Tatizo hujui
TAtizo hujui nguvu ya uchumi wa China ipo wapi, na nini kimejenga uchumi wa China.
Hivi unajua kuwa makampuni yote yanayotengenezea bidhaa China na kupeleka masoko ya Ukaya na America, ni makampuni ya Wamarekani wenyewe na nchi za Ulaya?
Hivi unajua kuwa baada ya uchumi wa China kudorora kwa muda mrefu, na China kuamua kuachana na uchumi wa kijamaa, iliziangukia nchi za Ulaya na America, na ndipo mataifa hayo yakawekeza heavily nchini China? Baada ya makampuni hayo ya Ulaya na America kuwekeza sana nchini China, uchumi wa China ulikua mpaka kufikia 12% kwa mwaka?
Hivi unajua kuwa wakati wote viongozi wa China wapo Ulaya na America kutafuta wawekezaji?
Unajua kuwa China ndiyo inayoongoza kwa kuvutia wawekezaji wengi Duniani? Wakati sisi tunawategemea sana wachina kuwekeza, kwao wanahangaika kuvutia wawekezaji. Kwa mwaka China inavutia mitaji inayofikia zaidi ya dollar bilioni 90. China kwenye suala la uchumi, huwezi kuishawishi chochote. Marekani na nchi za Ulaya, zikiweka tarrif ya 100% bidhaa za kutoka China, itakuwa ni sawa na kuyaambia makampuni ya Ulaya na America, zaidi ya milioni 1 yanayotengenezea bidhaa nchini China lakini soko laker likiwa Ulaya na Ametica, yahamishe mitaji yao kutoka China, kitu ambacho China haiwezi kukubali.
Kumbuka pia kuwa China ndiyo nchi pekee Duniani yenye akiba kubwa ya dollar nchini Marekani. Kama dollar itapoteza thamani yake maana yake ni lazima na China iathirike.