Trump hatashinda japo na Kamala Harris hatauweza urais wa Marekani kipindi ambapo taifa hilo linadidimia

Trump hatashinda japo na Kamala Harris hatauweza urais wa Marekani kipindi ambapo taifa hilo linadidimia

Nafikiri wewe una matatizo mawili yanayokusumbua:-

1. Ujinga (Ignorance): kwamba hujui mfumo wa uchaguzi wa Marekani ulivyo.

2. Udini: kwamba ile kasumba ya kusujudia utamaduni wa kiarabu unakufanya uwe na msimamo huo ulionao kwa Marekani.

Lakini ukweli unabakia palepale kwamba hakuna uchaguzi duniani unaoheshimika kama uchaguzi wa Marekani na ndio tukio la pili linalotizamwa na watu wengi duniani baada ya kombe la dunia la kabumbu na hilo halina ubishi.

Huu mfumo wa uchaguzi tayari umeshadumu kwa zaidi ya karne mbili na uliwekwa ili rais aonekane kukubalika na watu wengi ktk kila jimbo na ndio maana mgombea anayeshinda kwa kupata kura nyingi katika jimbo basi huchukua Electoral College Votes zote za jimbo husika.

Kama utakuwa hujaelewa basi ni kwa sababu hizo hizo nilizo zitaja hapo juu 🖕

The Muslim American vote matters and it can no longer be taken for granted

Huenda leo ikawa mara ya mwisho asee kabla sijapotea kwa muda ntajitahidi kukujibu kabla sijapotea kwa muda

Kuikwepa Americant na system yao waloieka sio rahisi ingawaje watu wanapambania hilo

Nasababu kubwa nikwamba system inayotawala kwasasa duniani ambayo kiongozi mkubwa ni Americant ila inabeba wahusika wakubwa kama uk ger nk

Huo mfumo kuupita pia inahitaji mikakati mizito na kuja kutimia sio jambo la mara moja

Nikikwambia wafanye nini ntakua nakudanganya sababu inaweza ikawezekana ila isiwe rahisi mfumo ulioanza kujengwa miaka zaidi ya 70 sasa kuondolew ghafla

Napia china na russia au brics wanapambania hilo suala ila wao kama wao hawaelewani

Mfano india na china ila kama kungekua na mfumo thabiti baina ya china na india tu basi system nzima ya huo mfumo ungebadilika

China na india ndio mataifa pekee duniani kama yatakua na ajenda moja duniani wanaweza wakaifanya na ikafanikiwa ndani ya muda mfupi sana ila sharti wawe na maelewano mazuri kwa 100%✓ ila mpaka sasa hilo hawana

Haya mambo ya Geo politics pia sio yakuyaamini sanaa ndio maana licha yakua naongea mengi ila hua nna yangu kichwani hao marekani china russia nk sio wakuwaamini sana kwenye haya majambo

Unaweza ukakuta huku nje wanaugomvi mkubwa haswa ila huko nyuma wana ajenda moja ila wanaijua wenyewe

Dunia inaendeshwa na siri sana mzee tunayoyaona nje ni machache sana kati ya mengi yaliopo
Shukrani sana kwa muda wako kiongozi.

Kwenye upande wa ULIMWENGU kuendeshwa kwa Siri kubwa hapo ndo kuna msingi mkubwa wa swali langu. Of course niliuliza ili kukutega tu na umekuwa makini sana umeruka mtego. Salute sana🫡

Dunia imewekwa kwenye MATRIX, tunapangiwa vitu vya kujua na taarifa za kuzipata (wanao fanikiwa kutoka nje ya Matrix ni wachache sana na ndio ambao wanafanikiwa kuujua ukweli ambao upo nyuma ya pazia).

Andrew Tate na harakati zake za kutaka kuufungua ulimwengu unamcost, now wameshika mali zake zote na yeye mwenyewe.

They call it "THE CONSPIRACY OF EVERYTHING"

50% ULIMWENGU unalishwa taarifa za uongo kwa manufaa ya hao wakubwa.

So far uwe na wakati mwema mkuu 👏
 
Soma hapo juu Nyani Ngabu ameelezea vizuri. Itakuasaidia sana kuelewa Trump alishindaje uchaguzi
Wewe ndo u some VIZURI.

