Trump kamuonya Ayatola ataingia kuwanusuru raia kama ataendelea kuwaua

Trump kamuonya Ayatola ataingia kuwanusuru raia kama ataendelea kuwaua

wanatafuta nini?
Nishati,walimtoa shah baada ya kuwataka walipe mirabaha stahiki kwenye mafuta,wakamtumia ayatollah Khomeini wakaingia nae mikataba kuwa akiingia watanyonya
Ayatollah alivyoingia akawaruka, mbaya zaidi akatangaza vita kwa USA na Israel
Leo Iran kagundua futa jingine,gesi ya kumwaga na rare Earth's za kutosha
Wameongeza vikwazo miezi miwili mitatu iliyopita,vimeanzw kung'ata,wametumia watu wao ndani ya Iran kuanzisha hili,punde tu raia watafumuliwa vichwa mbaya
 
Maandamano wameinjinia wenyewe hao huu ndio mfupa mgumu Kwa Westerners Ayatollah washamshindwa wamebaki kulia lia tu, yule sio mtu wa kupiga piga magoti
Inawezekanaje marekani ashawishi watu wote hao kuandamana?wameingiaje hapo iran,intelegensia ya Iran ilikua wapi?
Kama hilo linawezekana,tukiri USA ni level nyingine kabisa,sio wa kucheza nae kabisa 🙌
 
Hakuna ujuacho. Mambo ni magumu sana Iran kwa sasa. Mfumko wa bei ndani ya miezi 2, umefikia 100%. Wairan kwa sasa 50% wanaishi chini ya mstari wa umaskini.
Halafu serikali yao inawezekeza kwa vikundi vya kigaidi na kuunda masilaha ya nuclear.

Ni kama serikali ya ccm, huduma kwa raia ni mbovu halafu wananunua magoli kwa milioni 100.
 
Back
Top Bottom