Bwana Utam
JF-Expert Member
- Feb 15, 2016
- 19,559
- 36,514
Naomba nikujibu sasa walau kwauchache kiongoziMkuu hongereni kwa mjadala huu, nimekuwa msomaji wa baadhi ya threads na mara kadhaa kwenye issue za siasa huwa naona upo active.
Nina swali ila linaweza kuwa nje ya discussion (hayo mengine sipo interested sana hususani watu kuchagua sides, napenda tu kupitia pitia)
Hivi ni kwanini unawachukia sana US? Ni mara kadhaa nimeona unawapiga vita sana na kuonyesha hasira kwa mtu yeyote ambaye anazungumzia ishu yoyote chanya kuhusu US as compared to Russia?
Reason behind ni ipi?
Hii sio personal mkuu, natamani kujua huenda kuna kitu nitajifunza
Kama nlivyokuelezea pale juu palipopita
Sio kwamba naichukia sana Us nakuipenda sana Russia
Ila naamua kusema ukweli siungi mkono kwa 100%✓ anayofanya Russia sehemu mbali mbali ila siungi mkono kwa 90%✓ yanayofanywa na west wakiongozwa na marekani
Marekani ni mzandiki mnafiq muongo na muharibifu mfano marekani kaharibu sehemu mbali mbali duniani kwakuzivamia akiongozana na shoga zake wa west (namlaumu marekani zaidi sababu sehemu zilizoharibiwa na nato na jamaa zake marekani angekua hataki pasingeharibiwa/ka) ila paliharibika kwabaraka zake
Unafiq marekani anakuja huku anatwambia demokrasia ndio anayoipigania akaenda akavamia libya akaua watu huku yeye ndio anakumbatia madikteta ambao hawana demokrasia tukianzia cameroon tukija mido ist kote marekani kakumbatia madikteta maadam tu wanaunga mkono maslahi yake
Ushenzi marekani kupitia yeye na mashoga zake wanaunga mkono tabia mbaya na zakishenzi mfano kuua watu kupitia vikwazo mfano venezuela na cuba watu wanakufa na kukimbia nchi zao shauri za vikwazo vya kishenzi na kinyonyaji vya marekani sababu tu hawaungani nae kwenye mambo yake bila kusahau zimbabwe
Hila na uzandiki marekani alitaka kuingia vitani na USSR sababu tu walitaka kupeleka makombora ya nyuklia pale cuba ila wakati huo huo yeye anaona sawa kuizunguka russia nakueka aloyakataa yeye kufanyika cuba (sioni sawa russia kuua watu ukraine ila naunga mkono sababu madai aloyapinga marekani cuba ndio anayoyafanya russia ukraine ila ukweli nikwamba Russia anaionea na kuua watu ukraine vita ya russia kwa Ukraine sio halali )
Kwauchache nihaya ingawa yapo mengi sana ila ukweli siungi mkono mambo mengi ya marekani sababu ya ushenzi na ubaya wao kiukweli marekani kwa dunia hii wana mabaya mengi kuliko mazuri nanimejitahidi kutaja madhila na madhara walopeleka kwenye nataifa mengi nimeyataja ya majority ya kikristo ili uzi wangu suije fungamanishwa na dini maana watu hawachelewi hapa jukwaani
Ahsante MKUU