Trump kawadhalilisha wayahudi wa Tandale

6 Pack

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2022
Posts
3,952
Reaction score
8,807
Niaje waungwana

Mimi ni miongoni mwa watu wachache wenye uwezo wa kuongea ukweli, hata kama ukweli huo utakubaliwa na wachache na kukataliwa na wengi.

Kwa wakongwe wa jukwaa hili la mambo ya kimataifa haswa kuhusu mambo ya Iran, Israel, Marekani nk nafikiri mnanifahamu vizuri kwenye uchambuzi murua wenye ukweli na uhakika.

Miaka mitatu au minne iliyopita niliwahi kuzungumzia nguvu na uwezo mkubwa wa kijeshi iliyonayo Iran. Na ninakasema kwamba pamoja na nchi hiyo kuwa na vikwazo vikubwa vya kiuchumi, na kijeshi vilivyodumu kwa zaidi ya miaka 50, lkn nchi hiyo imekuwa na uwezo mkubwa mno wa kijeshi kuliko nchi nyingi ambazo hazina vikwazo ikiwemo Israel (inayotegemea silaha kutoka Marekani), zingine ni Saudi Arabia, Jordan nk. Wenye akili timamu walikubaliana na mimi, ila wale ambao waliozoea kulishwa matango pori walibisha kwamba Iran haina silaha wala nguvu yoyote ya kijeshi kama ninavyosema.

Mungu si athumani tukaja kushuhudia vita ya Iran na Israel mara mbili, ambapo mara zote Israel ilionekana kuchakazwa vibaya sana, na mifumo yake ya ulinzi THAAD, Iron Dome nk kuchanwa chanwa kama tambala bovu.

Baada ya hapo Israel ikaanza kuiogopa Iran na kuamua kuidondokea Marekani imsaidie kupambana na Iran. Hata hivyo Marekani imeonekana kugwaya baada ya kugundua kwamba Iran ina makombora ambayo yanaweza kupiga nchi yoyote ya Ulaya na Marekani kwa ujumla.

Ndiomaana Trump alipoomba Uingereza impe kisiwa chake ili akitumie kwa ajili ya kupambana na Iran, Muingereza aliogopa na kumtolea nje Trump, cause wanamjua vizuri Ayatollah Khomeini huwa hana muda wa kucheka na kima. Wewe ukiweka ugoko yeye anaponda na jiwe tu 🤣🤣🤣🤣🤣

Trump anasema sasa Iran wameunda makombora ambayo yanaweza kufika katika Jimbo lolote la Marekani. Hii ni kwa mujibu wa Trump mwenyewe alipokuwa akihutubia bungeni.

Hii kauli ya Trump kwamba kwa sasa Iran ina makombora ya kupiga nchi yoyote ya Ulaya na Marekani kwa ujumla inaonekana imepiga kwenye mshono wa wayahudi wa Tandale ambao hawakupenda kabisa Dunia iujue ukubwa wa nguvu za Iran daima.

Imagine hiyo miaka 50 Iran ingekuwa haina vikwazo vya silaha na uchumi kama Israel, leo hii ingekuwa na silaha za namna gani na uwezo wa aina gani kijeshi!
 
Jidanganye. Hapo mwana anatafuta justification tu toka congress ili ayatollah awahishwe kwa bikra 72.
Mbona kwa Maduro hakuitafuta hiyo justification?

Wewe endelea kuteseka, mwenzako Netanyahu alienda Marekani zaidi ya mara 8 kuomba asaidiwe baada ya yeye mwenyewe na genge lake kumshindwa Ayatollah.
 
Mbona hawajayatumia kupiga Israeli wakarusha rasharasha zilizooshwa juu kwa juu, inaonekana humjui Trump kijana
 
Mbona hawajayatumia kupiga Israeli wakarusha rasharasha zilizooshwa juu kwa juu, inaonekana humjui Trump kijana
Rasha rasha zilizooshwa jujuu!!!

Ndiomaana nikasema wenye akili timamu tu ndo huelewa nlichoandika.

Hebu muangalie Netanyahu wa kabla ya vita.

Na Netanyahu wa wakati wa vita ili uone ni jinsi gani Netanyahu mwenyewe alikuwa halali, hapigi mswaki wala kula.

Vita ya siku 12 tu, mtu kapururuka namna hiyo. Je ngoma ingeenda miezi?

Hapo nimeshaona ni kwanini alimwambia Trump aombe vita isimame 🤣🤣🤣

Na hapo Iran walitumia makombora ya zamani ambayo huwa wanawapa houth bure waihenyeshe Israel kwao 🤣🤣🤣

Trump ataishia kuwa mwamba kwa Maduro tu, lkn sio kwa Ayatollah.. NEVER
 
Ushasema vita wewe ungekuwa vitani ungelala? Hii mbona ni common sense tu? Wakati wa vita vya Kagera (km ulikuwepo) Nyerere alikua analala? Watoto wa kisasa kila kitu hadi mkadese?
 
Ushasema vita wewe ungekuwa vitani ungelala? Hii mbona ni common sense tu? Wakati wa vita vya Kagera (km ulikuwepo) Nyerere alikua analala? Watoto wa kisasa kila kitu hadi mkadese?
Wewe si ulisema zilikuwa rasha rasha zilizooshwa hewani, sasa huo usingizi ulikosekanaje?

Mbona Ayatollah au Putin hawakuwahi kuwa namna hii?
 