Wewe pamoja na huyo nani ngabu mnakiri kuwa popular votes hazichagui rais wa marekani jambo ambalo hata Mimi kwa kusoma vyanzo vya habari vya uhakika kama BBC najua Hilo kuwa popular votes hazichagui rais wa marekani na ndicho nilichomwambia mleta mada katika post yangu namba #30.
 
Kwamba watu 400+ ndio wanaweza ama wana haki ya kuthibitisha maamuzi ya watu zaidi ya 300M+ wao kama nani kuwazidi hao wengine Million walopiga kura?
Acha kudandia mambo yanayokuzid kimo, hujui chochote na hakuna kitu kibaya kama kujikweza unajua kumbe hujui kitu. Hao unaowaita 400+ bila shaka hujui wanapatikanaje!
Kama uingereza ile ndio imekufa kabisa kila angle Americant haijafika huko ila itafika nanatamani iwe chini ya kamala kama atashinda kura zao zamchongoma
Gharama ya ujinga ni mkubwa na kama taifa limejaa wajinga kama wewe, si ajabu yakatokea kama haya tunayoyashuhudia ya kijinga kama hapa kwetu.

Marekani (USA) ni nchi ya wahamiaji ambayo hadi sasa imefaulu kwa kiwango kikubwa kuishi pamoja duniani bila kujali tofauti zao kama rangi, dini, itikadi, kabila wala jinsia,

Marekani (USA) wapo binadamu kutoka bara zote duniani kuanzia Marekani kwenyewe, Ulaya, Asia na Afrika. Marekani ni jaribio (experiment) la binadamu tofauti kuishi pamoja.

Marekani kama jaribio (experiment) limefaulu kwa asilimia kubwa sana kuwaweka mamilioni ya binadamu waliozikimbia nchi zao wakisaka maisha bora ndani ya taifa hilo.

Wazungu kama Trump kwa mamilioni, Warusi kwa mamilioni. Wachina kwa mamilioni, Waafrika kwa mamilioni na Waarabu kwa mamilioni, wote wanaiita Marekani (USA) taifa lao.

Kwa sasa nitaachia hapo...!
 
Nimerejea tena hapa kukuelewesha kuhusu electoral votes.
Kwa kuwa umetumia mfano wa Hillary Clinton kushindwa na Trump kwenye uchaguzi wa mwaka 2016, basi ngoja nianzie hapo hapo.

Mara baada ya kura za jumla za wamerekani kupigwa (kabla ya kura za wajumbe kupigwa), na Hilary kuongoza kwa zaidi ya kura milioni mbili, alitangaza kushindwa na dunia nzima ikajua tayari Hilary ameshindwa. Kwanini atangaze kushindwa na kila mtu ajue Hilary ameshindwa wakati kura za wajumbe (electoral votes) zilikuwa bado hazijapigwa (zilikuja kupigwa wiki kadhaa baadaye)?
Jibu ni moja tu, kura za wajumbe ni kivuli cha taswira ya maamuzi ya mamilioni ya wamerekani waliyoyafanya kwenye sanduku la kura hapo kabla.

Kwa kumalizia tu, uchaguzi ule uliompa Trump ushindi ulitokana na ushindi wa Trump kupata kura nyingi zaidi kwenye majimbo muhimu yenye nguvu ya kuchangia ushindi wa kiti cha urais. Upigaji wa kura USA upo kimajimbo, na kila jimbo lina mchango wake tofauti na jimbo lingine. Ukielewa hili hauwezi kuja kubisha tena.
Kwa maelezo yako mwenyewe ni ngumu kiasi gani kwako kukiri kuwa popular votes marekani haziamui nani awe raisi?
 
Nimekuelewa sana pia

Sasa kwanini matokeo ya mwisho tu kwamba Hillary alimshinda DT kwa kura nyingi yasiwe final say kwamba Hillary aingie ikulu

Kama kweli kura zawananchi pekee zatosha kua mwamuzi
Kura za jumla jumla zinaweza kuwa na Upendeleo, zinaweza zisiwe na picha nzima ya kuwakilisha wamerekani kutoka katika majimbo yote 50+.

