Trump: Harris Kamala ameamua "kugeuka mtu mweusi" kwa manufaa ya kisiasa

Watu weusi wanajibagua wenyewe.
Kama unaambiwa ni mweusi wakati ni mweusi kweli, sasa umebaguliwaje hapo ?
Ulitaka uambiwe ni mtu mweupe ndio uone kuwa hujabaguliwa ?
Kwanini unaukataa ukweli kuwa wewe ni mtu mweusi ?
Trump anadai Kamala sio mweusi ila kajitwisha Uweusi kwa manufaa ya kisiasa
 
Trump ni mpuuzi sana, ila ana kundi kubwa la Wamarekani wajinga wajinga MAGA ambao wana mkubali sana.
Werevu ndiyo wanamkubali, wapuuzi ni wale walioamua kumuelewa kwa akili zao badala ya kusubiri walishwe propaganda kuhusu Trump wakati wao wenyewe wanaweza kutumia akili zao kuelewa
 
Watu weusi wanajibagua wenyewe.
Kama unaambiwa ni mweusi wakati ni mweusi kweli, sasa umebaguliwaje hapo ?
Ulitaka uambiwe ni mtu mweupe ndio uone kuwa hujabaguliwa ?
Kwanini unaukataa ukweli kuwa wewe ni mtu mweusi ?

MKuu wtu weusi wana matatizo ya akili
 
Nitakueleza kwa kifupu kwa nini blacks ni kundi muhimu Marekani na kwa nini linazungumzwa sana.
Kwanza ni kundi la tatu kwa ukubwa baada ya White na Latinos ambao nyie wote hao wawili mnawaita wazungu tu.

Pili, Marekani inayong'aa sana imejengwa kwa sehemu kubwa na jasho la blacks waliotumikishwa mashambani, migodini na viwandani.

Tatu, sababu za blacks kuwa Marekani ni tofauti sana na makundi mengine, blacks walibebwa kwa nguvu kupelekwa Marekani tofauti na makundi mengine yote yaliyoenda kwa hiyari yao, wao wana haki kubwa zaidi ya kulalamika na kudai hali bora kuliko wengine wote.

Nne, ni historia ndefu ya utumwa iliyowaweka kwenye disadvantaged position kwa muda mrefu, Nafasi ya mtu mweusi Marekani ni muhimu sana kiasi kwamba vita vya wenyewe kwa wenyewe Marekani vilisababishwa na utumwa wa blacks.

Tano, blacks ndio wamekuwa wanaharakati wakubwa na chachu muhimu kwa makundi yote minority kupatiwa haki zao kama raia wa Marekani. Fursa wanazofurahia leo wanawake wa kizungu, wahindi, waislamu, mashoga n.k zilichochewa na zimetokana na harakati za nguvu za blacks,

Huwezi kulipuuza kundi la aina hii kama una akili.
 
Watu weusi wanajibagua wenyewe.
Kama unaambiwa ni mweusi wakati ni mweusi kweli, sasa umebaguliwaje hapo ?
Ulitaka uambiwe ni mtu mweupe ndio uone kuwa hujabaguliwa ?
Kwanini unaukataa ukweli kuwa wewe ni mtu mweusi ?
Trump anasema miaka yote Kamala alikuwa ni Mhindi ila all of a sudden kabadilika na kuwa mweusi
 
tujikite zaidi kwa alichokisema Trump.
ulichokieleza hapa hata jamii zingine ndani ya Marekani zinachakueleza kuhusu ushiriki wao katika Marekani.

iweje kabla ya Siasa huyu Mama alijibrand kama Muhindi ila kwenye Siasa anajitambulisha kama Mweusi?.
kwanini sasa na baada ya kuona nini hasa?.

nikisema kwamba: kusimama na brand yake ya Hawali kungelifungua Milango ya watu kuhoji UWEZO wake zaidi na sio ASILI nitakuwa nakosea?.

nikisema " sasa hivi anataka KURA tu, toka kundi la jamiii ya Tatu kwa ukubwa nitakuwa nimekosea?".

anajua uhindi wake aliokuwa anajibrand nao sio Dili kwa watu wa asili hiyo na hata kama ni Dini bado Wahindi ni jamii wa watu wachache zaidi,hawana impact yoyote kwenye Uchaguzi.

Marekani inahitaji mtu mwenye Uwezo, asili yake si kitu
 
Kamala Harris akiwa chuoni alikuwa mwanachama wa chama cha weusi cha Alpha Kappa Alpha sorority, akiwa seneta alikuwa ni member wa Congressional Black Caucus. Kamala hajawahi kuji brand muhindi, hakuna uthibitisho huo, hizo ni mojawapo ya kauli nyingi tu za kipuuzi za Trump.
 
Uislam mwema sana.

Mboora kati yao ni mcha Mungu.
Mcha Mungu ni Trump anayetaka kufuta ushoga na ndoa za jinsia moja ili kulienzi jina la bwana wetu Kristo aliye hai

Huyu Trump ni Mlokole hasa ndio maana alisema anashangaa kuona mataifa ya kiarabu miaka yote yanateseka kumpiga Myahudi kwani huko ni kupoteza muda tu!!!!! Israel itadumu milele na milele

Mungu mbariki Trump
 

Attachments

  • IMG_1340.jpeg
    877.3 KB · Views: 3
Nchi apewe tu trump hawa wahindi watajazana marekani bule bule na kuanza kutumikisha watu kama viwandani kama huku bongo
 
Trump sio mlokole, ameoa mara tatu na ametaliki mara mbili. Pia amekuwa na mahusiano ya kimapenzi na mcheza filamu za ngono akiwa kwenye ndoa.
 
hatuna shida na uAnachama wake wa Black caucus,kama tusivyo na shida na Weusi wa Baba yake.
race ya mtu is isiwe kigezo,weusi si kilema hata afikiliwe kwa jicho tatu kwasababu ya weusi wake.
 
Anawapiga porojo tu. Wote hao hali moja tu kuhusu ushetani. Hakuna mwenye afadhali hapo, si Trump si Kamala.
 
Naona hamuelewi kuwa Rais wa Marekani hapatikani kutokana na sanduku la wapoiga kura.

Hivi hamuelewi kuwa USA ni Republic?
Uongo!

Rais wa Marekani anapatikana kutoka kura za wapiga kura!
 
Watu weusi wanajibagua wenyewe.
Kama unaambiwa ni mweusi wakati ni mweusi kweli, sasa umebaguliwaje hapo ?
Ulitaka uambiwe ni mtu mweupe ndio uone kuwa hujabaguliwa ?
Kwanini unaukataa ukweli kuwa wewe ni mtu mweusi ?
Hata unachoandika wewe mwenyewe huelewi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…