipa Sana huko kipindi hiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…