Kumbuka ili uwe Rais wa USA unatakiwa uwe unakubalika kwenye majimbo mengi zaidi miongoni mwa majimbo yote (vinchi 50) ndani ya USA, hivyo mtu anaweza akapata kura zote za jimbo moja kubwa (labda kura milioni 10) lakini akakosa kura zote za majimbo mengine matano (labda yana jumla ya kura milioni 8). Matokeo katika majimbo sita yataonyesha ameshinda kura milioni 10 dhidi ya kura milioni 8, lakini ukichambua hicho kitu utagundua atakuwa amechaguliwa na jimbo moja na kukataliwa katika majimbo sita. Ni vipi awe rais wa USA?
 
Hiyo ni kwa sababu ya idadi ya watu waliopo kwenye majimbo.

Majimbo yenye watu/wakazi wengi, electoral college votes zake nazo ni nyingi.

Electoral college votes zinatolewa kulingana na idadi ya wabunge waliopo kwenye chemba mbili za bunge la Marekani: senate na House of Representatives.

Kila jimbo lina maseneta wawili. Hiyo ni bila kujalisha idadi ya watu waliopo kwenye majimbo.

Marekani kuna majimbo 50, hivyo ina maseneta 100.

Kwenye House of Representatives ndo idadi ya wawakilishi hutokana na idadi ya watu/ wakazi waliopo kwenye majimbo wanayoyawakilisha.

Kwa mfano, jimbo la Florida lina wawakilishi 28 kwenye House of Representatives.

Kwa hiyo, kwenye electoral college votes, linazo 30.

Hiyo 30 inatokana na hao wawakilishi 28 ukijumlisha na maseneta wake wawili [2].

Mfano mwingine:

Jimbo la Georgia lina wawakilishi 14 kwenye House of Representatives.

Kwa hiyo kwenye electoral college votes, Georgia inazo 16.

14 kutokana na hao wawakilishi 14 ukijumlisha na maseneta wake wawili [2].

Ili mgombea urais aweze kuzipata electoral college votes za jimbo, ni lazima ashinde popular votes za jimbo.

Iko hivyo kwenye majimbo 48. Majimbo ya Nebraska na Maine, yenyewe huzigawa votes zake kutokana na congressional districts.

Marekani uchaguzi huendeshwa na majimbo. Kila jimbo lina sheria zake za uchaguzi.

Kwa hiyo, Marekani hakuna uchaguzi wa kitaifa.

Chaguzi zilizopo ni za kimajimbo.

Na ndo moja ya sababu kwa nini national popular votes haziamui mshindi wa urais.

Lakini huwezi kushinda electoral college votes bila ya kushinda state popular votes.

Cha msingi ukitaka kuelewa vizuri, ielewe tofauti ya state popular vote [ambayo ndo inatoa electoral college votes] na national popular vote ambayo haitumiki kuamua mshindi.
Nimekuelewa vizuri sana mkuu, Kumbe ndio maana huwa kuna majimbo yanagombaniwa sana kumbe sababu ni hiyo,

Utaratibu mzuri sana
 
Kwa maelezo yako mwenyewe ni ngumu kiasi gani kwako kukiri kuwa popular votes marekani haziamui nani awe raisi?
Mimi nimesema Electoral college votes(kura za wajumbe) ni hitimisho la maamuzi ya Popular votes (kura za wananchi wote). Popular votes ndio huzaa electoral college votes.
Na ndio maana nikakwambia kabla ya kupigwa kura za Popular votes hakuna anayejua mshindi ni nani, lakini baada ya kupigwa kura za popular votes kila mtu anamjua mshindi, na hakuna anayewaza tena mshindi kuja kupatikana kupitia Electoral college votes ambayo huja kupigwa wiki kadhaa huko baadaye.

