Trump kusimamisha misaada duniani ni kosa kubwa la kiufundi. Ni muda wa China na Urusi kuja kutufariji Waafrika

Unajidanganya sana kama unadhani hatuendelei kwa sababu tunapewa misaada.

Israel na Egypt ni nchi zilizoendelea sana lakini bado zinapokea misaada.

Kusema kwamba hatuendelei kwa sababu tunapokea misaada ni ukichaa
 
Wamarekani weusi wa Ifakara na Tandahimba si kila siku hua wanasema humu kua US inaendeshwa na mfumo na sio Rais?

Trump kaingia tu kaifungulia Tik tok,kakata misaada,anataka kukata Birthright citizenship,na mabadiliko kibao.
 
Urudi ya sasa sio USSR, hivo Haina Hela .

Uchina ? Hawez .

Kwa Ufupi safari hii maji yataitwa Mma.
 
Mmalize pesa na rasilimali zenu kwa rushwa na ufisadi halafu mumlaumu Trump
 
Wewe ambaye akili yako iko spoiled na utawala wa kishenzi wa fisiemu unapata wapi guts za kukosoa rais pekee wa Marekani aliyeweza kukutana na Rais wa North korea.

Donald Trump is way smarter than all African presidents combined.
 
Mmalize pesa na rasilimali zenu kwa rushwa na ufisadi halafu mumlaumu Trump

What part of my piece imemlaumu Trump kwa rushwa zinazoendelea Tanzania?

Umesoma nilichoandika?

Na ni wapi Trump amesema amesitisha misaada kwa sababu ya uwepo wa rushwa?
 
Ana deal na undocumented na sio documented.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Akili za hovyo, eti wakati wa china kutufariji waafrika! Kwani mna matatizo gani hadi mfarijiwe? Hamna akili za kujitegemea? Mbonà marekani wanajitegemea? Mkitukanwa ni sawa tuu.
 
Wewe ambaye akili yako iko spoiled na utawala wa kishenzi wa fisiemu unapata wapi guts za kukosoa rais pekee wa Marekani aliyeweza kukutana na Rais wa North korea.

Donald Trump is way smarter than all African presidents combined.

Sawa Mmarekani wa Buza kwa mama kibonge.

Siku ukisikia ARV zimekatwa bongo usije ukatuanzishia uzi kulalamika
 
Wanaopiga kelele wengi ni wale wafanyakazi wanaotarajia mapesa yaingie kutokea marekani , trump toka akiwa Rais awamu yake ya kwanza alisema wazi misaada kwa waafrika inawalemaza akili huku wakilalia rasilimali lukuki, Russia Hana uwezo wa kutoa misaada itakayolingana na misaada ya marekani labda misaada ya kijeshi. Tujifunze kujitegemea anayekupa msaada ameamua hakupi tena na wala haikua haki Sisi kupewa misaada hiyo hivo tukae kwa kutulia
 
What part of my piece imemlaumu Trump kwa rushwa zinazoendelea Tanzania?

Umesoma nilichoandika?

Na ni wapi Trump amesema amesitisha misaada kwa sababu ya uwepo wa rushwa?
Trump akiendelea na sera yake hii, ataua kabisa significance ya Marekani Afrika meanwhile Uchina na Urusi wakiwa busy kusaka influence yetu.
Mkuu, Marekani hata afanye kitu gani hawezi shushwa significance yake na hizo nchi umeandika hapo. Sio Africa tu.
 
Nakuunga mkono ila shida ni hii mkuu, HATUWEZI KUJITEGEMEA na tangu Afrika iwepo HATUJAWAHI KUJITEGEMEA.

Unaiambiaje nchi ambayo hata toothpick inaleta kutoka nje ianze KUJITEGEMEA?
Huu ujinga kwamba toothpick ni big deal aliuanzisha nani ?
Nchi imejaa viwanda kibao vinavyotengeneza muhimu, nyie mnakuja na comedy zenu za toothpick
 
Wamarekani weusi wa Ifakara na Tandahimba si kila siku hua wanasema humu kua US inaendeshwa na mfumo na sio Rais?

Trump kaingia tu kaifungulia Tik tok,kakata misaada,anataka kukata Birthright citizenship,na mabadiliko kibao.
Marufuku kuitolea Ifakara mifano ya kijinga.
 
Akili za hovyo, eti wakati wa china kutufariji waafrika! Kwani mna matatizo gani hadi mfarijiwe? Hamna akili za kujitegemea? Mbonà marekani wanajitegemea? Mkitukanwa ni sawa tuu.

Angalia ni nchi gani zinazoongoza kupokea misaada kutoka Marekani. Tanzania hatupo hata kwenye top 10 duniani.

Hakuna nchi inayoweza KUJITEGEMEA.

Marekani kuna vitu inapata kutoka kwetu and vice versa.

Israel, Egypt, Taiwan na South Korea zote zinapokea misaada kutoka Marekani.

Jielimishe kabla hujatukana watu
 
Nakuunga mkono ila shida ni hii mkuu, HATUWEZI KUJITEGEMEA na tangu Afrika iwepo HATUJAWAHI KUJITEGEMEA.

Unaiambiaje nchi ambayo hata toothpick inaleta kutoka nje ianze KUJITEGEMEA?
Kumbuka hiyo misaada sio sheria ni utashi wao tu.Kama misaada ikiminywa mbona akili zitatukaa sawa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…