Vita ni vita mura hata kama adui ana manati hutarara hata hapo mtaani kwako kijana ni common sense tu, ayatolah hana hizo silaha na Trump anamzuga tu akae uchi na kasema anatengeneza hizo silaha so kama ni kweli zipo kwnye process, angekuwa nazo wala asingemuacha muyahudi aue majenerali wake na wakuu wa hamas ndani ya ikulu yake, period
 
Tatizo lenu ninyi Mazuzu hamjui Geopolitics!! Hata Dikteta Saddam Hussein aliambiwa ana silaha za maangamizi ili tu kuhalalisha kipigo kwake.

Hata waswahili husemi ukitaka mbwa apigwe wewe mpe jina baya atapigwa mtaa mzima.

Wajinga kama ninyi hamjui Geopolitics ndiyo maana mnabwabwaja sana kama Mazuzu!!
 
Huu ndiyo Ujinga mkubwa walionao Wafuga Midevu na Majini wanapenda sana sifa na kujisifia wao wenyewe. Huenda waliondoka a na ujinga kama huu huenda wakawa nao watu!!
Miaka mitatu au minne iliyopita niliwahi kuzungumzia nguvu na uwezo mkubwa wa kijeshi iliyonayo Iran. Na ninakasema kwamba pamoja na nchi hiyo kuwa na vikwazo vikubwa vya kiuchumi, na kijeshi vilivyodumu kwa zaidi ya miaka 50,
Jamhuri ya kiislamu ya Iran ilianzishwa 1979 na Ayatollah Khomen miaka 47 iliyopita sasa hiyo miaka zaidi ya 50 unayoisema bwege wewe umeitoa wapi? Au ndivyo mnavyofundishwa kwenye Madrasa yenu??
IDF huwezi kulinganisha na IRGC ya Iran kwenye vita vya siku 12 Iran ilipoteza watu zaidi ya 1,000 wakiwemo Makamanda waandamizi na Mkuu wa Majeshi ya Iran. Hawa kuweza kuangusha hata ndege-vita ya Israel hata moja na hawakuua Askari yeyote wa Israel.
 

Attachments

  • IMG_3499.jpeg
    132.9 KB · Views: 34
  • IMG_3483.jpeg
    59.3 KB · Views: 28
  • IMG_3479.jpeg
    351.6 KB · Views: 33
  • IMG_3466.jpeg
    339.2 KB · Views: 37
  • IMG_3419.jpeg
    35.8 KB · Views: 34
  • IMG_3414.jpeg
    197.7 KB · Views: 31
  • IMG_3406.jpeg
    68.7 KB · Views: 38
  • IMG_3405.jpeg
    65.3 KB · Views: 38
  • IMG_3404.jpeg
    72.7 KB · Views: 37
  • IMG_3403.jpeg
    130 KB · Views: 35
  • IMG_3402.jpeg
    112.9 KB · Views: 33
  • IMG_3401.jpeg
    59.9 KB · Views: 28
  • IMG_3366.jpeg
    347.7 KB · Views: 35
Unaamini anacho SEMA trump? Bro HIZO ni akili zavita, JAMAA anatafuta kuungwa mkono isionekane anamuonea, UKITAKA KUMUUA mbwa mpe JINA BAYA, vita inapiganwa kisasa MKUU, Kuna MTU ananyongonyeshwa hapo
 
Mbona unapayuka kama kuku aliekatwa kichwa!!

Sadam hakuwai kurusha hata jiwe Israel, lkn Iran imerusha makombora na kuiponda ponda Israel hadi Netanyahu akawa analala handakini kama panya.

Sadam hakuwa kuwa na silaha yoyote zaidi ya skadi, Iran ana makombora hatari ulimwenguni, na baadhi ya makombora hayo amewapa vijana wake Houth wayavurumishe Israel anytime na kufunga njia ya bahari muda wanaojisikia.

Hapo sijazungumzia drone zake ambazo zimebadilisha uelekeo wa vita ya urusi kule Ukraine na kusababisha raisi wa Ukraine aishi kwa mashaka na wasi wasi mkubwa.

Mwaka 2019 Marekani iliwahi kutumia drone hatari ya udukuzi yenye uwezo wa kuingia katika nchi kudukua bila kuonekana wala kujulikana. Lakini ilipoingia tu anga la Iran ilishushwa (dunguliwa) muda huo huo.

Sasa unapoona Netanyahu kila siku anakwenda Marekani na kurudi kama mtu alieshikwa na tumbo la kuhara na choo, ujue anakuwa anatambua nguvu za Iran na hivyo anaogopa kum face mwenyewe mpaka apate usaidizi kutokana nje ambao hata hivyo wote wawili Marekani na Israel watashindwa.

Mark my words 🤞
 
Unaamini anacho SEMA trump? Bro HIZO ni akili zavita, JAMAA anatafuta kuungwa mkono isionekane anamuonea, UKITAKA KUMUUA mbwa mpe JINA BAYA, vita inapiganwa kisasa MKUU, Kuna MTU ananyongonyeshwa hapo
Ile ilikuwa ambush. Kuna tofauti ya ambush na vita ya moja kwa moja.

Leo hii mtu akikupiga kisu ukiwa umelala au umekaa sehemu, hiyo haimaanishi kwamba mtu huyo ana nguvu kushinda wewe.

Tumia akili kujadili hoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…