Mwisho kabisa kwanini hujiulizi wagombea wanatumia muda mwingi, pesa na mbinu mbalimbali kupiga kampeni USA kuwafikia mamilioni ya wamerekani ili kupigiwa kura za Popular votes badala ya kwenda kuwasaka hao wajumbe 400 wa Electoral college votes ikiwa kura za hao wajumbe ndio huamua rais wa USA?
 
wewe na Nyani Ngabu nimewaelewa sana, asante

Wewe sasa ndio unaweza ukawa hunielewi nasidhanii kama hii hoja unanielewa

Kinachoendelea marekani ndio kama kinachoendelea uk wanadanganya watu malkia sijui mfalme sio mwanasiasa wakati huo huo ili uwe PM lazima ipite idhini yake

Moja ya points kubwa inayopewa jimbo fulani kua na nguvu ni uwingi wawatu

Kwanini wapiga kura wasitoshe kua waamuzi wamwisho

Mwisho umerudi pale pale kwenye points yaani mtu anazidi kwakura 2M bado anatangaza kushindwa

Kura zawananchi haziheshimiwi na Hillary alikiri sababu system ishaekwa walivyoamua kuieka lazima ifuatwe Hillary lazima angekiri

Ila ukweli hauondoki wala kubadilika kama maamuzi ya raia zaidi ya 2M hayajaheshimiwa

Huu ukweli hata muupake rangi vipi hauwezi kubadilika wazeee
Nadhani huenda hautaelewa tena kuhusu hili ikiwa tumekuelewesha mpaka basi. Nenda katazame hizo kura milioni mbili za zaidi alizopata Hillary zimetokea wapi halafu nenda kawaze Rais wa USA anachaguliwa na wamerekani kutokea majimbo 52. Halafu njoo tujadili upya.
 
Mimi nimesema Electoral college votes(kura za wajumbe) ni hitimisho la maamuzi ya Popular votes (kura za wananchi wote). Popular votes ndio huzaa electoral college votes.
Na ndio maana nikakwambia kabla ya kupigwa kura za Popular votes hakuna anayejua mshindi ni nani, lakini baada ya kupigwa kura za popular votes kila mtu anamjua mshindi, na hakuna anayewaza tena mshindi kuja kupatikana kupitia Electoral college votes ambayo huja kupigwa wiki kadhaa huko baadaye.

Mwisho kabisa kwanini hujiulizi wagombea wanatumia muda mwingi, pesa na mbinu mbalimbali kupiga kampeni USA kuwafikia mamilioni ya wamerekani ili kupigiwa kura za Popular votes badala ya kwenda kuwasaka hao wajumbe 400 wa Electoral college votes ikiwa kura za hao wajumbe ndio huamua rais wa USA?
Huo ndo utaratibu waliojiwekea usiumize sana kichwa
 
Baada ya kufuatilia kwa makini mkutano mkuu wa Democratic na kampeni za Donald Trump nimegundua kwamba Trump hatoweza tena kamwe kuupata uraisi wa Marekani anaoutamani.
Historia ya maisha yake ya kihuni na kupenda ubaguzi pamoja na uadui kwa waislamu hautamuwezesha Donald Trump kurudia kwenye kiti cha uraisi.Wamarekani wanaompinga wakiwemo wa rangi mbali mbali na wahamiajia hawatampigia kura kabisa.
Trump atabaki na kundi la wabaguzi wa rangi ambao hawatotosha kumpatia kura za uraisi.
Kwa maana hiyo Kamalla Harris ndiye atakayekuwa mshindi wa kiti hicho,kwanza kwa vile ni mwanamke na enzi hizi wanawake ni wengi sana kwenye chaguzi za mataifa mengi na ni rahisi kushawishika na vitu ambavyo si rahisi kuwapata wanaume.
Vile vile Kamalla ni Mmarekani mwenye asili ya nje ambapo katika Marekani idadi ya watu hao ni wengi sana.Waliotokea Afrika,America kusini,China na bara hindi.Wote hao ni wapiga kura wake.
Wapiga kura waislamu japo sio wengi lakini wote pamoja na matatizo ya viongozi wa Democratic akiwemo raisi wa sasa Biden kujipendekeza kwa mayahudi,pamoja na hivyo Trump anaonekana ni hatari zaidi kwao kuliko Kamalla.
Tukija upande wa Kamalla ambaye ana asilimia kubwa za kushinda.Jee atauweza uraisi huo wakati taifa hilo liko kwenye hali mbaya za kiuchumi na liko mbioni kuzama .Uadui na mataifa makubwa kama Urusi na China pamoja na vita vya Gaza ni majukumu ambayo huwa ni mazito kwa raisi mwanamke.
Kwa namna yoyote ile kinachoendelea kwa Marekani kwa sasa ni tope ambalo hatimaye litaizamisha na kuwa nafuu kwa dunia nzima baada ya taifa hilo kufanya jeuri na kufuru kwa muda mrefu duniani.
Marekani kuwa kwenye mbaya ya kiuchumi umeitoa wapi?
 
