Trump: Nchi za BRICS zenye mpango wa kuikwepa Dola ya Marekani zitakumbana na ushuru wa asilimia 100, Wanaweza kwenda kutafuta “mjinga” mwingine

Trump: Nchi za BRICS zenye mpango wa kuikwepa Dola ya Marekani zitakumbana na ushuru wa asilimia 100, Wanaweza kwenda kutafuta “mjinga” mwingine

Waambie wewe kiazi, mimi mhogo nitaambiwa nina mizizi. Wao wanadhani hizi ''takataka'' za mchina zinazokuja Afrika ndizo zinakuza uchumi wa China. Soko la mchini liko kwenye mataifa yaliyoendelea na wakiamua kumkomesha wanaweza.
Kwani mwaka 2018 Trump alipo pandisha ushuru china aliathirika kwa kitu gani?
 
BRICS ni upuuzi ulioshindwa kabla ya kuanza. Nchi za Africa zilizokimbilia BRICS hata hazikuwa zinaelewa BRICS ni nini, zenyewe zilijua ni shirika jipya la kutoa misaada😀
Yaani Trump yupo anatokwa na povu kwa ajili ya BRICS alafu ww mhehe unasema hamna kitu.
Hivi wtz akili mlisha zipeleka wapi?
 
Trump ni mwendawazimu atakaye harakisha zaidi anguko la marekani.
MJINGA. Donald Trump aliwahi kusema " Changamto ya dunia ya sasa ni kwamba wenye AKILI wanajitenga na siasa na kuwaacha WAJINGA wafanye maamuzi ya kila kitu juu ya maisha ya wajinga na wenye akili. Anguko la Marekani litakuwa ni kusambaratika kama ilivyokuwa USSR na ndicho anachokitamani Putin kitokee kabla hajafa.
 
Juzi wamezindua simu yenye teknolojia kali huku kila kitu wakitegemea toka nchini kwao.

Na wamemtoa kimauzo I phone homeground jambo ambalo halikutegenewa.

Unataka maelezo zaidi ?
Inatosha mzee ushamtafunia unataka na umlishe pia kama hataweza kumeza mwenyewe basi tena
 
Waambie wewe kiazi, mimi mhogo nitaambiwa nina mizizi. Wao wanadhani hizi ''takataka'' za mchina zinazokuja Afrika ndizo zinakuza uchumi wa China. Soko la mchini liko kwenye mataifa yaliyoendelea na wakiamua kumkomesha wanaweza.
Wataamua lini maana China kua hapo ilipo sio bahati mbaya na haijatoka kwa ghafla
 
Muhanha hapa atakuwa mzee Putty mwenye kiburi Cha kijinga huku uchumiwa wao ukiendelea kupekechwa taratibu Kwa vikwazo lukuki.

Mchina mwenye machoadogo ni mjanja.

Ukimpeleka Kwa waliokodoa hayupo na Kwa waliofumba macho nako hayupo😆😆😆

Yaani ni ndumi la kuwili
😄😄
 
They can find another SUCKER
hili li potus linamaneno ya kujiamini na kukera.

MAGA
20241201_105212.jpg
 
Labda watu wamekuwa wajinga kupindukia au uwezo wangu wa kufikiria umeporomoka beyond reasonable doubts.

Marekani ni nchi iliyoendelea, hivyo ni nchi yenye viwanda vya karibia kila bidhaa wao wanaitengeneza. Hili linamfanya USA kuhitaji raw materials nyingi kuliko finished products ili aweze kuvisustain viwanda vyake. Juu ya yote, hakuna bidhaa inayoongaza kuuzwa na Marekani kama shilingi yake.

BRICS inataka kuanza kuuza bidhaa zao kwa shilingi zao, sio tena dollar. Mfano, vitu vyote China anavyoviuza nje, basi analipwa kwa dollar, vyote anavyonunua alinapa kwa dollar. Ina maana biashara zote za mchina malipo yake ni dollar. Kama mchina akiamua kuanza kuuza bidhaa zake kwa yuan, inamaanisha nchi zote duniani zitakazotaka kufanya biashara n mchina itabidi zinunue Chinese yuan kwanza, ndio zikanunue bidhaa za kichina.

Ukizingatia mchina anafanya biashara na takriban Dunia nzima, basi Dunia nzima itabidi inunue pesa ya mchina*yuan kwanza badala ya dola ndio iendeleze biashara n mchina. Hili litainufaisha China kuliko maelezo, maana bidhaa yake kuu itakuwa ni pesa ya China, ndio bidhaa nyingine zifuate.

USA n mchina hakuna anayemtegemea mwenzie 100%, Ina wote wanategemeana, haswa USA anamtegemea mchina zaidi. ¹Anahitaji mchina auze na anunue kutumia dola, ² analihitaji soko la kichina linunue bidhaa zake ghali na ³anahitaji mchina amuuzie malighafi ili viwanda vyake visife. Mchina analihitaji soko la bwanyenye la usa tu ili aweze kuziuza bidhaa zake USA.

Hapo nimemtumia mchina kama mfano. Ila kumbukeni tunaiongelea brics nzima. USA inaihitaji brics kuliko brics inavyomhitaji. Maana dhumuni kuu la kuundwa kwa brics ni kuunda soko kubwa (nchi wanachama zitegemeane kimasoko) ili ziweze kulipotezea soko la USA.

