Trump kusimamisha misaada duniani ni kosa kubwa la kiufundi. Ni muda wa China na Urusi kuja kutufariji Waafrika

Kwa Nini ukae na bakuli omba omba tu ? Simama imara , chapa kazi kizalendo, ufisadi ni kosa la uhani, uongozi bora . Afrika ni tajiri
 
Huu ujinga kwamba toothpick ni big deal aliuanzisha nani ?
Nchi imejaa viwanda kibao vinavyotengeneza muhimu, nyie mnakuja na comedy zenu za toothpick
Acha wakalie ngonjera. Acha wajiaibishe mtu anakupa msaada kaamua kuacha kukupa msaada ambao sio haki yako unaanza kuleta umbea wa kitoto
 
Huwelewi hata unacho kiongea,niambie ni msaada gani ambao S.korea inaupokea kutoka Marekani?
S.korea ndo inayo ilipa Marekani kwa ajili ya kuilinda dhidi ya N.korea.
Misri haipokei msaada bali pesa anazo pokea ni kama malipo ya yeye kukubali kusaini mkataba wa amani kati yake na Israel hivyo kukata hizo pesa ni kuvunja vipengele vya mkataba huo.

Israel ni kijitaasisi cha Marekani kilicho jivika vazi la nchi hapo mashariki ya kati ,hivyo Marekani hatoi msaada bali anaihudumia taasisi yake ili kulinda masilahi yake.
 
Unaijua MAGA mkuu, jamaa anataka kuirudisha marekani kuwa baba wa dunia sio kiranja tena.

Jamaa anakata mirija kila kona ya dunia sio Africa tu, mipango yake ni kabambe sana.

Umoja wa ulaya kawatekenya kidogo tu wanalia lia kama mashoga sasa ivi, kawaambia wajitegemee hakuna bakuli tena,

Katika vita ya Ukraine, marekani alikua anachangia zaidi ya asilimia 60 wakati umoja wa ulaya(nchi 27) walikua wanachangia 40, sasa kawaambia komaeni wenyewe kwenye mambo yenu.

Elon kazi yake ni kuzichokoza serikali tofauti kupitia mtandao wake wa X halafu jamaa anamaliza kazi.

Kwa kifupi chaguzi nyingi za dunia, X lazima itumike kuleta matokeo ndio maana nchi nyingi wanataka kuifungia.

Pale UK za ndaaaani zinasema wanataka kumpa nchi Andrew tate awe pm, na tayari ameshaanzisha chama chake mtandaoni kupitia X kinaitwa BRUV,

Sweden wameanza kufundisha raia wao kama vita ikitokea wanajipangaje wameshajua hali sio nzuri, ulaya lazima ijitegemee.


X ni mtandao utakaotumika kuangusha serekali nyingi sana duniani, hata hapa bongo wasipoangalia itaacha makovu sana kwenye huu uchaguzi.
 
Ni wakati wa kujifunza kusimama wenyewe kama nchi.Kuwa na uhakika wa kupewa misaada kunapelekea kutokuwepo na nidhamu ya fedha huko serikalini
Nahisi hata mama alishausoma huu upepo,kuna kipindi nilimuona China,hii ilikuwa idea nzuri sana.Nchi za maghatibi kwenye vita ya Ukraine na iIsrael zimeumia sana kiuchumi,sasa katika kutapatapa ndio zinakuja na hii idea ya kupunguza misaada...
 
Wacha kuwa ombaomba, utatawaliwa maisha yako mpaka wajukuu zako.

Ondokana na fikra za kijinga.
 
Fresh tu kwani lazima misaada.
Misaada yenyewe wanakula FISIEM tu
 
Hiyo Marekani ikipoteza influence yake itajijua yenyewe ni wakati wa sisi kujitegemea. Hata hivyo siyo rahisi kwa Marekani kupoteza influence yake duniani kumbuka yeye ndo mfadhili mkubwa wa IMF, World Bank na UN.
 
Sasa utajiri wake sisi unatuhusu nini?

Unahisi amechaguliwa kwa sababu ya utajiri?
Acha kuwapangia watu maisha. Wachina ndio wanatuibia fedha nyingi kila siku na tenda wanazopata kwa hongo na kuishia kujenga barabara zisizo na viwango.
 
Wamarekani weusi wa Ifakara na Tandahimba si kila siku hua wanasema humu kua US inaendeshwa na mfumo na sio Rais?


Trump kaingia tu kaifungulia Tik tok,kakata misaada,anataka kukata Birthright citizenship,na mabadiliko kibao.
🤣🤣🤣 Wanasemaga ni nchi inayo ongozwa Kwa mifumo ya kisheria wakati Tunaona trump now anaiongoza nchi Kwa matamko
 
Yaani badala ya kuwaza kujitegemea, tunashupaza shingo kulalamikia misaada!!! Rasilimali za kutosha kabisa tunazo! Viongozi wakiwa waadilifu tunaweza kujitegemea! Fikiria, idadi ya viongozi wanaotumia magari ya thamani kubwa, wangekuwa na magari ya kawaida hiyo hela si ingeboresha huduma za jamii? Piga picha anakujia mtu nadhifu kabisa, kavaa suti ya bei ghali, halafu akwambie ana njaa anaomba umsaide hela ya kula! Utamuonaje mtu huyo?
 
Cpt. Ibrahim traore alishajiengua mapema sana. Burkinafaso partner wake ni Russia na sio hao waeneza ushoga
 
Kinachoendelea mpaka sasa duniani ni uhalisia wa msemo wa wabongo "KICHAA KAPEWA LUNGU"
Yaani ni kumechangamka mnooo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…