Nadhani huenda hautaelewa tena kuhusu hili ikiwa tumekuelewesha mpaka basi. Nenda katazame hizo kura milioni mbili za zaidi alizopata Hillary zimetokea wapi halafu nenda kawaze Rais wa USA anachaguliwa na wamerekani kutokea majimbo 52. Halafu njoo tujadili upya.
Majimbo 52 Marekani? Yamekuwa 52 toka lini?
 
Nikikwambia kama wewe miongoni mwa hao wajinga unabisha

Nyie msiokua waislamu sasa ndio mnaofuata tamaduni za kijinga zajiarabu

Sababu utamaduni wakiarabu unajuulikanwa tokea enzi na zama kua unaabudia na kufuata ujinga mnaofata nyie wakuabudia masanamu na mambo mengine maovu

Uislamu ndio ulikuja kuwafunza waarabu dini na sio kinyume chake kama mnavyomezeshwa huko kanisani

Nikikwambia kua una ujinga na hujui mambo uwe unaelewa

Huwezi utenganisha Uislam na uarabu.
Uislam NI uarabu lakini Uarabu siô Uislam.

Yàani uarabu umezaa Uislam ila Uislam Kamwe hauwezi kuzaa Uarabu.

Mtu anayetenga Uislam na uarabu NI mtu àmbaye aidha hajui Uislam ni nini au ameamua makusudi kabisa kudanganya Akili Yake.

Bila Uarabu Hakuna Uislam
 
Hao Mia tano wanapatikanaje , Ushawaji jiuliza hilo?
Kamala huenda historia ikaja kumuandika kama ndie rahisi alofiwa na Americant mikononimwe

Ila usilolijua ama umelisahau nikwamba kura za marekani hazichaguliwi na raia wamarekani kama ulivyoandika hapo

Wamarekani zaidi ya 200M+ sijui 300M+ wanachaguliwa ama wanateuliwa rais wao na kakikundi chawatu tu hawazidi hata mia nne(400) sijui mia tano (500)

Moja ya nchi inayotakiwa kufunzwa kuhisiana na demokrasia basi marekani inatakiwa iende ikajifunze demokrasia hata kwa Zimbabwe au Venezuela
 
Baada ya kufuatilia kwa makini mkutano mkuu wa Democratic na kampeni za Donald Trump nimegundua kwamba Trump hatoweza tena kamwe kuupata uraisi wa Marekani anaoutamani.
Historia ya maisha yake ya kihuni na kupenda ubaguzi pamoja na uadui kwa waislamu hautamuwezesha Donald Trump kurudia kwenye kiti cha uraisi.Wamarekani wanaompinga wakiwemo wa rangi mbali mbali na wahamiajia hawatampigia kura kabisa.
Trump atabaki na kundi la wabaguzi wa rangi ambao hawatotosha kumpatia kura za uraisi.
Kwa maana hiyo Kamalla Harris ndiye atakayekuwa mshindi wa kiti hicho,kwanza kwa vile ni mwanamke na enzi hizi wanawake ni wengi sana kwenye chaguzi za mataifa mengi na ni rahisi kushawishika na vitu ambavyo si rahisi kuwapata wanaume.
Vile vile Kamalla ni Mmarekani mwenye asili ya nje ambapo katika Marekani idadi ya watu hao ni wengi sana.Waliotokea Afrika,America kusini,China na bara hindi.Wote hao ni wapiga kura wake.
Wapiga kura waislamu japo sio wengi lakini wote pamoja na matatizo ya viongozi wa Democratic akiwemo raisi wa sasa Biden kujipendekeza kwa mayahudi,pamoja na hivyo Trump anaonekana ni hatari zaidi kwao kuliko Kamalla.
Tukija upande wa Kamalla ambaye ana asilimia kubwa za kushinda.Jee atauweza uraisi huo wakati taifa hilo liko kwenye hali mbaya za kiuchumi na liko mbioni kuzama .Uadui na mataifa makubwa kama Urusi na China pamoja na vita vya Gaza ni majukumu ambayo huwa ni mazito kwa raisi mwanamke.
Kwa namna yoyote ile kinachoendelea kwa Marekani kwa sasa ni tope ambalo hatimaye litaizamisha na kuwa nafuu kwa dunia nzima baada ya taifa hilo kufanya jeuri na kufuru kwa muda mrefu duniani.
Wewe utakuwa mwana CCM, maana unafikiri Wamerika wapumbavu. Wenzako wanafanya uchaguzi wa haki na unaojali wapiga kura wanachokitaka
 