Kwa sasa USA ananunua gesi n mafuta ya mrusi kwa rubbles. Na huu ni mwanzo tu, sasa itakuwa brics nzima. Hii nchi zitaendelea n kupiga hatua bila ya USA kuliko hata alipokuwepo. USA amewapa soko la Bure, ila anawanyonya kupita maelezo. Kama mnavyojua, mfa maji haishi kutapatapa. Hivyo USA anguko lake sasa rasmi limefika. Potelea mbali *****, skuizi watu sio washenzi kama zamani. Putin ndio anguko la USA rasmi. Ndio maana USA yupo tayari kutumia matrilioni ya dola za kimarekani kumuondoa putin kwenye uso wa Dunia lakini hawezi. Juu ya yote, kumbukeni kauli mbiu ya brics ni kuzisaidia nchi wanachama kukuwa kiuchumi na sio kuendelea kumsaidia USA aendelee kuwa tajiri hasi duniani. Aishi maisha marefu putin, Aishi maisha marefu putin. Tunaihitaji Dunia bila mashoga.
Uzi ufungwe maana kama chakula basi hii koment ni pilau au biriani
 
ALIWAHI kumpiga biti Emanuel Macron wa ufaransa ambae alijaribu kuongezea ushuru kwa bidhaa za US zinazoinhis france...alimpa warning kwa kumpigia simu kwamba anapandisha ushuru kwa 100% na anafanya kwel...Macron alinyanyua mikono juu na kufanya kama Trump anavyosema .. Trump atafanya hivyo na mchina ambae soko lake kubwa ni America atanyoosha mikono juu. Hata muhindi ambae ni rafiki mkubwa wa marekani atasimama nae.... BRICS wataanzisha sarafu Yao sawa lkn hawataacha dollar na hawataipiki dollar..na Kila biashara huko America watafanya kwa dollar...ilianzishwa Euro kwani imeifanya nini dollar??
Euro haikuanzishwa kama mbadala wa dola au hili hulijui na ndio maana hakuna siku marekani aliipigia kelele hio Euro
 
View attachment 3166300

BRICS = Brazi, Russia, India, China, South Africa

Kaandika kwenye ukurasa wake wa Twitter

Wazo kwamba nchi za BRICS zinajaribu kuachana na Dola ya Marekani huku tumekaa na kuwatazama LIMEKWISHA! Tunahitaji ahadi kutoka kwa nchi hizi kwamba hawataunda Sarafu mpya ya BRICS, wala kuunga mkono sarafu nyingine yoyote kuchukua nafasi Dola ya Marekani yenye nguvu duniani, vinginevyo zitakumbana na ushuru wa asilimia 100 kwenye bidhaa wanazoingiza na zijiandae kuaga kuuza kwenye uchumi ulionona wa Marekani. Wanaweza kwenda kutafuta “mjinga” mwingine! BRICS haiwezi kuchukua nafasi ya Dola ya Marekani katika Biashara ya Kimataifa, na nchi yoyote itakayojaribu inapaswa kuaga Marekani !

The idea that the BRICS Countries are trying to move away from the Dollar while we stand by and watch is OVER. We require a commitment from these Countries that they will neither create a new BRICS Currency, nor back any other Currency to replace the mighty U.S. Dollar or, they will face 100% Tariffs, and should expect to say goodbye to selling into the wonderful U.S. Economy. They can go find another “sucker!” There is no chance that the BRICS will replace the U.S. Dollar in International Trade, and any Country that tries should wave goodbye to America.​
Huyu jamaa kweli mwamba,kaanzia palepale walipomkatizia,ananyoosha rula...
 
Ukipandisha ushuru watakao umia ni watumiaji wa mwisho wa nchini kwako.

Kafuatilie trade war ya marekani na China 2018 Trump hajaanza kuwa mwendawazimu leo.

Uzuri ana deal na mataifa yenye akili yanayo nufahika na upumbavu wake.
Kwani bro wangu mo energy ikipandishwa ushuru na samia ikaanza kuuzwa elef tano Kisha wewe ukaacha kuitumia baada ya bei kuwa sana ukaanza kunywa jambo energy ambaye atakuwa ameathilika hapo ni nani? Ni wewe mnywaji ambaye kwa sasa unatumia jambo energy au mo dewj ambaye atakuwa kakupoteza wewe mteja wake

Jambo Mbona liko wazi kabisa bro
 
Ndio ukweli, hii ni vita ya maslahi na hamna mtu atakubali kupoteza alichojijengea tayari kwa ajili ya kujenga kipya ambacho kwanza hana hata uhakika kama kitafanikiwa! Na tusasahau hii miungano inavunjwa kwa divide and rule!
Na hapa ndio munapokosea au tunapokosea sisi waafrika kwa kudhania kwamba watu hua wanapenda kuporomoka hasa hao superior pia kudhania ama kuwa na mawazo eti huna hakika kama itakua fanya isipokua unakua umejaribu ikiwa umetoboa nyie kaeni tu brics ishatoa nanga
 
Kwani bro wangu mo energy ikipandishwa ushuru na samia ikaanza kuuzwa elef tano Kisha wewe ukaacha kuitumia baada ya bei kuwa sana ukaanza kunywa jambo energy ambaye atakuwa ameathilika hapo ni nani? Ni wewe mnywaji ambaye kwa sasa unatumia jambo energy au mo dewj ambaye atakuwa kakupoteza wewe mteja wake

Jambo Mbona liko wazi kabisa bro
Nauli zilipandishwa bei hapo dar vipi watu waliacha kupanda magari kwasasa wanatembea kwa miguu tokea mbagala mpaka kkoo au waliamua tu kwenda nayo hio hio hali yakua wanaumia
 
Na hapa ndio munapokosea au tunapokosea sisi waafrika kwa kudhania kwamba watu hua wanapenda kuporomoka hasa hao superior pia kudhania ama kuwa na mawazo eti huna hakika kama itakua fanya isipokua unakua umejaribu ikiwa umetoboa nyie kaeni tu brics ishatoa nanga
Tusubiri kama tutakua hai!
 
Back
Top Bottom