Wewe utakuwa mwana CCM, maana unafikiri Wamerika wapumbavu. Wenzako wanafanya uchaguzi wa haki na unaojali wapiga kura wanachokitaka
Usisahau kuwa hilo taifa lipo kwenye dimbwi la matope.Kila wanakoelekea wanajitapakazia mtindo mmoja.
Uchaguzi wa mwaka huu ndio utakaondika historia ya kuanguka kwa Marekani.
 
Baada ya kufuatilia kwa makini mkutano mkuu wa Democratic na kampeni za Donald Trump nimegundua kwamba Trump hatoweza tena kamwe kuupata uraisi wa Marekani anaoutamani.
Historia ya maisha yake ya kihuni na kupenda ubaguzi pamoja na uadui kwa waislamu hautamuwezesha Donald Trump kurudia kwenye kiti cha uraisi.Wamarekani wanaompinga wakiwemo wa rangi mbali mbali na wahamiajia hawatampigia kura kabisa.
Trump atabaki na kundi la wabaguzi wa rangi ambao hawatotosha kumpatia kura za uraisi.
Kwa maana hiyo Kamalla Harris ndiye atakayekuwa mshindi wa kiti hicho,kwanza kwa vile ni mwanamke na enzi hizi wanawake ni wengi sana kwenye chaguzi za mataifa mengi na ni rahisi kushawishika na vitu ambavyo si rahisi kuwapata wanaume.
Vile vile Kamalla ni Mmarekani mwenye asili ya nje ambapo katika Marekani idadi ya watu hao ni wengi sana.Waliotokea Afrika,America kusini,China na bara hindi.Wote hao ni wapiga kura wake.
Wapiga kura waislamu japo sio wengi lakini wote pamoja na matatizo ya viongozi wa Democratic akiwemo raisi wa sasa Biden kujipendekeza kwa mayahudi,pamoja na hivyo Trump anaonekana ni hatari zaidi kwao kuliko Kamalla.
Tukija upande wa Kamalla ambaye ana asilimia kubwa za kushinda.Jee atauweza uraisi huo wakati taifa hilo liko kwenye hali mbaya za kiuchumi na liko mbioni kuzama .Uadui na mataifa makubwa kama Urusi na China pamoja na vita vya Gaza ni majukumu ambayo huwa ni mazito kwa raisi mwanamke.
Kwa namna yoyote ile kinachoendelea kwa Marekani kwa sasa ni tope ambalo hatimaye litaizamisha na kuwa nafuu kwa dunia nzima baada ya taifa hilo kufanya jeuri na kufuru kwa muda mrefu duniani.
Asante kwa uzi,hizo siasa za ubaguzi na kuitenga Marekani na jumuia za kimataifa ndiyo zilizompa uraisi Trump kwenye ule uchaguzi aliopita,halafu hiyo point ya mwisho hapo uliyoielezea kuhusu udhaifu wa raisi mwanamke kwenye siasa za dunia ambazo kwa sasa zimegubikwa na vita na migogoro mikubwa isioisha,zilimuangusha pia Hilary Clinton na Trump akapeta,Marekani bado haipo tayari kutawaliwa na raisi mwanamke,Kuna undi kubwa la wapiga kura ambao wana hiyo mentality ya kutaka Marekani iendelee kuwa mbabe duniani wanahitaji Kiongizi kama Trump,kwa Mimi binafsi na uzoefu wangu wa kufuatilia chaguzi mbalimbali duniani,namuona Trump akirejea madarakani na Chama chake cha Republican,japo hayo siyo matarajio ya watu waliowengi duniani.
 
Back
Top Bottom